MeinKempf
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 11,092
- 7,235
Bibi harusi mmoja ajulikanae kama dorothy Msuya amezua gumzo la kufungia mwaka 2015 kwa wakazi wa Moshi na vitongoji vyake baada ya kutokomea mazingira yasiyojulikana saa chache kabla ya harusi yake na Bw Joseph Mchange .
Vyanzo nyeti sana vinadai kuwa Bi.Dorothy alitokomea mazingira yasiyojulikana mida ya saa 6:30 wakati aalipokuwa amekwenda saluni kuandaliwa, ilidaiwa aliaga anaenda chooni, lakini toka alipoenda chooni hakuweza kurudi tena saluni hali iliyompa wasiwasi msaidizi wake aliyekuwa naye akipambwa, kwania alihisi labda bibi harusi mtarajiwa alipatwa na tumbo la kuhara damu au alipigwa na jini akaanguka huko huko chooni, hivyo ilibidi amtimbie mazima huko toi ili kujiridhisha
lakini vyanzo nyeti na makini vilidai kuwa bibi harusi mtarajiwa alipofika chooni aliruka ukuta wa choo (HUKU AKIWA KAVAA GAUNI LAKE - SHERA JEUPE LA HARUSI) na kuchukua boda boda ya fasta fasta na kisha kupotea mazingira ya kutatanisha kusipojulikana , kiasi kwamba mpaka ninapokuletea habari hii hajapatikana Moshi nzima, Marangu, Himo, Mwika licha ya msako mkali wa askari wa kikosi cha miavuli (i.e wadau waliojitolea kumsaka kwa udi na uvumba either dead or alive).
Inadaiwa kuwa bibi harusi huyo mtarajiwa ni msomi wa shahada ya pili katika elimu (Masters Degree of Education)
na mumewe mtarajiwa ni mwalimu mwenye shahada ya kwanza (Bachelor degree of Education).
Ghrama za maandalizi ya hiyo harusi ilikuwa ni zaidi ya Tsh. 7 Million, Siku mbili kabla ya hapo ilifanyika sherehe ya kumuaga bibi harusi mtarajiwa ( send -off). Na bibi ahrusi mtarajiwa alikuwa ni mwenye furaha na mchangafu sana hasa ule muda wa kwenda
kumsaka mumewe mtarajiwa ulipowadia , alifanya hivyo kwa bashasha sana kiasi cha kuacha gumzo kuu kwa waliohudhuria send off hiyo.
Baada ya juhudi za kumsaka kwa udi na uvumba kushindikana hata baada ya kutmia askari wa kikosi cha miavuli , ilibidi taarifa ya kupotea kwake itolewe kanisani hapo ambapo wazazi na ndugu wa pande zote mbili walikuwa wakisubiria kwa hamu kushudia tukio hilo hadhimu katika maisha ya watoto zao.
Mchungaji aliyetakiwa kufungisha ndoa hiyo , mchungaji Rodrick Mlay aliwaomba radhi wahudhuriaji na wana kwaya na hivyo kupelekea kuhairishwa tukio hilo.until further notice.
Utata pia uliendelea hadi ukumbini ambapo kila muda MC wa sherehe hiyo Bw. Willium Ngalo alipokuwa anaendelea kuwasihi wahudhuriaji kuwa wavumilivu kwani wahusika (maharusi ) watawasili muda si mrefu, lakinio hadi kufikika saa tatu kamili usiku ilikuwa isha thibitika kuwa (confirmed ) kwamba hakutakuwa na sherehe tena, hivyo aliwabebembeleza watu waliohudhuria kula kile chakula kibishi hivyo hivyo kwani tayari kilikuwa kisha andaliwa kwaajili yao.
Baadae Bwana Harusi mtarajiwa na baba yake mzazi walienda hadi kituo cha polisi kufungua mashitaka, ila kukatokea utata mwingine
juu ya aina la jalada la malalamiko husika, kwani hiyo ilikuwa ni ishu ya aina yake kuwahi kupata kuripotiwa kituoni hapo.
UPDATE ZA BIBI HARUSI ALIYEPOTEA MAZINGIRA YA KUTATANISHA :
HATIMAYE KAPATIKANA MKOA WA JIRANI (R-CHUGA) NA HIVI SASA
KALAZWA SELIAN HOSPITAL CHINI YA UANGALIZI WA KARIBU SANA
(INTENSIVE CARE UNITY) -HIYO NI BAADA YA KUPOTEA KUANZIA
JUMAMOSI YA TAR 7 NOV 2015-TAR 10 NOV ,2015.
Ni yule Bi harusi aliyetoroka akiwa saloon sasa amepatikana mkoani Arusha, na hali yake haikuwa nzuri alikuwa anaweweseka, habari zinadi kwamba anapatiwa matibabu Selian hospital, Doroth Msuya ( Kulia )
Moshi. Bibi harusi Doroth Msuya aliyetoroka saluni akipambwa saa tatu kabla ya kufungwa kwa harusi yao na kumwacha solemba bwana harusi, Joseph Machange amepatikana jijini Arusha.
Polisi mkoani Kilimanjaro imesema binti huyo hakutekwa nyara kama ambavyo wanafamilia walitoa taarifa Kituo cha Polisi Himo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema jana kuwa uchunguzi uliofanywa umethibitisha kuwa bibi harusi huyo hakuwa ametekwa nyara. Polisi walifungua jalada la uchunguzi na ilibainika kuwa taarifa za kutekwa zilizokuwa zimetolewa hazikuwa na ukweli, bali aliondoka kwa kupanda pikipiki, alisema.
Kamanda Ngonyani alisema uchunguzi huo ulibaini kuwa wakati akipambwa, aliomba kwenda kujisaidia na baadaye kuomba apelekewe kanga na tishu lakini akatumia mwanya huo kuondoka, alisema.
Alisema uchunguzi huo umebaini kuwa baada ya kupanda pikipiki ilimpeleka hadi kituo cha mabasi na alimlipa dereva wa bodaboda kisha alipanda gari la abiria lililompeleka hadi mjini Moshi.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita saa 6.30 mchana eneo la Lole huko Mwika, Moshi wakati bibi harusi huyo alipotoroka saluni akimwacha mpambe wake akiendelea kupambwa.
Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe saa tisa alasiri katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Lole Dayosisi ya Kaskazini na baadaye sherehe ingefanyika katika Ukumbi wa Mamba Complex.
Habari zilizopatikana jana kutoka kwa familia ya Machange, zilieleza kuwa Doroth alipatikana juzi baada ya kuonekana akiweweseka kama yule "jeshi wa kwenye mkanda wa YESU , na hivyo kupelekea kufungwa kamba nzito mikononi na miguuni ", kisha akapelekwa hospitali ya Seliani kwa matibabu zaidi ikiwemo kupimwa kama ana dege dege au malaria imepanda kichwani.
Ndugu wa karibu wa familia ya Machange ambaye aliomba jina lake lisitajwe, alisema kulikuwa na kikao kilichokuwa kikiendelea kati ya familia ya Machange na Msuya.
Jana (juzi) tulipigiwa simu na kuelezwa kuwa Doroth amepatikana Arusha lakini yuko kama hajielewielewi na hajui nini kimetokea, Alisema.
Habari zaidi kutoka ndani ya familia hiyo, zinadai kuwa bibi harusi huyo alikuwa ametaka harusi hiyo iahirishwe na ombi hilo alilitoa zaidi ya mara 10 bila kueleza sababu.
Huyu hapa bibi harusi mtarajiwa saa chache kabla ya kutokomea mfichoni
hapo alikuwa na msaidizi wake katika saloon aliyotokomea....