Bibi harusi afariki dunia saa moja kabla ya kufunga ndoa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Bibi harusi afariki dunia saa moja kabla ya kufunga ndoa kanisani, Handeni, Tanga. “Inadaiwa alishajiandaa huku bwana harusi akimsubiri kanisani” Katika hali isiyokuwa ya kawaida, bibi harusi ambaye ni mkazi wa Chanika mjini Handeni, Tanga; Levina Mmasi (23) amefariki dunia saa moja kabla ya ndoa yake kufungwa siku ya jumamosi na hivyo kuilazimu kamati ya maandalizi ya harusi kujigeuza na kuwa kamati ya msiba.
===
Handeni.Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Bibi Harusi ambaye ni mkazi wa Chanika mjini Handeni, Levina Mmasi (23) amefariki dunia saa moja kabla ya ndoa yake kufungwa katika Kanisa la Katoliki la Roma Wilaya Handeni Jumamosi na hivyo kuilazimu kamati ya maandalizi ya harusi kujigeuza na kuwa ya msiba.
Kifo hicho kilichotokea Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita, kimekuwa gumzo mjini Handeni huku wananchi wakisema kuwa ni tukio ambalo halijawahi kutokea katika wilaya hiyo.
Msemaji wa familia ya marehemu aliyejitambulishakwa jina la Firmin Mrimasha,alisema kuwa chanzo cha kifo cha Levina ambaye alijifungua mwanzoni mwa wiki iliyopita,ilikuwa ni homa aliyoipata ghafla siku ya Alhamisi na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya yaHandeni na kukutwa na malaria na kisha kulazwa kwa matibu.
Huyu bibi harusi alikuwa ametoka kujifungua, alikuwa na mtoto wa kiume kutokana na ujauzito wa miezi saba, ndipo ghafla Alhamisi akapata homa tukampeleka hospitali alikolazwa na baada ya kupata nafuu, aliruhusiwa Ijumaa.
Baada ya kuruhusiwa akaanza maandalizi ya harusi na Jumamosi ambayondiyo siku ya ndoa yake, alijiandaa lakini ilipofika saa 8.05 akafariki dunia akiwa nyumbani akisubiriwa kwenda kanisani kufunga ndoa ambayo ilikuwa ifungwe saa 9.00, alisema Mrimasha.
Alisema, Inasikitisha sana ila imeshatokea yaani marehemu amefariki saa moja kabla ya ndoa yake na baada ya kifo hicho, mtoto wake naye alifariki muda mfupi baada ya mama yake kufariki dunia, alisema Mrimasha.
Akizungumzia mkasa huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Harusi hiyo iliyogharimu Sh7.7 milioni, Abdi Kipacha alisema kuwa kwake ni tukio la kwanza kutokea tangu kuzaliwa kwake na kamwe hawezi kulisahau.
Nilishazipangia kazi kamati za maandalizi, lakini ghafla tukapewa taarifa kuwa bibi harusi amefariki...Hatukuamini, ikabidi niwatangazie wanakamati wenzangu kuwa hakuna tena shughuli, bibi harusi amefariki, alisema mwenyekiti huyo wa kamati na kuongeza:
Kitu tulichokuwa tukisubiri ni kuambiwa bibi harusi angefika saa ngapi, lakini ghafla tukapewa taarifa za kifo, ilikuwa ni vigumu kuamini lakini ni kweli imetokea na inasikitisha kwani si jambo la kawaida, alisema Kipacha.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na wanandugu ni kuwa marehemu alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Nndawa mkoani Lindi na kwamba alikuwa katika kundi la walimu wa ajira mpya ambayo hadi mauti yanamkuta alikuwa hajapokea hata mshahara wake wa awali.
Akizungumzia hali hiyo, Padri aliyekuwa afungishe ndoa hiyo, Max Sabuni wa kanisa hilo Katoliki Handeni alisema: Nimesikitishwana tukio hili kwa kuwa halikuwahi kunitokea...Kilichobaki ni wanandugu kuwa watulivu kwa kuwa Mungu amechukua kiumbe wake kwa muda alioupanga.
Aliwataka ndugu, jamaa na marafiki kuwa na subira katika kipindi hiki cha majonzi.
Naye mume wa marehemu, Kasisi Masawe alisema: Nimechanganyikiwa sana na hili...Ni jambo ambalo sikulitarajia. Ninamshukuru Mungu kwa yote japokuwa kifo hiki kimeniharibia mipango yangu mingi ya maisha na Levina.
Nilipanga mengi na yeye, lakini Mungu hakupenda...Nilimpenda sana Levina,leo ameniacha. Amekwenda na mwanangu...Ni pigo kubwa kwa kweli, mke na mtoto kwa wakati mmoja, inauma sana.
Mwili wa bibi harusi huyo ulisafirishwa jana kupelekwa Machame mkoani Kilimanjaro kwa maziko ambayo yanafanyikaleo Jumatano pamoja na mtoto wake ambaye naye alifariki saa chache baada yamama yake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alithibitisha kutokea tukio hilo lakini akasema hawezi kuzungumzia kwa undani kwa kuwa ni tukio la kifamilia zaidi.

Chanzo: MCL
 
Pole sana Mume mtarajiwa na familia nzima!

Vyombo vya usalama vishughlikie swala hili na kuleta matokeo yake mara moja! so saaD!:embarrassed1:
 
Mungu hakupenda. Rest in Peace Bibi Harusi mtarajiwa.
 
duu imeniuma utafikiri ndie mimi, poleni sana wafiwa hasa bwana harusi
 
Poleni sana wafiwa ..hili tukio la aina yake
Au bibi harusi alikuwa na BP?
 

This is "specially made in Tanga only". Hawa rafiki zangu wadigo, wasaa-mbaya (wasambaa) kuna haja kubwa ya kuwaomba wachungaji wetu watuwezeshe ili tuwafanyie mkakati maalum tuwavune waje kwa Yesu. Kuna haja pia ya kuwahamasisha wachungaji wetu wajiunge na forum hii, maana naona kama tunaye mchungaji mmoja tu Peter Msigwa. Au kuna wengine? Kama wapo tafadhali naomba kama wanaweza kujitambulisha itakuwa nzuri. Kabisa hawa wadigo wanahitaji msaada wa kiroho,tena mkubwa mno.
 
Pole sana Mume mtarajiwa na familia nzima!

Vyombo vya usalama vishughlikie swala hili na kuleta matokeo yake mara moja! so saaD!:embarrassed1:

kama vitaweza kumchunguza na mungu vitakuwa vimefaulu mtihani
 
Tragedy!!! Pumzika kwa amani bi harusi. Mungu amjalie bwana harusi aweze kusonga mbele na maisha
 
So sad!! What a unfortunate day for the groom to be!
 

Hata mama rwakatare yupo humu mkuu, si unakumbuka aliisha wahi kusema kitu kule bungeni juu ya huu mtandao wa JF?
 
poleni wafiwa..kama ni mkazi wa handeni mbona anaenda kuzikwa moshi-machame?
 
Makanyaga watch your words usilete upuuzi humu ndani unavyotaja makabila na ku associate kifo cha mtu unamaana wewe ndo Mungu au?Wewe sijui dini gani usieelewa kua Mungu pekee ndiye anae toa uhai na kuuchua tena UOMBE RADHI KWA MAKABILA ULIYOYATAJA......YESU unaetaka utuvune utupeleke kwake tunamjua na ametuokoa kuliko wewe coz yeye haangalii kabila wala mkoa.Na utubu pia kwa imani yako.umeniudhi sana n SHAME on YOU.
Ingetolewa mada ya mapenzi hapa ungeshashadadia wanawake wa Tanga.....Think before u do anything stupid.
 

Tena wewe ndo wale wachawi kwenye misiba watu wanauchungu wanaomboleza mnaanza kutunga stori za uongo muonekane wajuaji mara oooh bibi harusi alisema usiku anaskia anaitwa mara oooh bibi harusi aliambiwa hiki mara kile.....Upumbavu tu sijui unafikiria na mata...o!!!!
 
Mitihani ya maisha. Ni muhimu kuhesabu baraka zako hata kama unapitia magumu.
Hapa bila Mungu kuhusika mwenyewe, sijui! Poleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…