Biashara yangu imefungwa

nelvine

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2015
Posts
1,114
Reaction score
1,879
Habarini wana jamvi, nisiwachoshe sana niende moja kwa moja kwenye point.

Ninamiliki kabiashara kangu hapa mtaani, jana wakapita watu wa Halmashauri wanakusanya hela za leseni za biashara kwa bahati nikawa sipo, ajabu leo wamekuja wamefunga duka langu wakati nina kitambulisho cha Rais cha wafanyabiashara wadogo.

Nimewauliza wanasema havifanyi kazi, hivi na hii corona na uchumi wetu huu napewa siku mbili nilipe 150,000 kweli?

Kiukweli maisha haya kwangu yanakuwa magumu kweli aiseee.
 
Nenda kaongee nao ofic kwao eleza azingira ya biasha na nk au nenda kwa afisa biasaha mwambie ataka leseni eleza biasha yako atakupa fomu ya kupeleka tra kuomba lesen pale utaeleza biasha yako mtani nk wakijuambia bei kubwa waambie wake wakague biashara maana leseni unaweza fika kama 50-100000 kutokan na maelezo na biashara yenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TRA ndio pasua kichwa hawana huruma wale watu.
Wamenilazimisha kodi kulipa wakayi mauzo hakuna kabisa. Mpka nikawa natoa hela mfukoni nilipe kodi.
Si a hamu na serikali ya awamu ya 5.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waambie kama wao wanaona kujiajiri rahisi waambie waende waache hivyo vibarua vyao waone taabu yake kama hawatapakatwa.!
Biashara ngumu kodi ipo juu.!
 
Usilipe hiyo hela nenda TRA ukapate ufafanuzi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kuna siku niko tra nakakadiriwa biashara yangu. Nikalia lia kinoma jamaa kanipunguzia mpk kiwango cha chini. Kuna usemi mkono mtupu haulambwi sijui maana yake nn mtanieleza maana sikwenda shule nimeishia la kwamza D.
Baasi bhana nimekaa pale akaja kijana wawatu maskini wa Mungu 😭😭 ana saloon yake sijui mbagala huko sijui wapi ndani ndani dahh😭😭 jamaa kamkadiria dogo kamuandikia laki 2 kwa mwaka. Dogo kashika ile karatasi nguvu za kiume zilimuishia halafu lijamaa la tra linapiga next.... Yaani aje mwingine.
I'm pretty sure serekali watapata sifuri kwa yule dogo. Kaji saloon tu ndani ndani mtu kaamua akalete tra then hata huna huruma???!!! Sasa si bora hata umwandikie dogo laki kwa mwaka aisee kuliko kuambulia sufuri.
Dogo akisikia tra mnapita siku hiyo KMMK anafunga duka mashetani mpite hivi 👈 then mkishapita anafungua geti. Hopeless government kabisa.
 


Inaumiza Sana...inauma mno....
 
Kazini mizinguo na kujiajiri bado ni ishu?
Tra wana kodi za kijinga Sana! Ndo maana watu wakipat machocho ya mishe haramu wanafanya .....sijui tu watunwakimbilie wapi..sema watz tumezoea shida...kulalamika tu yanaisha maisha yanasonga
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…