Naomba kufahamishwa kuhusu leseni ya biashara

Naomba kufahamishwa kuhusu leseni ya biashara

Rockefeller

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2016
Posts
1,236
Reaction score
2,365
Habari za mida wakuu!

Kwenye side hustle yangu hapa mjini leo wamekuja ma afisa biashara kutoka kituo cha mapato manispaa, walitaka kuona leseni ya biashara sasa mimi sikuwepo kuna chalii anashinda hapo nimerudi nimekuta wameacha form ya mashtaka kwamba nimekiri kwenda kinyume na sheria za biashara Na: 25 (17a-h), nina kosa la kufanya biashara bila leseni na afisa biashara kaamuru nilipe 226,000 ambayo ada ni 100,000 + 1000 ya fomu + 25,000 ya Penalty + 100,000 ya faini na nitakiwa kufika katika ofisi za kituo kidogo cha mapato.

Maswali yangu:

1. Ni nini hiki? Sielewi!!!!
2. Naombeni maoni juu ya mchanganuo wa hiyo fedha nilioambiwa nilipe.
3. Je ni sawa kujaziwa fomu ya mashtaka moja moja what if leseni ninayo?
4. Naombeni msaada jinsi ya kupata leseni ya biashara (kweli sina[emoji847][emoji28]). Sikupata muda kufuatilia by the way ni biashara ndogo tu

Natanguliza shukrani
 
Nenda kwa mfanyabiashara wa jiran yako mwenye leseni akupe ABC then watimbie hukohuko bonga nao watakupa leseni bila hayo ma faini
 
Back
Top Bottom