Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Kama tulidhani suala la biashara ya kusafirisha binadamu na wahamiaji haramu ni tatizo dogo, basi tumekosea, kwa sababu tayari 'wakubwa' wamekiri kuwa biashara hiyo ni kubwa zaidi kuliko hata ile ya uuzaji wa silaha pamoja na dawa za kulevya.
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Czech, Martin Stropnicky, anasema biashara hiyo ya kuwaingiza wahamiaji haramu katika nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) inazidi kwa mbali biashara zote chafu akisema hana imani kama Uturuki na Ugiriki zina uwezo wa kuivunja mitandao haramu ya magendo na usafirishaji binadamu.
“Kiwango cha biashara inayohusisha usafirishaji wa wahamiaji haramu barani Ulaya ni kikubwa mno, mapato yake ya jumla yanazidi kwa mbali sana mapato ya dawa za kulevya na uuazaji haramu wa silaha, wanatengeneza - bila kuongeza chumvi - mabilioni ya dola," alisema Martin Stropnicky.
Taasisi ya Frontex inayojihusisha na masuala ya mipaka kwenye nchi za Jumuiya ya Ulaya inakadiria kwamba mitandao haramu ya kusafirisha binadamu iliingiza zaidi ya euro bilioni 4 (Dola 4.45 bilioni) kwa biashara hiyo mwaka 2015 pekee, huku mapato yao makubwa yakitokana na usafirishaji wa wahamiaji haramu. Mapato hayo ndiyo baadaye yanatumika kufadhili biashara ya dawa za kulevya pamoja na biashara haramu ya silaha.
Wakati zaidi ya wahamiaji haramu 1.83 milioni waliingia kwenye Jumuiya ya Ulaya mwaka 2015, kwa mujibu wa Frontex, Stropnicky anaeleza wasiwasi wake uwezo wa Uturuki na Ugiriki kukomesha ama kukabiliana na ongezeko kubwa la wahamiaji haramu.
‘Enormous business’: Criminal refugee smuggling bigger than guns & drugs – Czech defense minister
=======
NB: Afrika, hususan Tanzania, tumejipangaje kukabiliana na biashara hiyo haramu?