kwa-muda
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 2,101
- 5,442
Kuna jambo limenigusa siku ya leo wakati antazama documentary flani inayohusu kupotea kwa msichana mmoja anaitwa Phoenix Coldon alipotea mwaka 2011 huko Missouri USA.
Kupotea kwake kumeacha maswali mengi mpaka leo polisi hawajaweza kujua kama aliamua kuondoka, ama alitekwa, ama aliuzwa kwenye biashara ya kingono ama aliuawa maana mpaka leo hakuna jambo lolote ambalo limeweza kusaidia upelelezi wa kujua ni nini kilitokea.
Lakini kitu pekee ambacho waliweza kugundua ni kwamba dada huyo alikuwa akiishi maisha ya aina mbili ambapo kuna ambao walikuwa wanajua upande mmoja ambao ni mzuri upande wa binti mlokole, mwema, mwenye tabia nzuri, mwanafunzi na kadhalika huku kuna upande wake wa pili ambao alikuwa akijitahidi kuuficha kwa kila namna. Upande huu alikuwa binti aliyekuwa akivuta ngada, alikuwa na simu ya ziada ya kuwasiliana na mpenzi wake mwingine maana alikuwa na mpenzi wake ambaye hata wazazi walikuwa wakimfahamu kumbe alikuwa na mpenzi mwingine tena, alikuwa ni mtu amabye alikuwa amechoshwa na maisha ya kuchungwa na wazazi hasa mama yake wakati alikuwa anajiona ni mtu mzima akiwa na umri wa miaka 23, pia alikuwa anaongopa kuwa kajiandikisha kujiunga na chuo wakati ukweli ni kwamba alikuwa amejiondosha masomoni.
Na jambo la kuvutia zaidi ni kwamba mama yake pia ni muongo muongo kwanza alimwongopea mwana habari kuhusu taarifa nyingi zinazohusiana na kupotea kwa huyu dada, pia alikuwa haoni kama tabia yake ya kutaka kumtawala mwanae kama imechangi mwanae labda kukimbia maana Marekani kuamua kukimbia ukaanza upya siyo kosa hata usipotoa taarifa polisi wakikupata na ukawambia ndiyo nimeamua kukimbia nyumbani na msiwambie nilipo wataambiwa tu mtu wenu yu hai lakini hatuwezi kuwambia alipo.
wazazi wake wametumia pensheni yao yote kuajiri wapelelezi binafsi mpaka wameweka rehani nyumba yao na kushindwa kulipa mkopo hivyo kwa sasa hawana hata nyumba lakini juhudi zao hazija zaa matunda.
Katika kufuatilia kisa hiki ndipo nikagundua kuwa biashara ya umalaya hasa ambapo wasichana wanafanyishwa umalaya kwa kulazimishwa ni kubwa sana nchini Marekani. Kwa takwimu za mwaka 2012 biashara hii ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 32.
Biashara hii ni mashuhuri sana kwa nchi za Ulaya ya Magharibi ambapo wasichana wengi huuzwa na kununuliwa kutoa Asia, Afrika na familia masikini za bara la Ulaya. Pia nchi kama Thailand ni mojawapo ya nchi ambapo kuna biashara kubwa ya kuuza na kununua wakinadada kwa ajili ya kufanya shughuli ya umalaya.
Siyo tu kwamba ni wakina dada wanaouzwa hata vijana wa kiume kuanzia miaka 9 kuendelea mpaka 25. Mdada ambaye ameshafunzwa inamchukua mwaka tu kurudisha ela ambayo mmiliki alitumia kumnunua na akiamua kumuuza anaweza kumuuza mpaka dola za kimarekani 14,000 kwa kuwa anakuwa ashakuwa mzoefu hivyo thamani yake imeongezeka.
Pia inasemakana madada wana namna hii life span yao ni miaka 7 tu kwakuwa ili waendelee kuwatumia uwa wanawapa madawa ya kulevya ambayo yanawaharibu ukichanganya na pombe na shughuli ya kupandwa na mijidume wanakufa haraka.
Pia nikakumbuka kisa kimoja, Kuna rafiki yangu ni foreigner alikuwa na Gf wake mnaijeria ambaye walipoteana miaka mingi, sasa through FB wakakutana mwaka juzi waka connect na kuanza chat, Huyo mdada akamwambia kwa sasa yuko Thailand ana mgahawa akawa anamtaka aende wasadiane kuendeleza biashara jamaa akamwambia hawezi.
Huyo mdada akamwomba basi amtafutie wadada watano toka huku wakafanye kazi kwenye mgahawa, jamaa akatumiwa na ela kabisa dola 7,000. Bila hiyana akawa ashawaandaa wadada ambao ni ndugu wa mkewe maana kaoa mtanzania, siku moja anakuja kushutuliwa na mwenzake ndiye aliye mwambia kuwa huyo Mnaija anahusika na biashara ya human traficking hao wakina dada anaenda kuwauza kwenye biashara ya kujiuza wakifika atawanyanganya passport.
Pia ikanikumbusha tukio lilitoka kumtokea ndugu yangu mmoja kwaka 2007, kuna mmama tena ndugu kabisa alimwambia ndugu yetu wa kike kuwa kunakazi ubarozi wa Tz China amemtafutia, huyo ndugu yetu kusikia hivyo akawa moto akahamia kabisa kwa huyo mmama eti wanafanya mipango y safari, bahati nzuri ni kwamba mzee wetu katembea sana dunia anaijua aliposikia hiyo habari na ajira za ubarozini anazijua na mambo ya dunia anayajua, alilivalia hilo suala njuga kiasi kwamba alimwokoa huyo ndugu yetu ila ndugu yetu alikasirika maana aliona kama vile kabaniwa na mzee ila looking back na mambo yalivyo na kutembea tembea kwa sasa sina shaka yule alikuwa anaenda uzwa tu.
Mabinti kuweni makini mnapoambiwa kuna fursa nje msiende ende tu bila kufanya research.