1.Tafuta eneo ambako maujenzi yanaendelea,
2.Kuwa na Mashine ya umeme na ya mkono (Bambam).
3.Jenga kaofisi kadogo hapo site kwa ajili ya Wateja
4.Tafuta wapigaji wazuri wa tofali na waaminifu.
5.Hakikisha eneo lina Maji ya kutosha ,kwa ajili ya umwagiliaji wa tofali.
6.Anza na angalau na Mtaji wa mifuko 100 ya cement.
7.Simamia upigaji na umwagiliaji Maji tofali wewe mwenyewe
8.Tofali zimwagiliwe kwa siku tatu mfululizo asubuhi na jioni.
9.Wakati huo tafuta mafundi ujenzi ambao unawahakikishia kamisheni pindi waletapo mteja,ambao ni matajiri wanaowajengea.
10.Kua na Daftari la mauzo ili kujua umeuza na ni kiasi gani unatakiwa kuongeza mzigo site.
11.Usiwaamini wafanyakazi ni rahisi kukuibia cement na pia kuchanganya mchanga mwingi
na kuweka cement kidogo ili wakuibie,na mwisho tofali kuwa mbovu (buyu),na ukapoteza Wateja ambao hutaweza kuwarudisha tena.
Hebu pata hiyo kwanza.Halafu nijulishe kama bado upo nikupe ratio ya uchanganyaji.Naogopa kuendelea kumwaga material wakati sina uhakika kama upo