Biashara ya nje ya China yaonesha uhai na uthabiti

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
198
Reaction score
322
Marekani ilitangaza kutoza “ushuru sawia” kwa washirika wake wote wa kibiashara ikiwemo China kwa visingizio mbalimbali, jambo ambalo limeharibu mfumo wa biashara wa pande nyingi duniani. Kutokana na hali hiyo, takwimu za robo ya kwanza ya biashara ya nje ya China zimefuatiliwa sana na jamii ya kimataifa.

Idara kuu ya Forodha ya China hivi karibuni ilitoa takwimu kuhusu hali ya biashara ya nje ya China katika robo ya kwanza ya mwaka huu. Kwa mujibu wa takwimu hizo, thamani ya biashara ya nje ya China katika kipindi hicho ilifikia yuan trilioni 10.3, sawa na dola trilioni 1.4 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 1.3 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

Kati ya biashara hiyo, mauzo ya bidhaa za China kwa nchi za nje yaliongezeka kwa asilimia 6.9. Wakati Marekani inapotishia biashara ya kimataifa kwa kutoza “ushuru sawia”, biashara ya nje ya China imeonesha uhai na uthabiti mkubwa. Kama msemaji wa Idara Kuu wa Forodha ya China Lv Daliang alivyosema, biashara ya nje ya China sasa inakabiliwa na hali ngumu, “lakini anga haitaanguka”.

Kwa upande wa washirika wa kibiashara wa China, China imedumisha biashara tulivu na washirika wake wengi. Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lililozinduliwa zaidi ya miaka kumi iliyopita, hadi sasa limeshirikisha zaidi ya robo tatu ya nchi za dunia na zaidi ya mashirika 30 ya kimataifa. Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ujenzi wa pamoja wa hali ya juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeendelea kukua kwa kina, na kasi ya ukuaji wa biashara kati ya China na nchi zilizojiunga na pendekezo hilo ni asilimia 0.9 zaidi kuliko kiwango cha jumla.

Kati ya nchi tofauti, biashara na nchi za Umoja wa Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) iliongezeka kwa asilimia 7.1, na biashara na nchi tano za Asia ya Kati iliongezeka kwa asilimia 6.9. Mbali na nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, biashara kati ya China na masoko mengine zikiwemo nchi za Ulaya pia iliendelea kwa utulivu.

Kwa upande wa muundo wa biashara ya nje ya China, biashara ya bidhaa za utengenezaji wa vifaa iliongezeka kwa asilimia 7.6 katika robo ya kwanza, ikichukua nusu ya thamani yote ya biashara ya nje ya China. Bidhaa za vifaa zilizotengenezwa nchini China zenye ubora wa juu zinakaribishwa katika soko la kimataifa.

Uhai na uthabiti wa biashara ya nje ya China pia unatokana na mahitaji ya ndani. China ina soko kubwa la ndani kufuatia idadi ya watu bilioni 1.4. Soko hilo sio tu linatoa uungaji mkono wenye nguvu kwa mashirika ya biashara ya nje, bali pia linatoa msukumo kwa uvumbuzi, ili kutengeneza bidhaa bora zaidi.

Kutokana na ongezeko la kipato na uboreshaji wa muundo wa matumizi ya watu nchini China, mahitaji ya soko la ndani la China yameonyesha mwelekeo wa mseto na maendeleo ya hali ya juu, hasa katika sekta mpya, kama vile nishati ya kijani, akili bandia (AI) na huduma za afya. Baada ya kukidhi mahitaji ya soko la ndani, bidhaa mpya zitatolewa kwa masoko ya nje, hali ambayo itahimiza biashara ya nje.

Wakati dunia inakabiliwa zaidi na vitendo vya upande mmoja vya kujilinda kibiashara, China itaendelea kuwa na nia thabiti katika kulinda utandawazi na kuhimiza biashara huria. Kama msemaji wa Idara Kuu ya Forodha wa China alivysema, “anga haitaanguka,” maneno hayo si kama tu yanaonyesha imani kwa biashara ya nje ya China, bali pia yanaonesha imani kwa mustakabali wa biashara ya kimataifa.
 
Usa elite are living in bable they think that they are number one and they can dictate everything
 
Back
Top Bottom