Habari wakuu,
Natumai wote ni wazima. Nimepanga kuanzisha biashara ya kuuza nguo (hasa T-shirts za kiume na kike - Grade 1 A). Lengo langu ni kuanzisha duka lenye muonekano wa kisasa na bidhaa bora kwa vijana wa mjini.
Nahitaji ushauri na mawazo mapya kuhusu mambo yafuatayo:
1. Njia bora ya kuendesha biashara hii ya nguo – hasa kwa wale walio na uzoefu, changamoto gani mmekutana nazo na mnaishindaje?
2. Wapi kuna machimbo mazuri ya kuzinunua hizi nguo za Grade 1 (A)? Sitaki kununua mzigo mzima wa belo, nataka kuchagua nguo moja moja (cherry-pick) ili kuhakikisha ubora.
3. Faida na hasara za kuchagua nguo moja moja kutoka kwenye belo – je, ni bora zaidi kulinganisha na kununua belo nzima?
4. Kama kuna mtu anajua wauzaji wa nguo za grade 1 kwa bei nzuri (Tanzania au hata nje), naomba contact au ushauri.
Niko tayari kujifunza na kushirikiana na yeyote mwenye nia ya biashara.
Ahsanteni sana wakuu. 0787117819