Biashara ya Mgahawa: Maswali, Majibu, Ushauri

nasrimgambo

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
1,858
2,348
Habari wanajamii forums, habari wajasiriamali.

Nafungua uzi huu ili kuleta pamoja wadau sisi wenye maswali kuhusiana na biashara ya mgahawa ama biashara ya chakula, na kuleta pamoja wale wenye uelewa wa biashara hii, mimi nitaandika maswali yangu, mwengine yeyote mwenye maswali nae basi aulize, na wenye majibu msiwe wachoyo mtujibu, ili uzi huu uwe uzi wa faida.
 
Mimi binafsi nataka kufahamu utaribu wa kumlipa mpishi, mathalani wa chipsi, huwa analipwaje, kiasi gani yani?

Jiko lipi linafaa, yani lipi halitii hasara kati ya gesi na la pumba ama mkaa, maana niliwahi msikia mtu akilalamika na jiko la pumba kuwa linamjazia uchafu sehemu ya biashara na mapumba yanaisha kila siku mbili, akanunua jiko la gesi akaanza kulalamiaka ni gharama linaisha haraka, sasa nishati gNi ni sustainable kwa biashara ya chakula?
 
Kwa jiko la chipsi gesi ina unafuu zaidi kwa sababu unaiwasha pale unapotumia tu ukimaliza unaizima. Tofauti na mkaa ambao utalazimika kuiwasha na kuongeza muda wote hata ambapo hupiki ili mradi moto uwepo.

Kuhusu malipo jiko la chips wanalipwa kuanzia 5000 mpaka 10000 inategemea na masaa anayokuwepo kazini, je ana usaidizi au yupo mwenyewe. Ingawa sana sana malipo ni 5000 au 7000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamlipa au anajilipa?

Maana unamuachia biashara wewe haupo inakuaje kiasi atakachokupa kuwa ndicho alichouza?
 
Unamlipa au anajilipa?

Maana unamuachia biashara wewe haupo inakuaje kiasi atakachokupa kuwa ndicho alichouza?
Kwa wabobezi wa kuuza chips wanajua kabisa debe moja la viazi linatoa sahani ngapi. Ukishajua hilo basi hata ukimwachia biashara hautapata shida kujua alichouza na anachokukabidhi ili mradi uwe na ufwatiliaji kwa karibu.

Kuhusu kwenye kumlipa au kujilipa naona yote ni sawa tuu.
 
Back
Top Bottom