Biashara ya mbao Vs Ufugaji wa kuku

TEAM 666

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
3,271
2,000
Habari wana JF.

Nimekuja mbele yenu nikiamini kwenye jukwaa hili nitapata msaada wa biashara hizi mbili kati ya ufugaji wa kuku au biashara ya mbao ipi the best kuanzia kwenye changamoto za soko na utendaji wake usimamizi nk.

Nimekua na sinto fahamu juu ya hizi fursa 2 ipi yenye good future malengo ni kufanya big project.

Ila bado sijapata mwangaza niifanye ipi?

--Kama ufugaji malengo nifuge kuku chotara aina ya Kroilers niwazalishe mwenyewe then wakikua baada ya miezi 5 niwauze I mean vifaranga nitazalisha mwenyewe.

--Kama biashara ya mbao nitanunua chensor nitawaajiri vijana tutakata vibali tutaingia msituni nakuanza kukata mbao.

Nahitaji neno kutoka kwenye wana JF.
 
Sauda

JF-Expert Member
Jun 26, 2018
865
1,000
Umesema Mbao?

Afadhali mkuu ufuge kuku! Ila sasa, ukiamua kufuga kuku, Uache masihara kabisa.
Maana kuku kama leo Ukiwakosea kidogo tu, Kesho asubuhi unakuta "Israil Mtoa Roho" Ameshafanya kazi Yake.
 
lukinga01

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
327
500
Mbao gani? Elezea biashara ya mbao ni za miti ipi? Miti ya kupandwa au miti ya asili? Kama miti ya kupandwa kama jamii ya mi paina hii ni kazi nzuri na ina faida kwa sasa ili mradi ujitafutie masoko ya uhakika ya mbao. Miti hii baadhi ya sehemu imeshuka bei na inalipa kweli kweli tofauti na ilivyokuwa kipindi cha hapo nyuma.
 
worldboss

JF-Expert Member
Jun 30, 2015
1,706

Inahitaji mtaji kiasi gani?
 
WAKUNJOMBE

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
494
500
Karibu makambako,soko kuu la soft wood

Mimi nafanya hii biasha ra,inaliap sana ila kwa hivi karibuni imesuasua kidogo,

Sasa hivi kununu eka moja ya miti ya pine ni cheep sana, maaeneo ya kununua ni Vijij vilivyo ndani ya tarafa ya Lupembe mkoa wa Njombe.
 
Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,682
2,000
Bishara zote hapo juu ni ngumu. Biashara ya mbao nimeona wengi wamejaribu ila wameishia njiani. Biashara ya kufuga hao kuku waliodumaa utahangaika kuwalisha miezi na miezi hawakui. Mpaka waje kufikia ukubwa wa kuuzika, watakuwa wamekwisha kausha mfuko wako.
 
lukinga01

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
327
500
inahitaji mtaji kiasi gani?
Inategemea unataka kufanya biashara ipi kati ya hizi: 1. Kununua miti na kupasua na kuuzia huku huku mashambani 2. Kununua miti kupasua na kusafirisha kwenye masoko ya mbali i mean mijini. Au kununua mbao na kuzisafirisha mijini. Unataka ipi kati ya hizo?
 
worldboss

JF-Expert Member
Jun 30, 2015
1,706
2,000
Inategemea unataka kufanya biashara ipi kati ya hizi: 1. Kununua miti na kupasua na kuuzia huku huku mashambani 2. Kununua miti kupasua na kusafirisha kwenye masoko ya mbali i mean mijini. Au kununua mbao na kuzisafirisha mijini. Unataka ipi kati ya hizo?
2 au 3
 
worldboss

JF-Expert Member
Jun 30, 2015
1,706
2,000
Ok, fanya utafiti kwa kutafuta wanunuzi wa mbao na bei zao, pia nijurishe unategemea kuuzia miji gani nami nikupe bei za mbao na tukadirie nauli kutoka huku mpaka huko. Hii biashara inalipa balaa!
Asante sana mkuu , nikimaliza tafiti nitakujurisha
 
kinywanyuku

JF-Expert Member
Jul 13, 2015
2,807
2,000
Ok, fanya utafiti kwa kutafuta wanunuzi wa mbao na bei zao, pia nijurishe unategemea kuuzia miji gani nami nikupe bei za mbao na tukadirie nauli kutoka huku mpaka huko. Hii biashara inalipa balaa!
mkuu huku dsm mbao mlingoti mwekundu elfu 12, mweupe 10000 na pines elfu nane vp huko shamba nipe bei
 
lukinga01

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
327
500
mkuu huku dsm mbao mlingoti mwekundu elfu 12, mweupe 10000 na pines elfu nane vp huko shamba nipe bei
Acha nikupe bei ya pines mlingoti ntakupa kesho nikisha thibitisha taarifa za uhakika. Ubaya wewe hujaweka mbao kwa vipimo. Mm ntaanzia mbao ndogo kuja kubwa kwa pines: 1*4*12= tshs 900. 2*3*12=tshs 1500. 1*6*12= tshs2000. 2*4*12=tshs2500. 2*6*12= tshs3800. 1*8*12=tshs4600. 1*10*12=tshs9000. Zingatia hiyo star imetumika kama mara, yaani mfano inch 1 mara 4 mara futi 12. Nadhani umenielewa.
 
lukinga01

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
327
500
Asante sana mkuu , nikimaliza tafiti nitakujurisha
Acha nikupe bei ya pines mlingoti ntakupa kesho nikisha thibitisha taarifa za uhakika. Ubaya wewe hujaweka mbao kwa vipimo. Mm ntaanzia mbao ndogo kuja kubwa kwa pines: 1*4*12= tshs 900. 2*3*12=tshs 1500. 1*6*12= tshs2000. 2*4*12=tshs2500. 2*6*12= tshs3800. 1*8*12=tshs4600. 1*10*12=tshs9000. Zingatia hiyo star imetumika kama mara, yaani mfano inch 1 mara 4 mara futi 12. Nadhani umenielewa.
Pitia na hii mkuu nilikuwa namjibu Kinywanyuku.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom