Biashara ya Masoko ya Mtandao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya Masoko ya Mtandao

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Nov 7, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Fikiria kama ungekuwa walipwa kwa kila ushauri wa kutumia huduma ama bidhaa ya kampuni au shirika fulani, ungekuwa wapi leo hii kimapato?
  Labda ujanielewa vizuri, Je unaweza kukumbuka leo hii ni marafiki, ndugu au jamaa wangapi umewashauri juu ya ubora au uzuri wa bidhaa au huduma fulani tangu uanze kutumia huduma au bidhaa zao?
  Fikilia kwa mfano unatumia huduma ya simu ya kampuni A, kwa ubora wa huduma zake umewashauri ndugu zako kadhaa, au marafiki zako ama pengine umeshawishi ofisi ijiunge na huduma ya kampuni hiyo, tena bila malipo, bure kabisa na wala kampuni haijui uwepo wako, je waweza kumbuka idadi ya watu uliowashauri?
  Labda watu 100 kwa miaka kama mine au mitano toka ujiunge na kampuni A, tena wengine wamehama kampuni zao za zamani, sasa fikilia kama kampuni A simu ingeamua kutambua huduma yako hiyo, ya kushauri watu kujiunga na huduma zao nzuri, wakaamua kuwa watakuwa wanakupa sh 100 kwa kila sh 1000 ya watu hao mia watakazotumia, je ungekuwa na sh ngapi kwa siku au mwezi na hatimaye mwaka?
  Hebu tufanye hesabu rahisi kidogo, ikiwa kila Mmoja atakuwa anatumia sh 1000 tu kwa siku ina maana utapata sh 100 x 100 kwa siku sawa na 10,000/- sawa na Sh 300,000 au 3600000 kwa mwaka, hiki ni kipato cha ziada kutokana na wewe kuwashauri watu 100 tu kwa miaka mine, je ungepata kiasi gani kama utakuwa na watu 500 au zaidi.
  Kumbuka, hapa ujamuuzia mtu simu wala ujamuuzia mtu vocha, wewe umewashauri tu nao wakaamua kuingia katika mtandao uliopo na kampuni A ikakulipa kiasi hicho cha pesa, pengine wadhani hii haiwezekani, lakini maishani mwetu tunafanya hivi kila siku, twashauri watu saluni nzuri, hoteli nzuri, simu, kampuni nzuri ya simu, hospital nzuri, dokta mzuri mwanasheria mzuri, kinywaji kizuri, nk. hatulipwi.
  Lakini katikati yetu wapo wanaolipwa kwa kushauri watu kutumia huduma ama bidhaa za kampuni hii au ile na kujipatia kipato kizuri cha ziada kufikia na kuzidi Milioni 30 kwa mwezi, ndio Milion 30, hii ndio inaitwa “work smarter not harder”, fikilia mtu huyu atakuwa na pato gani kwa mwaka au miaka kadhaa?
  Hawa ni wafanya Biashara ya Masoko ya Mtandao, wako mamilioni duniani na idadi ikiindelea kuongezeka kila uchao, uwaoni lakini wako kila pahala, pengine ni jirani yako au mfanyakazi mwenzio au bosi wako, hii ni aina ya biashara ambayo mtu yeyote wa kipato chochote anaweza kuwekeza kiasi kidogo cha pesa na kupata kipato kinachopanda kwa kasi hata kufikia kuwa na uhuru wa kipato.
  Ndio maana ya Mtandao, walipwa kwa kuwasidia, kuwaongoza na kuwafundisha wengine kuanzisha biashara zao, kuwasaidia kufikia malengoyao na hatimaye uhuru wa kipato, hivyo wanamtandao ulipwa muda wao wanaotumia kuwasaidia na kuwaongoza wengine.
  Hii ndio njia inayopendekezwa na wataalumu wa uchumi waliobobea kuwa mkombozi pekee kwa watu wa hali ya chini kuwekeza na kufikia kuwa na Uhuru wa Kipato.
  Nukuu mbalimbali toka kwa watu maarufu, wasomi na watawala kuhusu Biashara ya Masoko ya Mtandao
  “You strengthen our country and our economy not just by striving for your own success but for offering the opportunity to others” Bill Clinton
  “Network Marketing has proven itself to be a viable and rewarding source of income. There have been some remarkable examples of success” Donald Trump
  “Network Marketing has produced more Millionaires than any other industry in the history of the world” Les Brown
  “When I read in the Fortune Magazine, that Warren Buffet, the Billionaire Investor was investing in Direct Sales (Network Marketing) I decided I was missing something”David Bach
  “In today’s world working for yourself is actually the safer route, and working for a corporation has become the riskier propositions” Paul Zane Pilzer
  “Network Marketing gives people the opportunity with very low risk and very low financial commitment to build their own income-generating asset and acquire great wealth” Robert Kiyosaki
  source:
  WINNERS Boulevard.
   
 2. MKOBA2011

  MKOBA2011 Senior Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ya people have to know this Tanzanian are real not aware with what is going on in tha world wengi wametawaliwa na utumwa wa kazi za kulipwa mshahara amabao kwa Tanzania hii hutofanya chochote cha maana zaidi ya kuwa mtumwa wa mikopo ya bank mbalimbali na Bank sasa wamegundua the best place to get profit ni wafanyakazi just imagine unakopa milioni sita unarudisha kumi na moja kwa muda wa miaka minne si utumwa huu,Na hiyo ela hata nyumba haiishi
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Wezi tu hakuna kitu, hakuna kitu kinachouzi kama "pitch" ya network marketer, huwa natamani ardhi ipasuke nidumbukie. Tena usiombe rafiki wa karibu aanze huu uzushi, utapewa story za Kayasaki mpaka utakoma, wakati hata centi hajatengeneza lol!
   
 4. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280

  Acha ubishi bwana KANG....hii biashara ndo mkombozi wa wanyonge...mimi nimetengeneza million 20 ndani ya miezi sita.....we ushindwe una nn?? swala ni kuamua tu. Tena na hiyo hiyo Forever Living Products......we kaa ndani tu ufkiri hela zitakufwata.
   
 5. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  Unajua it has to reach a stage all you think of is SUCCESS......nuthin else. Mi nakwambia ukiwa na mindset hiyo lazima utoke.
   
 6. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  madudu gani haya mnatuletea humu??
   
Loading...