Makwarukwaru
Member
- Mar 10, 2012
- 66
- 25
Kwa mtazamo wa kawaida, madawa ya kulevya ni kitu kinachopigwa vita sana. lakini kiuhalisia haiko hivyo. Kwani watu wanauza madawa haya peupe bila woga wala wasiwasi. Nani yuko nyuma ya biashara hii?ananguvu kiasi gani mpaka imekua halali kiasi hiki?Ukitembelea maeneo ya kawe ukwamani vijana wanatumia madawa 24/7 bila kificho wala wasiwasi,nani yuko nyuma yao anaewapa kichwa kiasi hiki? Sijataka kusema maeneo mengine ila hali ni mbaya,kama serikali kila mara inapiga kelele kuhusu madawa hawa mbona hawakamatwi? Mwisho, bangi ikikamatwa huwa inaharibiwa tunaona, ule unga unaokamatwa huwa unapelekwa wapi au unafanywa nini?
dah!!! umenifanya nimkumbuke marehemu Amina Chifupa, alitaka kutujibia haya maswali maana alidai alikuwa tayari anayo majibu yake. kwa bahati mbaya hakujaaliwa kuishi na kutupatia hayo majibu, YASEMEKANA WAHUSIKA WALIM-NYAMAZISHA FASTA. kwa hiyo ndugu yangu, nionavyo mimi, kutaka kuwajua wahusika, ni sawa na ku-beep kifo. lakini siwezi kushangaa kuwa ni watu wenye nafasi zao kwenye hili LI-SERIKALI BOVU KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA SERIKALI HAPA DUNIANI, maana katika hali ya kawaida haiwezekani pamoja na kelele zote hizo halafu eti wahusika hawakamatwi, si ajabu anayepiga kelele ndo mmiliki wa hiyo biashara, ROHONI KWA MTU MBALI.