Mkuu mpya wa mkoa wa mwanza unaenda kuua biashara za machungwa na matunda mengine kwa kukataa matunda yasiuzwe barabarañi yauziwe sokoni tu,hivi unajua huko mabarabarani ndio kwenye wateja?,yaani unataka mtu akitoka kazini akihitaji hata machungwa mawili ayafate masokoni hujui unaenda kuua biashara za watu, leo hii gari ya machungwa iliyokua inamaliza mzigo kwa siku mbili au tatu sasa itachukua siku tano ,hilo ni anguko la zaidi ya asilimia 50.Chondechonde mkuu mpya wa mkoa wa Mwanza hebu litafakari hili maana madhara yameanza kuonekana,juzi kati kuna mama dalali wa mananasi amepata stroke ,amepokea mzigo wa milion 5 akaukopesha kwa wauzaji wa barabarani nao hawana pakuyapeleka na wengine wamemkimbia