Biashara ya kuuza Uhuru wa Nchi ni mbaya zaidi ya kuuza Watumwa

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1][/h]

beit-564x272.jpg

Mimi ni mmoja wa watu waliokuwa wakipenda sana kulisoma gazeti la Nipe Habari na nilikuwa nikipeleka makala zangu ndani ya gazeni hilo. Nilibaini kwamba hilo gazeti kumbe ni gazeti lenye malengo mawili maalum. Kwanza ni gazeti lenye kumpiga vita sana Maalim Seif Sharif Hamad. Pili kutaka kuharibu mahusiano mema ya watu wa Oman na Zanzibar.
Hata hivyo nikijibu baadhi ya makala zake. Siku za awali walikuwa wakizitia makala zangu lakini nilipoikaza kalamu kwa staili ile ile ya uwandishi wao huwa hawazitii makala zangu kabisa. Mfano mzuri nilipoijibu makala ya Mh. Mohd Seif Khatib iliyobeba kichwa cha habari “SIO NJOZI” kwa makala yangu yenye kichwa cha habari “BIASHARA YA KUUZA UHURU WA NCHI NI MBAYA ZAIDI YA KUUZA WATUMWA” hawakuipa nafasi katika gazeti lao la Nipe Habari.
Nimeona ni vizuri niitume makala hiyo ndani matandao ili waungwana waisome na waelewe nilichokikusudia.
Najua kwamba Maalim Seif hawamuezi Abadan. Hawa ndio waliokuwa wakipanda majukwaani na kuandika magazetini kwamba Maalim Seif ni mpinga Mapinduzi, cha ajabu leo wamevikalia viti vya Baraza la Mapinduzi.
Jee wanamuweza maalim Seif hawa? Ni hawa waliojikusanya na kupita kila kona ya nchi hii ili kuwashawishi wananchi ili wasiipigie kura Serika ya Umoja wa Kitaifa, matokeo yake walishindwa vibaya mno. Jee ndio wanamuweza Maalim?
Juhudi za serikali zote mbili ya Jamhuri na ile ya Mapinduzi wameshindwa kukizuia chama cha CUF kufanya kazi zake Visiwani na Bara. Ni hawa waliokataa Mseto leo wanaula mseto. Ndio hawa hawa wanaokataa mfumo wa serikali tatu na leo uko njiani unakuja kwa uwezo wa ALLAH. Tunawaelewa hawa tokea asili walikuwa wakiukataa UHURU wakati wazalendo wakitowa kauli mbiu yao ya kusema “UHURUUU” wao wakijibu “ZUIAAA” Mpaka walipokemewa na Dr. Kwame Nkurumah wa Ghana.
Leo wazalendo wanasema tunataka mamlaka kamili wao wanasema hapana tunataka hivi hivi. Hebu nambieni jamani kila kukicha gazeti la Nipe Habari halina jipya zaidi ya Muarabu, Muafrika na Maalim Seif. Giza zito la chuki limewagubika na Mwenyezimungu amewapa adhabu ya mambo mawili, kwanza sauti ya Maalim Seif inawatesa, na pili kila wanapomuona anadunda sehemu mbali mbali katika nchi hii matumbo yanawauma ndio maana hawaendi mazikoni wala harusini maana wakienda watamuona Maalim Seif akilakiwa na umma wa wazalendo wa visiwa hivi.
Nasaha zangu. Msimuogope Muomani muogopeni Muengereza maana yeye ndie anayemlinda na kumpa mipango Mfalme tokea 1860.
Tulipodai Uhuru hatukwenda Oman kwa Muarabu tulikwenda Ulaya kwa Mzungu. Hiyo Oman yenyewe hivi sasa inalindwa Muengereza. Muengereza amejaa tele kwa kutumia milango miwili huwa anachaguwa upi aingilie, wa Kanisa au wa Serikali. Mlango wa kanisa ni mlango wa ANGLIKANA na mlango wa seririkali ni UBALOZI wa hapa nchini. Ndio maana viongozi wetu huitwa wakaenda Uengereza. Muogope Muengereza na sio Muomani.
Sasa jipatie burudani kwa kujisomea makala inayofuta hapo chini walioikataa kuipa nafasi katika gazeti la Nipe Habari. JIPATIE BURUDANI YA AKILI.
.
BIASHARA YA KUUZA UHURU WA NCHI NI MBAYA ZAIDI YA KUUZA WATUMWA.
Nilisoma makala ya Dk Mohammed Seif Khatib iliyoandikwa ndani ya gazeti la Mzalendo la Jumapili January 13/19 , 2013. Makala hiyo imebeba kichwa kisemacho “Sio njozi”. Maelezo hasa ndani ya makala hiyo ni kujaribu kuonesha unyama na ubaya uliofanywa na gengi la ukoo wa kinyonyaji la watu wa Oman.Dk Seif Khatib ameelezea kwamba Oman iliwanyonya Wazanzibari na kuwadhalilisha wenyeji wa visiwa hivi. Dk anasema baya zaidi kuliko yote ni ile biashara ya kuuza watu( biashara ya watumwa).
Dk Mohammed Seif Khatib amepokea tunzo la nishani ya kazi nzuri alioifanya ya kuuilinda Muungano wetu. Nishani hii amepokea kutoka kwa bosi wake Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo hasa la Dk Mohammed Seif ni kuwafahamisha vijana wa leo kwa vile wao walikuwa hawajui wala kuyaona yaliyotokea nyuma si njozi? Halafu anauliza kwamba vijana waleo walikuwa wanajuwa kuwa wapo wakiitwa watumwa, watwana na masuria?
Kujaribu kukumbusha mambo ya waOman na Usultani, utumwa na uarabu katika melenia mpya ni ubutu wa mawazo ya siasa au ufinyu wa dhamira ya historia ya mambo hayo. Mtu anaweza akajiuliza inakuwaje mheshimiwa huyu kiongozi na mwanasiasa ambaye ameshashika nafasi za Uwaziri katika serikali akaweza kuandika mambo ambayo athari za maelezo yake yanaweza kuathiri na kuleta chuki baina ya Serikali na watu wa Visiwa hivi ambavyo wengi wa wakaazi wake wamechanganya damu na watu wa Oman tokea zamani.
Hata hivyo maelezo yenyewe yamekosa usahihi.Ni dhahiri hakua na dhamira njema ya kutaka kuwaeleza vijana wa leo na matokeo sahihi ya historia ya wa Oman na watu wa Visiwa hivi.Mheshimiwa Dk Mohammed Seif Khatib alijaribu kutaka kuifunika historia ya waOman na watu wa Visiwa hivi bahati mbaya historia haikubali kufunikwa inajitokeza popote pale inapohitaji kufanya hivyo.
Unapoweka uzito wa jiwe la mezani ndani ya mezani kwa upande mmoja wa mezani hiyo. Unatarajia nini pale usipoweka kitu chengine kwenye upande wa pili wa mezani hiyo? Hapana shaka utakua huna ulicho kipima kwa wale wanao elewa mambo . Ukimueleza kijana wa leo uovu wa muOman na usimuelezee na yale mazuri yake aliyoyafanya hapana shaka unalengo la kumwambia hawa waOman ni watu wabaya sana kwa Wazanzibari. Mimi nimeona ni vyema nitie kitu kidogo kwenye upande wa pili wa mezani. Katika mwanzo wa karne ya 16 katika mwaka 1503 Zanzibar ikapata msukosuko mkubwa wa kwanza Wareno walivamia wakaingia , wakakalia Zanzibar.
Walienda kupiga Unguja Ukuu. Utawala wa kireno ulikuwa utawala wa kuwadhalilisha na kuwatesa wananchi. Wananchi walipambana nao wakashindwa . Mateso yakawa makubwa Wareno walikuwa wakiwakata miguu na mikono wananchi wa visiwa hivi. Mateso yake yalipokuwa makubwa wakakusanya watu kutoka sehemu mbali mbali za Unguja na Pemba wakasema :- Jamani huyu mzungu atatumaliza tufanyejee? Wakasema:- Tumesikia katika nchi za ghuba , kuna nchi ambayo imepambana na Mreno na imeshinda. Oman . kwanini hatuendi tukawaambia waje watusaidie? Wakakubaliana wakatafuta jahazi wakapeleka ujumbe kwenda kuomba msaada wa kuja kumuondoa mreno.Wakaja wakapambana na mreno akashindwa. Wakaingia wao (WaOman) na ndio kawaida kama umetafuta mtu akusaidie mkishashinda basi na yeye anakaa pale pale . kwa hivyo na wao wakakaa . natumai hili muandishi unalielewa kutokana na Mapinduzi ya Zanzibar.
Muliwaita watu kutoka Tanganyika waje kukusaidieni kupindua matokeo yake ndio hivyo hivyo kama ya waOman.Ukweli kama sio wa Oman kumuondoa mzungu hii leo Wazanzibar wangaliabudu sanamu na kujifutia karatasi wakati wa kwenda haja kubwa. Misaraba ndio ingalikuwa pambo la visiwa hivi .
Tumshukuru sana M/Mungu kwa hilo Mungu ametunusuru kupitia kwa wa Oman.Jambo jengine hawa hawajawabagua wenyeji kama muandishi alivyotaka kuzielekeza fikra zake kwa vijana wa leo. Wa Oman walikubali kuowa na kuolewa ( waliingiliana kwa kuowana na wenyeji wa Visiwa hivi). Ni wazanzibari wachache waliokosa kua na damu ya Kioman au makabila mengine .Zaidi yayote hayo ifahamike kwamba vita baina ya wazungu na Waoman haikuwa mchezo. Wareno walikuwa washenzi kweli kweli makatili sana.
Waoman wengi waliuwawa katika mapambano ya kuwafukuza wareno visiwani Zanzibar. Wazee wa Kioman walipoteza watoto wao, waume zao na baba zao. Hili sio jambo la mchezo Wenyeji wa Oman wanalielewa hilo. Kama sisi wazanzibari tumesahau hilo wao hawakulisahau.
Lazima hali hiyo tuwe nayo ndani ya akili zetu. Uhusiano wa Muoman na Mzanzibari ni uhusiano wa damu.Tuwache mchezo wa hawa wana siasa wanao gaiwa tonge iliokua haina hata mchuzi.Chuki binafsi wamezitanguliza kuliko ukweli.
Tuzingatie maelezo ya Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw Ali Ahmed Saleh nilio yaona ndani ya gazeti letu la Zanzibar Leo Disember 28,2012 Balozi anasema kuna haja Uhusiano wa Kidugu uliopo kati ya Oman na Tanzania hasa Zanzibar utafsiriwe kwa vitendo ili uwe na tija kwa pande zote mbili. Alisema uhusiano uliopo utakua hauna maana yoyote kama pande zote mbili hazitotumia fursa zilizopo katika kuimarisha ustawi wa wananchi wake.
Tusitosheke tu kuwa na uhusiano na Oman lakini chakufanya ambacho kitakuwa na manufaa zaidi kwetu sisi Zanzibar ni kutafsiri uhusiano huu kwa vitendo .
Alisema oman na Tanzania hasa Zanzibar zimekuwa na uhusiano wa kidamu na kamwe hauwezi kuvunjwa.Natumai hebu pima busara za watu hao wawili Mohammed Seif Khatib na Omar Ali Ahmed , utagundua kwamba balozi amejaaliwa kuwa na hazina ya busara na hekima ambayo inahitajika katika nyakati hizi hususani Zanzibar.
Unajuwa ukiangalia na kutafakari kauli za wanasiasa katika madai ya Sultani, Utumwa ,Utwana,Ubwana Uarabu na ungwana ndani ya siasa za Tanzania.Ikibidi kutumika kauli kama hizo, hakukuwa napengine popote ya maneno hayo isipokuwa zitoke ndani ya vinywa vya viongozi. Wanaotumiwa ambao ni watu walioiweka chuki mbele ya kila kitu.
Hawa kuharibu ndio kazi zao. Fitna , majungu,ubaguzi na chuki dhidi ya wale wanaojiita Wazanzibari, ukiwauliza wao ni nani? Hawajielewi Uzanzibari hawautaki na makabila yao hawayajui.Mara nyingi hupenda kujinasibu kwa Uafrika hata Nyerere alikuwa ni Muafrika lakini alijuwa kabila yake kwamba ni mzanaki. Watu wa aina hii ndio hutumiwa ili kuharibu mahusiano yaliopo baina ya watawala wetu wa zamani na wananchi.Tumeshuhudia wakoloni wa Kijerumani na utawala wao nchini Tanganyika. Viongozi wengi wa makabila mbali mbali walinyongwa na kuteswa, kufungwa jela na kujengeshwa njia za reli kwa mijeledi wengi wa watu hao walikufa kutokana na mateso na madhila waliyoyapata.
Tanzania kila mwaka inasherehekea siku ya uhuru wake tarehe 9 Desember ya kila mwaka.Hatujapatapo hata siku moja kumsikia Nyerere hata Mkapa kusimama na kuwalani au kuyakumbusha yale waliyoyatenda wakati walipo itawala Tanganyika.Je! walikuwa hawayajui hayo? kwa nini basi wasiseme uovu wa wakoloni hao? Kama biashara ya kuuza watu , wao ndio waliobobea hasa kwa kazi hiyo.Tuseme Nyerere na Mkapa walikuwa hawajui habari hizo ?
Maskini Mohammed Seif Khatib unakubali kutumwa kuibomoa nyumba yako na kutengeneza ya mwenzako .Wenzetu akina Nyerere na Mkapa hawakuwa tayari kuyakumbusha maovu ya wakoloni yalio kwisha pita kwa vile bado wanahitaji mambo mengi kutoka kwao.Nyerere alitambua bila ya misaada ya wakoloni na wauza watu nyakati za zamani Serikali yake haitamudu kwenda hata kwa mwezi mmoja achilia mbali mwaka mmoja.
Halafu msahafu wao Nyerere na Mkapa umeruhusu kuuza watu.Mfano mzuri ni: “Tena katika habari za watumwa wako na wajakazi wako, utakao kua nao mataifa yaliyo kando kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi wako utakao kua nao mataifa yalio kando kando yenu,katika hao mtanunua watumwa na wajakazi”,
WALAWI 25:44
Sikiliza. Dk Mohammed Seif. Nyerere amesoma Encyclopaedia of Religions jalada 11, UK 602 inaeleza kwa kusema : katika mafunzo ya Mungu wetu hakupatikani kuchukia utumwa na hakuna hata dalili moja inayoonesha kaharamishwa mtumwa.
Vile vile katika Insight on the Scripture Vol II UK 997 inaeleza hivi:- For a slave to have a Christian master was a blessing maana yake ni:- Kwa mtumwa kuwa na bwana alie Mkristo ni Baraka kwake!
Mimi nafikiri ni vizuri kwanza tukajiuliza mtumwa ni nani na utumwa ni nini? Tukianzia katika miaka ya kiza mwenye nguvu ndie atawale. Vita inayotokea baina ya nchi na nchi au kabila hii na kabila ile, wale watakao shindwa vita hao huchukuliwa kama mateka .
Hivyo aliyeshinda vita hiyo ni hiyari yao kuwauwa hao mateka au kuwatumia kwa shughuli zao kama wataona inafaa kufanya hivyo. Ikiwa watawatumikisha basi hapo huitwa watumwa .Zanzibar imetawaliwa na wareno,Wajerumani, Waengereza (kiujanja) na waoman mwishoni hivi sasa inatawaliwa na Watanganyika.
Maana ya kutawaliwa ni nchi kukosa maamuzi yake .Mfano mzuri pale tunapodhani kwamba mfalme ndio alietawala lakini utawala gani huo kuanzia 1890, kila jambo kubwa na dogo lilikuwa lazima liamuliwe kutoka Uengereza.Mfalme wa nchi alifanywa kuwa ni alama tu ya dola, hakua na uwezo katika kukata shauri juu ya uendeshaji wa nchi. Je! Ipo tofauti gani hivi sasa ukilinganisha alivyokuwa mfalme zamani na Rais wa Zanzibar hivi sasa?
Kawaida ya wakoloni popote ulimwenguni wanapo tawala lazima watumie mbinu ya kuwagawa watu ili waendeleze utawala wao . katika Zanzibar Muengereza alitumia njia za kuwagawa wananchi kwa kutumia asili za makabila yao. Hivi sasa wananchi wa Zanzibar wanagawiwa kutokana na Unguja na Upemba , hapana tofauti, zote ni njia za kuwagawa watu. Kaburu ni kaburu tu yoyote yule atakaefanya matendo ya makaburu basi na yeye atakua kaburu.
Ikiwa mzungu au Mwaafrika.Narudia tena. Muuza watu na muuza nchi ni nani mbaya zaidi? Huyu anaeuza watu ni mkoloni mkongwe huyu anaeuza nchi kwa kuwatumia aliowateka vitani ni mkoloni mpya. Vipi ukijiuliza tulishindwa vitani sisi Wazanzibari? Ndio uvamizi wa 1964 umetufanya sote kuwa watumwa. Wingine tumekubali kuwatumikia. wengine wanataka kutoroka. Katika minyororo ya utumwa kutokana na kazi nzito ya kuimaliza Zanzibar.
Hawawezi tena kuwavumilia sasa wanataka kutoroka. Tanganyika ilifanya INVATION (Uvamizi) Mapinduzi lazima yapangwe, yaongozwe na yatekelezwe na wananchi wenyewe kwa faida ya nchi na wananchi wake .Tukiangalia yaliotokea Zanzibar yalipangwa yaliongozwa na yalitekelezwa na WAGENI kutoka nchi za nje za jirani zetu. Ukweli huu unathibitishwa zaidi kwa vile Jamadari aliyeongoza haya mavamizi ni John Okello na wachini yake alikuwa Injini na Mfaranyaki.
Nani kati ya hao aliyekuwa kitovu chake kimezikwa visiwani ? Okello amezaliwa na amekulia kwao Uganda .Injini amezaliwa na amekulia kwao Kenya na Mfaranyaki amezaliwa na amekulia kwao Tanganyika wote hao walikuja Zanzibar wakiwa watu wazima na shughuli zao.Wamekuja kutafuta kibarua na kukimbia kodi za kichwa katika nchi zao Hata hilo waliloliita Baraza la Mapinduzi . Utaona sehemu kubwa ya wanachama wa Baraza hilo walikua si Wazanzibari, laa kwa kuzaliwa wala kwa kuchukua tajnisi (kuandikisha uraia).
John Okello, Khamis Daruweshi,Seif Bakar, Said Natepe,Said Washoto,Muhammed Mfaume,Edngton Kisasi,Mohd Abdalla Kaujore,Khamis Hemed Nyuni n.k Nathubutu kusema hawa ni vijana wa Nyerere aliokwisha wapenyeza humu Visiwani kwa kungojea miongozo ya Nyerere kupitia chama cha A.S.P Nyerere nae akiongozwa na waingereza kwa mashirikiano na marekani. Nchi ndio imevamiwa tumeshindwa kujikomboa waliotushinda wametufanya mateka na kwa hivyo tumekuwa watumwa .
Tuko aina mbili za watumwa, kulikuwa na Yule wa nyumbani na mwengine anae zurura. Aishie katika nyumba na bwana wake, alivaa vizuri, alikula vizuri pia, kwani alikula kile kilichoachiwa na bwana wake, akilala humo humo ndani ya nyumba ya bwana wake ingawa yeye hulala sakafuni, hata hivyo aliishi karibu na bwana wake waliwapenda wamiliki wao kuliko hata hao mabwana kujipenda wenyewe.
Walidiriki kujitolea hata maisha yao ili kulinda nyumba ya mmiliki wake (Muungano) tena kwa haraka kuliko hata huyo bwana mwenyewe. Kama tajiri wake akisema. Tuna nyumba nzuri hapa basi Yule mtumwa atarukia “kweli bosi tuna nyumba nzuri”.Kila wakati ambapo bosi atatumia sisi nayeye hatosita kutumia neno hilo, hivyo ndivyo walivyokuwa.
Kama nyumba ya bosi ikashika moto Yule mtumwa atakimbia zaidi kuuzima moto kuliko hata mwenye nyumba mwenyewe,kama bwana akiumwa, utamkuta mtumwa wake akiuliza, vipi bosi hata sisi tunaumwa (kwa hali ya kumsikitikia na kumliwaza bosi wake) Alijitahidi kumtambua bosi wake zaidi ya bwana wake kujitambua mwenyewe.Na hata ukienda kumtembelea mwenzako huyu ukimuasa atoroke ! utakuta anakuangalia kwa jicho la mshangao na kusema He! Unawazimu? Una maana gani unavyosema tutoroke?
Mtumwa wa sasa hana tofauti na mtumwa wa zamani
Wapi nitakaa katika nyumba nzuri kama hii? Wapi nitavaa nguo nzuri kuliko hizi? Wapi nitakula kizuri kuliko hiki? Huyo ndio mtumwa wa nyumbani. Kwa kipindi hiko bado tunao humu ndani wanazunguka zunguka kuturudisha nyuma mitaani.Huyu mtumwa wa kisasa anampenda bosi wake sana. Anataka aishi karibu nae .
Ataridhika kulipa mara tatu ya thamani ya nyumba ili apate nafasi ya kuishi karibu na mabosi wake (Viongozi wa juu) na kutamba kwa wenzake, mimi ndio nastahiki pekee hapa. Ndio pekee katika kazi hii ndio pekee katika chama hiki. Tunakwambia wewe si chochote zaidi ya mtumwa wa nyumbani kama wale watumwa wa zamani.Na kama mwenzake akija kukushauri kuondoka hapa, unasema kile kile alichosema mtumwa wa kale katika mashamba, Unamaanisha nini ukisema tuondoke? Tutoke katika Muungano? Muungano huu ni mzuri wa Waafrika.
Bwana wa watumwa wa zama hizo alimtumia Nokoa kulinda wenzake, ndio hicho hicho kinachofanyika sasa kwani hawa vibaraka sio lolote zaidi ya kuwa ni wajomba wa kisiasa tu.Kina mjomba wa karne ya 21 wanatumika kutulinda sisi na wanaturudisha nyuma. Wanatufanya tupende amani ambayo ni ya uongo tusiwe na Vurugu.
Huyo ni Yule Yule bwana anaekufanya uwe hivyo ili uendelee kutawaliwa. Ni sawa sawa umeenda kwa tabibu wa meno ambaye atakutoa jino lako, utampiga tu atapoanza kuvuta jino. Sasa itabidi tuweke dawa katika taya zako ili usikie ganzi na hapo utakuwa unaumia kwa amani kabisa .Damu itakuwa inamwagika katika taya zako na wewe hutahisi chochote kikiendelea .Eti kwa sababu kuna mtu amekufanya uumie kimya kimya!
Wenzetu wanatufanyia jambo hilo hilo nchini mwetu.Anapotaka kututumia atakavyo na asiwe na hofu yawewe kupigana nae huwa wanawatumia hawa ndugu zetu, wakituelekeza tusiache kuumia ila tuumie kimya kimya! Wanatufundisha damu za raia zimwagike mitaani.Wenzetu hawa wamewachukua ndugu zetu, wakawavalisha vizuri wakawapa elimu kidogo ili sisi sote tuwatazame wao.Kwa njia hiyo iwe rahisi kuwatawala wale waliobakia kupitia kwa hawa ndugu zetu.
Mbinu hizo hizo zilizotumika kipindi cha watumwa ndizo hizo hizo zinazotumika hivi sasa .Anamchukua mwenzetu mmoja na kumfanya mshauri , anamjenga, anamtangaza na kumfanya awe mzungumzaji na kiongozi wa wenzake.Mtumwa ni mtu aliyetekwa na atatumika kama bwana wake atakavyo.
Wengi miongoni mwetu tumetumika kuuza nchi badala ya kuuza watu.Lipi baya zaidi kati ya hayo mawili.
Muandishi hujinasibisha na uafrika ni vizuri sio kitu kibaya, maana hata Nyerere nae alikuwa muafrika lakini hakusita popote pale kuitaja kabila yake kwamba ni Mzanaki,Je!!! Ndugu yetu Dk Mohammed Seif Khatib wewe hebu tuambie sisi nduguzo wewe ni kutoka kabila gani katika makabila yetu ya hapa Tanzania? Ukweli nimekuuliza suala hilo kwa vile hizo ndizo falsafa zako zote ulizo nazo na husikii kitu zaidi ya Uarabu,Uafrika,Utumwa,Usultani,Utwana,Ujakazi nk.
Malumbano ya kisiasa ya karne hii si ya biashara ya utumwa au Wakoloni, huo sio ukombozi tunaoutafuta hivi sasa.maneno hayo hayana ushawishi hivi sasa. Katika hoja za kisiasa haya ndiyo maneno yenye ushawishi kwa kila mwenye kura:-
Yaliyo muhimu hivi sasa ni uhuru wa mawazo katika kudhibiti uchumi wa nchi yetu ya Zanzibar ili uwafikie wananchi na kukoma kudhalilishwa kwa wananchi kwa kukosekana kwa huduma muhimu yaani elimu nzuri matibabu muaafaka na kujikimu kwa kila familia katika upatikanaji wa mahitaji muhimu ya siku hadi siku.
Haya ndio maneno yenye ushawishi kwa kila mwenye kura, sio Uarabu,Utumwa wala usultani mategemeo ya wananchi ni:-
Uhuru badala ya ukoloni
Neema badala ya umaskini
Usawa badala ya ubaguzi
Haki badala ya uonevu na ukandamizaji
Pigania haya upokee nishani kutoka kwa wananchi sio watawala.

Ibrahim Mohammed Hussein
Simu: 0715 – 498363
 
Back
Top Bottom