Governor of Bettors-GB
JF-Expert Member
- Jul 14, 2013
- 10,734
- 9,915
Hahaha nakubalina na wewe,ila changamoto ni usafirishaji.Yahee pweza njoo ununue kwetu huku zanzibare tunauza bei nafuu sana kuliko huko tanganyika.
Air Tanzania ndio ilikuwa mkombozi,ila Precision Air kwa flight ya Zanzibar-Mwanza ni changamoto kubwa saana.
Ila ata hivyo,Zanzibar sio rahisi saana pia,maana mahoteli ya kitalii ni mengi saana kuliko Dar,sasa demand ni kubwa mno kupita maelezo.Maana hata ukienda Vijiji vya Pwejuu na Paje ambapo idadi kubwa hupatikana huko bado ni ghali saana.Maana wanuzwa kwenye mahoteli kwa bei mbaya.
Labda mtu atumie kununua kisiwani Pemba ambapo hakuna changamoto kubwa ya Mahoteli,maana hata wafanyabiashara wa hapa Zanzibar wale wanaooza Jumbo Prawns wanawaagiza Pemba huko kwa Wakojani.
Unajua ukiwa na connection nzuri ya usafiri inalipa,ila hili ndio changamoto,maana bidhaa ikiharibika ni bonge la hasara.
Mliopo Dar hembu niambieni Kilo moja ya Pweza ni Kiasi gani?