Nijuavyo,unatakiwa kupata mpimaji kwanza atakaekupimia na kukuambia maji kama yapo hapo na yapo umbali gani,atakupa report ambayo utampa mchimbaji,siku hizi kampuni nyingi za uchimbaji visima zina watu wa upimaji,wakisha chimba kisima ni lazima wakapime maji waliyoyapata kama yanafaa kwa matumizi ya binadamu na watakupa report pia ambayo itaonyesha madini yaliyomo na ph ya maji.Kuna kipindi nilisikia wizara ikisema watu wapate vibali vya uchimbaji visima,unaweza watafuta uone inakuwaje,hayo machache ambayo niliyapitia tulipochimba hapa kwetu.