Biashara ya kuuza kitimoto

Quinne

Member
Dec 29, 2022
9
6
Habari za wakati huu wana Jamii Forums, kheri ya mwaka mpya.

Naomba msaada wenu kujua sehemu ninayoweza kupata mtu anaechinja nguruwe na kuuza kwa bei angalau 5000tsh maana nahitaji na mimi kufanya biashara ya kuuzia watu wa majiko ya kupika kitimoto na wenye butchers za nyama ya nguruwe.

Hii ndo biashara niliyokua naifikiria sana nikiwa chuo na nilisave baadhi ya pesa ili nikimaliza nianze hii biashara maana naamini itaniletea matokeo chanya ya kusaidia maisha yangu na familia.

Naombeeni msaada wenu wana JF. Namba yangu ya mawasiliano ni 0628487481
 
Inategemea hupo mkoa gani !.
kuna muda watu wanasafirisha kutoka Iringa, Mbeya, Shinyanga na maeneo yenye ufugaji.
 
Namaanisha hata nikipata anauza nguruwe mzima mzima ila kwa bei ambayo naweza kufanya biashara kuuzia watu wenye biashara za mabutcher na majiko ya kitimoto
chakula kilivyo ghali huwezi kupata kwa bei hiyo, labda kwa mtu asiyeelwa.
 
Namaanisha hata nikipata anauza nguruwe mzima mzima ila kwa bei ambayo naweza kufanya biashara kuuzia watu wenye biashara za mabutcher na majiko ya kitimoto
namba uliyoweka hapo nimepiga kapokea mwingine haelewi hata kisawahili. Ingia field, kwanza ujue bei ya jumla iliyopo kwa kipindi hiki, pili ujue ni watu wangapi wa majiko wako tayari kununua nyama kutoka kwako na uwezo wa kilo ngapi. Kazi ya kutafuta mdudu unipe, niko kibaha huku na nilishawahi kufanya moshi hivyo naelewa abcd zake. karibu kama utapenda hii combo
 
Samahani sana Emamarki kupata huu usumbufu,number ni 0628487481
 
Nnavyojua,huku dar-mbezi (kimara) nyama mbichi bei ya jumla ni 7000 kwa kilo,na hata mtu akiwa na nguruwe wake atakuita uchinje thn mnapimiana kilo mtakazopata mnazidishiana kwa 7000.
 
mkuu unafanya hii biashara
 
Nnavyojua,huku dar-mbezi (kimara) nyama mbichi bei ya jumla ni 7000 kwa kilo,na hata mtu akiwa na nguruwe wake atakuita uchinje thn mnapimiana kilo mtakazopata mnazidishiana kwa 7000.
Mkuu, chimbo gani Kimara ili?
 
Back
Top Bottom