Biashara ya kuuza Barafu (ice cubes), msaada location | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya kuuza Barafu (ice cubes), msaada location

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Doltyne, Sep 15, 2011.

1. Doltyne

Doltyne JF-Expert Member

#1
Sep 15, 2011
Joined: Aug 29, 2011
Messages: 443
Likes Received: 8
Trophy Points: 35
Habari wana JF, ninatarajia kuanzisha biashara ya kuuza barafu (ice cubes) na kuuza kwa kilo. Sasa nastruggle kupata location itakayoendana na biashara yangu. Mchakato mzima uko hivi.

1: natarajia niwe natengeneza kilo 800 (mia nane) za barafu kwa siku. Natarajia kuziuza zote kwa order au random. Kilo moja ntauza sh 1500, hii ni ice cubes na mifuko yake ya kupack.

2: umeme ntatumia wa generator kwani machine inakula umeme mkubwa, na nina generator ya 11kva tayari. Generator hii itakuwa ni back up tu, tanesco ntaendelea nao kama kawaida pale watakapojisikia kutupa huduma.

3: maji ya ice maker yatakuwa yanatoka kisimani. So nachimba kisima kimoja tu kwa kazi hii. Na yatakuwa sio tatizo.

Naombeni msaada wa location, niiweke wapi hii biashara, nifanyie site mbali na watu halaf nitarget orders, au niwe na frame sehemu. Uwezo wa kuhifadhi barafu zisiyeyuke ninao bila kutumia umeme wala jokofu. Pia kama kuna anyeweza kuspot threat na risk za biashara hii aniambie ili niweze kuresolve mapema. Challenges nk ni zipi mbali na nilizonazo mimi kichwani.

Nb: unapotoa mchango tafadhali be frank and sincere kwasababu hii ni biashara ya 48m investment.

Shukran sana ndugu.

2. KeyserSoze

KeyserSoze JF-Expert Member

#2
Mar 14, 2014
Joined: Feb 26, 2014
Messages: 1,835
Likes Received: 88
Trophy Points: 145
Selling Ice to Eskimos.... Anyway Joking aside nadhani cha muhimu ni kuangalia wateja wako wapo wapi na kuwa nao karibu sababu in the long run hii itakusaidia kwenye kupunguza cost ya transport na itasaidia wateja kukufikia kwa urahisi.

Kwahio mkuu walengwa wako wapo wapi ? Na kama haujajua walipo unaweza kuangalia watu wanaofanya hii biashara wapo sana sehemu gani (hii ni indication kwamba sehemu hio kuna wateja), baada ya hapo ni wewe kufungua karibu na hapo na kutoa huduma bora / bei ya chini kuliko competition, (kama uwezo unao) hence wateja wao kuhamia kwako.

Njia nyingine bora zaidi ni kuangalia wapi hakuna huduma hii ila inahitajika, mfano watu wanaosafirisha vitu vya kuharibika, mfano samaki kwahio mikoa kama Mwanza, au sehemu za ndani ndani ambapo kuna wavuvi ila huduma hii haipo na inahitajika.

Kwahio mkuu kwa ufupi kama wateja unao / unajua wapo wapi itakusaidia kupunguza cost ukiwa karibu nao; Kama wateja hauna wala hujui wapo wapi unaweza ukaset-up karibu na competitor wako iwapo huduma yako ni bora zaidi.., kama wateja wametapakaa set up katikati na wewe kuwapelekea huduma popote walipo, cha maana pia angalia na cost ya location sio busara wewe kukodi sehemu na kulipia 50% ya income yako kama rent.., wakati kumbe ungeweza ku-setup mbali kidogo kwa rent ndogo.

3. Lady niece

Lady niece JF-Expert Member

#3
Mar 14, 2014
Joined: Feb 18, 2014
Messages: 886
Likes Received: 10
Trophy Points: 0
wewe usipate shida kupata masoko mbona yako mengi nenda sehemu za biashara kwa mafano magengeni utapata wateja na sehemu nzuri ni maeneo ya hospitali kwani ukiongea vizuri na yule muhusika wa mochwari atayanunua na kuweka kwenye mafriji ........ yapo utafanya biashara nzuri sana sijui kama umenielewa hapa

4. Sita Sita

Sita Sita JF-Expert Member

#4
Mar 14, 2014
Joined: Aug 25, 2008
Messages: 1,197
Likes Received: 33
Trophy Points: 145
Soko zuri ni pale feri kivukoni
Naona watu wengi wananunua kwa ajili ya kusafirishia samaki
tatufata location maeneo ya kigamboni

au nenda kwenye soko la samaki la ununio
utapata wateja wa kutosha ingawa mnada wa samaki sio wa kila siku

5. KeyserSoze

KeyserSoze JF-Expert Member

#5
Mar 14, 2014
Joined: Feb 26, 2014
Messages: 1,835
Likes Received: 88
Trophy Points: 145
Seriously Mkuu are you Serious ?, Mahospitali wana tenda / wanahitaji kununua/outsource barafu kutoka kwa wadau wa nje ? au tayari wanazo cold room in place. Yaani binadamu mortuary anahifadhiwa na kugandishwa kama samaki ?

6. Lady niece

Lady niece JF-Expert Member

#6
Mar 15, 2014
Joined: Feb 18, 2014
Messages: 886
Likes Received: 10
Trophy Points: 0
mwambie asisahau na maeneo ya mwanza pale victoria lake

Loading...