Biashara ya kujenga na kuuza nyumba

lizyisaac

Member
Feb 24, 2016
12
13
Mimi ninataka kuanza mradi wa kujenga na kuuza nyumba (ambazo zinakuwa zimefika hatua ya lenter) nipo Dodoma hivyo mradi huu natarajia kuufanya hapa Dodoma.

Naomba elimu, ushauri, uzoefu n.k utakaonisaidia kupata elimu nini cha kufanya ili kuanza.

Asanteni
 
Yani nyumba ikifika hatua ya lintel ndo unauza? kwanini usimalizie kabisa?
 
Bora ujenge upangishe
sijui soko likoje huko Dom
viwanja huko vimepimwa?una hati?
 
jamani Mimi ninataka kuanza mradi wa kujenga na kuuza nyumba(ambazo zinakuwa zimefika hatua ya lenter).nipo Dodoma hivyo mradi huu natarajia kuufanya hapa Dodoma.naomba elimu,ushauri,uzoefu n.k.utakao nisaidia kupata elimu nini cha kufanya ili kuanza.
asanteni[/QUOTE

Lizyisack nashino hauzingi,,,
 
Kwa dom nakushauri ufanye biashara ya kujenga hostel za wanachuo na kuzipangisha zinalipa sana kama kule chuo cha mipango kuna uhaba wa hostel
 
Mimi ninataka kuanza mradi wa kujenga na kuuza nyumba (ambazo zinakuwa zimefika hatua ya lenter) nipo Dodoma hivyo mradi huu natarajia kuufanya hapa Dodoma.

Naomba elimu, ushauri, uzoefu n.k utakaonisaidia kupata elimu nini cha kufanya ili kuanza.

Asanteni
Jambo zuri sana...mimi nipo kwenye hiyo fani.
Fursa zilizopo.
1.Ni kuwa watu wako busy sana tz hasa dar hawana muda wa kusimamia miradi yao.
2. Watanzania hawaaminiki kabisa ukimkabidhi akusimamie shughuli yoyote basi unakuwa umempa ulaji.
3. Tanzania hasa dar kuna uhaba mkubwa wa nyumba za kipato cha kati (midium income earners ).

Challenges
1. Kupata real low cost designs hili limekuwa ni tatizo sana tz.
Nalisema kwasababu mimi ni architect pia.
Taasisi yetu tunahusika na kujenga sana nyumba za bei nafuu

Ndio changamoto pekee utakayokuwa nayo kubwa zaidi.
2. Soko la kuuza na kununua nyumba tz halijawakubwa kiasi hicho japo ndio njia rahisi zaidi wenzetu UK na nchi za ulaya wameweza sana hili.

Mtu ananunua nyumba kulingana na mahitaji yake muda huo.

Zaidi nakutakia biashara njema!
 
Mimi ninataka kuanza mradi wa kujenga na kuuza nyumba (ambazo zinakuwa zimefika hatua ya lenter) nipo Dodoma hivyo mradi huu natarajia kuufanya hapa Dodoma.

Naomba elimu, ushauri, uzoefu n.k utakaonisaidia kupata elimu nini cha kufanya ili kuanza.

Asanteni
Jaribu inalipa japo ni moja kati ya biashara ambazo ni moon like. Speed yake sio ya kuridhisha japo kuna wakati ukilifumania soko inalipa kidogo. Nimewahi kujenga boma kwenye kiwanja kilichosajiriwa, nilitumia kama shs 7,000,000/= hivi. Nikapata bahati ya kulifumania soko na kuiuz kama Tsh 15,000,000/=.
Jaribu, mjasiriamali huwa haogopi.
 
Back
Top Bottom