Mkuu nilipomaliza masomo niliamua kufanya hii biashara maeneo ya wazo kupita Twiga cement kuna machimbo, ni biashara nzuri inayolipa hasa kipindi cha kiangazi, changamoto zake ni watu wa vipimo na mizani wanaweza kukomalia mzigo kuwa haujatimia ilihali Ww uliupima pia watu wa mazingira so called nemc wanakusumbua hata kama una docs zote, kuna watu wa madini nao wanatega njiani wakisubiri chao hata kama unarisiti ya madini bado kukimbizana na polisi hawa huwa hawana agenda maalum mwisho kabisa madalali ukijichanganya unaweza kuagiziwa mzigo ila malipo ni majaliwa, all in all hii ni biashara nzuri ushauri Wangu kama una mtaji mzuri fanya utafiti wapi ardhi yake ina kokoto ununue shamba baada ya muda wewe utakua mmiliki wa machimbo!