Biashara ya figo yashamiri nchini Tanzania

Biashara ya figo yashamiri nchini Tanzania

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,703
Reaction score
59,224
figo.jpg

Dar es Salaam. Katika kile kinachoonekana kukithiri kwa hali ngumu ya maisha, baadhi ya Watanzania wameanza biashara ya kuuza figo zao kwa gharama kubwa kwa watu wenye mahitaji ya kiungo hicho muhimu mwilini.

Uuzaji huo umetokana na ongezeko la maradhi ya figo miongoni mwa Watanzania kwani takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zinaeleza kuwa kuna wagonjwa 470,000 nchini ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi kabisa na wanahitaji upandikizaji. Katika uchunguzi wake, mwandishi wa gazeti hili alifanya kazi ya kutafuta kama wafanyavyo watu wengine wenye mahitaji hayo na alifanikiwa kukutana na watu kadhaa ambao walikuwa tayari kumwuzia lakini kwa gharama kubwa.

Kijana mmoja alikuwa tayari kumwuzia figo mwandishi wetu. Katika kufikia makubaliano mazungumzo ya kijana huyo, Abiyudi Mtaki na mwandishi wetu yalikuwa hivi:

Mwandishi: "Habari yako kaka, nimepata namba yako kutoka kwa (jina linahifadhiwa) amesema upo tayari kuuza figo yako, mimi nina shida kwa sababu mama yangu anahitaji na hali yake si nzuri."

Muuzaji: "Nitumie meseji nipo kwenye gari."

Alipotumiwa meseji alijibu hivi: "Dada yangu mimi naelekea Uganda, kuna mtu kanitumia tiketi jana, wakala nilimwambia kuwa nauza, ila yeye hakuniambia iwapo kuna mtu wa Dar es Salaam anayehitaji."

Mwandishi: "Jamani kaka tusaidie kwa sababu tuna shida, kwani huyo wa Uganda anakupa shilingi ngapi?"

Muuzaji: "Napata milioni 80 aisee!"

Mwandishi: "Basi sitaweza kupata hizo fedha, ngoja niangalie namna nyingine."

Muuzaji: "Kwani we ulikuwa na ngapi?"

Mwandishi: "Tuna shilingi milioni 20 tu."

Kiwango hicho hakikukubaliwa na muuzaji huyo.

Mei mwaka jana, Mwanahabari wa Gazeti la The Telegraph la Uingereza alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook na kujifanya kuwa ni kaka wa mwanamke anayehitaji kupandikizwa figo hivyo anahitaji mtu anayeuza.

Ndani ya wiki moja alipata wateja zaidi ya 16 kutoka Uingereza, India na Tanzania waliojitolea kuuza figo zao kwa gharama ya Euro 20,000 hadi 30,000, zaidi ya Sh68 milioni. Daktari Bingwa wa figo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Linda Ezekiel alisema uuzaji wa figo ni kosa la jinai kwani kisheria ni makosa kuuza kiungo cha binadamu kwa gharama yoyote.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Figo Tanzania, Jaji Frederick Werema alishangazwa na hatua za baadhi ya watu kuchukua uamuzi wa kuuza figo kwa ajili ya kujipatia fedha.

"Kutoa figo ni kosa la jinai, lakini si hivyo tu, kutoa figo ni lazima ufuate taratibu za kisheria na za kitabibu," alisema Jaji Werema, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja alisema miongozo na sera za Wizara ya Afya hazikubaliani na biashara ya uuzaji wa figo kama ilivyo kwa uuzaji wa damu.

Source: Mwananchi
 
Huu uandishi wa habari hovyo kabisa,badala ya kuleta tafiti wangapi na kina nani waliouza na wslionunua na hospital zilizohusika yeye anaweka bla bla za mawasiliano ya simu
 
Ole wenu mnaojaribu nafsi za wenzenu kwa lengo la kujinufaisha, ewe mwandishi (Source: Mwananchi) ungejisikiaje kama huyo ndugu aliyekuwa njiani kwenda Uganda angesema anarudi ili uinunue figo yake kwa Shs 20M, tambua kuwa huyo naye ni mwenye uhitaji, hajapenda ila kalazimika, hana njia nyingine,
 
Mbona dili iyo.maisha yenyewe magumu ivi hujui ya kesho coz ccm warema nae anashanga nn?tatzo yy na ccm.80m nauuza bana.
 
Hata mimi niliwahi kuonana na shushushu fulani alisema anataka figo yangu kwa sh mil 30
 
Hii ni biashara ni kichaa,wasipoangalia daktari wa figo anaweza kuvuta kitu kidogo kwa mnunuzi halafu akammalizia(akamuua) huyo mtoaji figo !
 
jamani eehhh maisha yenyewe ndo yanatu force watu tufanye buashara hii kama means ya kutafuta capital, hii biashara haina tofauti na biashara ya utumwa iliyofanywa na whites, japo ni mbaya zaidi lakini historia inasema iliwanufaisha sana wazungu....mwenye uhitaji wa figo hata mimi nipo tayari kuiuza afanye kuni PM...bora nife kwa udhaifu wa viungo vyangu vitakavyosalia kuliko ninavyokaribia kufa kwa njaa na viungo nikiwa navyo....
 
Kweli Umaskini huu utatumaliza.
Itafikia hata hatua watu watauza watoto wao Kwa wanandoa wa jinsia moja.
 
Back
Top Bottom