Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Kwa angalizo, kuwa makini sana na Kukopesha mf. Faida ya vocha hua ni dogo sana Hivyo kumkopesha mtu vocha unaweza ukose hata Ela ya kununulia zngne
 
Unahitaji vitabu (nunua hata counter books) vya kumbukumbu za hesabu kama vile : KITABU CHA MATUMIZI, KITABU CHA MANUNUZI, KITABU CHA MAUZO, KITABU CHA MADENI - kwa unaowadai na wanaokudai, KITABU CHA MALI YA BIASHARA, KITABU CHA STOCK. Vilevile unahitaji kununua mafaili ya kutunzia stakabadhi za manunuzi, malipo, bank slips, mikataba, na nyinginezo ktk mpangilio kila moja na faili lake.

Pia unatakiwa kuwa na diary au note book kubwa kuandika bidhaa ambazo hautakuwa nazo wateja ambazo wateja wamehitaji (missing items) ili kukupa kumbukumbu za kuzinunua. Kitu kingine panga vitu ktk mpangilio mzuri usifanye duka ili mradi duka, panga vitu vinavyofanana kwa pamoja na usijaze items nyingi ktk display kwa pamoja. Kauli nzuri kwa wateja, uharaka, uhakika, ubora na hali ya kujali wateja ndo uchawi wako ktk biashara hii.

Usisahau kufuga paka mdogo kufukuza panya. JINGINE MUHIMU, hakikisha kila siku asubuhi unapeleka mauzo ya jana yake benki kabla ya kuyatumia, pia usajili biashara yako na uifungulie akaunti ambayo itakuwa na jina la hiyo biashara (mfano MAJIGO RETAIL SHOP).

Ooh thanks Mkuu I was well taught then,
 
Habari zenu wana JamiiForums,

Mimi ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa tatu,katika harakati za kujiandaa na kupambana na maisha pindi nitakapohitimu elimu yangu na kurudi mtaani,nimetafuta pesa ikiwa kama mtaji wa biashara milioni moja (1,000,000)hasa ya duka la bidhaa za vyakula.

Tatizo ni kwamba si mzoefu ktk biashara na ni mara ya kwanza kutaka kuifanya hii biashara kwan matarajio yangu ni kujiajiri mwenyewe.

Naomba ushauri kwa yeyote mwenye uelewa kuhusu hili kunipa mchanganuo wa bidhaa muhimu zinazotakiwa kuwepo dukani kama vile unga kiasi gani,mchele n.k kulingana na mtaji huo wa Milioni Moja.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Hongera sana Mkuu karibu ktk ulimwengu wa fikira tofauti kwa wajasiriamali! Vizuri ukifanya mwenyewe research kwa wafanya biashara na wenye maduka mbali mbali! ama kama upo tait nipe tenda hiyo Kampuni yangu inadeal na masoko inaweza kukufanyia kwa bei nafuu kabisa! my kampani ni Tangaza Marketing Solutions (TMs)

Karibu sana.
 
Shukran mkuu,ngoja nijaribu kufanya research mwenyewe maana pesa ya kutoa tenda kwa utafiti itamaliza capital yenyewe.
C'mon man anaweza kuwa na bei nzuri, mfano kuna kampuni moja pale kenya wanakufanyia market research kwahizi biashara ndogondogo kwa gharama haifiki hata elfukumi ya kibongo.wanakupa full infor kuhusu biashara husika,mfano capital ya kuanza nayo, process ya kuanzisha, location inayofaa rent ya flame, maunjanja katika biashara husika etc.
 
coomon man anaweza kuwa na bei nzuri,mfano kuna kampuni moja pale kenya wanakufanyia market research kwahizi biashara ndogondogo kwa gharama haifiki hata elfukumi ya kibongo.wanakupa full infor kuhusu biashara husika,mfano capital ya kuanza nayo,process ya kuanzisha,location inayofaa,rent ya flame,maunjanja katika biashara husika etc.

kwa mtaji wa m 1 rent ya flame itamuumiza labda kile cha mbao (movable) pia akikinunua ni poa zaidi.
 
Mkuu Ibravo,

Kwanza kabisa nikukaribishe humu maana unaonekana umejiunga humu this month hivyo you are still junior member, kwa kifupi humu kuna changamoto nyingi na shauri nyingi ambazo hata nyingine zinaweza kukukatisha tamaa kabisa au hata kujuta kuwa hivi nani alikushauri kuingia humu na ku-post threads za hovyo hovyo (wachangiaji wengine wanaweza kuziona hivyo), leo nikupe changamoto moja juu ya hii thread uloleta hapa:

Ibravo, sina nia ya kukukatisha tamaa juu ya mpango wako wa kuanzisha biashara ya duka hilo kwa capital hiyo ambayo umebahatika kuipata, ila to be honest nimeshangazwa na kusikitishwa na wazo hili kutoka kwako (msomi/graduate mtarajiwa). Naomba niseme wazi kuwa elimu unayosoma haijakusaidia chochote na nadhani ulikuwa unapoteza muda huko au labda ulikosea fani ulokuwa unasomea, wapo vijana wengi wanaenda vyuoni kusoma kwa mkumbo tu bila kujua anakwenda kusomea nini hasa. Lakini nadhani hapa ni uelewa wako tu ndo maana una wazo la kujiajiri, vinginevyo ningekulaumu kwa namna tofauti.

Nina imani watajitokeza wana JF wengi ambao wakisoma mchango wangu huu hawatanielewa, ila acha tu niseme ulonilazimisha kusema hasa baada ya kusoma uzi wako Ibravo.

Hata kama tunasema UJASIRIAMALI, inawezekanaje MSOMI/GRADUATE mtarajiwa unatoka chuoni unapewa mtaji wa mil 1, then unakurupuka na wazo la kufungua duka la kuuza UNGA, MCHELE n.k (UCHUUZI)? hivi hapa tutasema shule/elimu imekusaidia? Na hapa niseme kuwa kama vijana wengi mnaenda vyuoni mnalipa fees huko miaka 2,3-4 nakuendelea, mnamaliza mnakuja na mawazo ya namna hii huku mitaji ya kiasi hiki mnabahatika kupata then niseme wazi kuwa elimu itakuwa haijawasaidia. Haya ni mawazo MGANDO, mtu unataka kufanya kitu kwa mazoea tu kwa kuwa watu wanafanya, huu si UJASIRIAMALI, ujasiriamali ni uwezo wa kubaini fursa kulingana na mtaji ulionao.

Nafurahia sana na watu wanaokuja humu kuuliza ili wapate mawazo kutoka kwa wachangiaji wanaJF great thinkers, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kutamka kiasi (initial capital) alichonacho na anaomba ashauriwe afanye shughuli gani, watu wanatoa ushauri ktk shauri hizo wanasema AKILI YA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO, then unapata shughuli ya kufanya. Ibravo nimesema sina lengo la kukukatisha tamaa ila nakueleza tu ya moyoni, wewe umeleta hapa wazo ambalo tayari unalo kichwani ndo maana watu wameshindwa kukushauri ila nina imani wengi wamekushangaa GRADUATE mtarajiwa unaleta wazo la namna hii hapa. Shughuli unayotaka kufanya hata ambaye hajasoma anafanya tu, ni UCHUUZI huo. Nilitegemea msomo uje na wazo tofauti kabisa kwa mtaji huohuo kwa kuwa kwa mjasiriamali wa kweli mil. 1 ni mtaji tosha tu.

Baada ya kukueleza haya sasa nakupa wazo, unaweza kulichukua au ukaliacha integemea kama umenielewa au utaniona nimeku-dis sana; Kwanza kabisa kwa kuwa umesoma inabidi uwe na mawazo mchemko si mgando, inabidi uwe tayari kutoka mjini kwa kuwa kwa wazo lako ulilo nalo unaonekana unaishi ama unataka kuishi mjini tu, kwa mjasiriamali hili halimfungi kwa namna yoyote.

Pili inabidi uondokane na mawazo ya biashara hizi za UCHUUZI, jaribu kufikiria mawazo ya ki-uzalishaji zaidi, (kilimo, ufugaji, viwanda n.k) na siyo duka, kwa mtazamo wangu miye kuwa na duka la kununua na kuuza (UCHUUZI) ni uvivu wa kufikiri tu, hivi uliona wapi Mzungu anauza duka bwn? Hizi ni kazi za Wahindi, ni wavivu wa kufikiri tu. Sisemi Wazungu ndo bora sana ila walio wengi wana mawazo bora, yeye anafikiria akutengenezee SIMU, uwasiliane na jamaa zako, ukishaona umuhimu wake utamtafuta tu ununue kwake na hapo utaona WAVIVU WA KUFIKIRI aka WACHUUZI wanapanga foreni kiwandani kwa Mzalishaji kuweka order ya handsets za simu, JAMAA ANAPIGA HELA. MZALISHAJI anatengeneza kitu BORA kwa kuwa anajua WAVIVU WA KUFIKIRI/WACHUUZI watamsaidia (bila wao kujua) kuuza bidhaa zake.

Ibravo nimesema sikukatishi tamaa ila ningekukubali kama ungekuja hapa na wazo kuwa kwa kuwa umeenda shule basi ungeuliza humu kuwa una mtaji wa hela hiyo (1mil) then unataka kulima Mahindi, Mpunga n.k (kwa kuwa unaonekana una interest na vitu hivyo) then upate sasa mawazo ya GREAT THINKERS. Asikwambie mtu, KILIMO ni moja ya UZALISHAJI na si UCHUUZI, wewe lima tu kitaalamu, vuna mazao yako, utaona WACHUUZI wanakuja wenyewe kutaka kuuza bidhaa zako, we unapiga hela tu unakuna kitambi (unajua tena wabongo kwa vitambi) na nikupe siri, Tsh.

1,000,000/= kuwekeza kwenye kilimo ni mtaji mkubwa mno (kama upo tayari kuondokana na mawazo ya kukaa mjini).
Huku kwetu kukodi heka moja ni Tsh. 30,000 hadi 45,000 kwa mwaka na huku kwetu kwa mwaka tunalima mara mbili (mvua za vuli na masika), kwa hela ulonayo utakuwa na heka za kutosha, sema anza na heka 5 ambayo itakugharimu Tsh. 225,000/= kukodi tu mashamba. kulima kwa tractor kila heka moja ni tsh. 40,000 x 5= 200,000/= zinazobaki fanya matumizi mengine kama palizi, mbolea na matumizi mengine kama hayo, hapa bro unazungumzia miezi mitatu tu kama ume time mvua za vuli tayari utakuwa na magunia yako 5x15= 75 ya mahindi, huku kwetu wakati wa msimu wa mavuno gunia la mahindi linauzwa Tsh. 45,000/= x 75= 3,375,000/=, kumbuka hapa umelima mvua za vuli tu, utaingia tena shambani mwezi Feb ili u-tme mvua za masika, na hakuna tena gharama ya kukodi maana ni ileile ulolipa awali, mwezi wa sita tena unavuna mazao yako unasubiria WACHUUZI tu, unapiga hela. Mkuu ukikomaa ki-jasiriamali baada ya miaka michache nina uhakika mashamba hutakodi tena, utakuwa na ya kwako, utaanza ufugaji, maana kuna uzi wa MALAFYALE Jukwaa la Ujasiriamali unasema 'Kilimo na Ufugaji kwa pamoja vinalipa' nenda kasome pale uone GREAT THINKER wanavyokuwa na mawazo ya ki-GT.
Kwa leo mkuu.
 
Hongera sana Mkuu karibu ktk ulimwengu wa fikira tofauti kwa wajasiriamali! vizuri ukifanya mwenyewe research kwa wafanya biashara na wenye maduka mbali mbali! ama kama upo tait nipe tenda hiyo Kampuni yangu inadeal na masoko inaweza kukufanyia kwa bei nafuu kabisa! my kampani ni Tangaza Marketing Solutions(TMs)

Karibu sana.
Acha tamaa wewe ,kijana ana kimillioni moja tu na wewe unataka upatemo acha upuuzi na roho mbaya, yaani tangu muambiwe mzitumie fursa basi imekuwa nongwa kila fursa mnayo ebo!! Kuwa nahuruma japo kidogo roho mbaya haijengi,.
 
Mkuu Ibravo,

Kwanza kabisa nikukaribishe humu maana unaonekana umejiunga humu this month hivyo you are still junior member, kwa kifupi humu kuna changamoto nyingi na shauri nyingi ambazo hata nyingine zinaweza kukukatisha tamaa kabisa au hata kujuta kuwa hivi nani alikushauri kuingia humu na ku-post threads za hovyo hovyo (wachangiaji wengine wanaweza kuziona hivyo), leo nikupe changamoto moja juu ya hii thread uloleta hapa:

Ibravo, sina nia ya kukukatisha tamaa juu ya mpango wako wa kuanzisha biashara ya duka hilo kwa capital hiyo ambayo umebahatika kuipata, ila to be honest nimeshangazwa na kusikitishwa na wazo hili kutoka kwako (msomi/graduate mtarajiwa). Naomba niseme wazi kuwa elimu unayosoma haijakusaidia chochote na nadhani ulikuwa unapoteza muda huko au labda ulikosea fani ulokuwa unasomea, wapo vijana wengi wanaenda vyuoni kusoma kwa mkumbo tu bila kujua anakwenda kusomea nini hasa. Lakini nadhani hapa ni uelewa wako tu ndo maana una wazo la kujiajiri, vinginevyo ningekulaumu kwa namna tofauti.

Nina imani watajitokeza wana JF wengi ambao wakisoma mchango wangu huu hawatanielewa, ila acha tu niseme ulonilazimisha kusema hasa baada ya kusoma uzi wako Ibravo.

Hata kama tunasema UJASIRIAMALI, inawezekanaje MSOMI/GRADUATE mtarajiwa unatoka chuoni unapewa mtaji wa mil 1, then unakurupuka na wazo la kufungua duka la kuuza UNGA, MCHELE n.k (UCHUUZI)? hivi hapa tutasema shule/elimu imekusaidia??? Na hapa niseme kuwa kama vijana wengi mnaenda vyuoni mnalipa fees huko miaka 2,3-4 nakuendelea, mnamaliza mnakuja na mawazo ya namna hii huku mitaji ya kiasi hiki mnabahatika kupata then niseme wazi kuwa elimu itakuwa haijawasaidia. Haya ni mawazo MGANDO, mtu unataka kufanya kitu kwa mazoea tu kwa kuwa watu wanafanya, huu si UJASIRIAMALI, ujasiriamali ni uwezo wa kubaini fursa kulingana na mtaji ulionao.

Nafurahia sana na watu wanaokuja humu kuuliza ili wapate mawazo kutoka kwa wachangiaji wanaJF great thinkers, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kutamka kiasi (initial capital) alichonacho na anaomba ashauriwe afanye shughuli gani, watu wanatoa ushauri ktk shauri hizo wanasema AKILI YA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO, then unapata shughuli ya kufanya. Ibravo nimesema sina lengo la kukukatisha tamaa ila nakueleza tu ya moyoni, wewe umeleta hapa wazo ambalo tayari unalo kichwani ndo maana watu wameshindwa kukushauri ila nina imani wengi wamekushangaa GRADUATE mtarajiwa unaleta wazo la namna hii hapa. Shughuli unayotaka kufanya hata ambaye hajasoma anafanya tu, ni UCHUUZI huo. Nilitegemea msomo uje na wazo tofauti kabisa kwa mtaji huohuo kwa kuwa kwa mjasiriamali wa kweli mil. 1 ni mtaji tosha tu.

Baada ya kukueleza haya sasa nakupa wazo, unaweza kulichukua au ukaliacha integemea kama umenielewa au utaniona nimeku-dis sana;

Kwanza kabisa kwa kuwa umesoma inabidi uwe na mawazo mchemko si mgando, inabidi uwe tayari kutoka mjini kwa kuwa kwa wazo lako ulilo nalo unaonekana unaishi ama unataka kuishi mjini tu, kwa mjasiriamali hili halimfungi kwa namna yoyote.

Pili inabidi uondokane na mawazo ya biashara hizi za UCHUUZI, jaribu kufikiria mawazo ya ki-uzalishaji zaidi, (kilimo, ufugaji, viwanda n.k) na siyo duka, kwa mtazamo wangu miye kuwa na duka la kununua na kuuza (UCHUUZI) ni uvivu wa kufikiri tu, hivi uliona wapi Mzungu anauza duka bwn? Hizi ni kazi za Wahindi, ni wavivu wa kufikiri tu. Sisemi Wazungu ndo bora sana ila walio wengi wana mawazo bora, yeye anafikiria akutengenezee SIMU, uwasiliane na jamaa zako, ukishaona umuhimu wake utamtafuta tu ununue kwake na hapo utaona WAVIVU WA KUFIKIRI aka WACHUUZI wanapanga foreni kiwandani kwa Mzalishaji kuweka order ya handsets za simu, JAMAA ANAPIGA HELA. MZALISHAJI anatengeneza kitu BORA kwa kuwa anajua WAVIVU WA KUFIKIRI/WACHUUZI watamsaidia (bila wao kujua) kuuza bidhaa zake.

Ibravo nimesema sikukatishi tamaa ila ningekukubali kama ungekuja hapa na wazo kuwa kwa kuwa umeenda shule basi ungeuliza humu kuwa una mtaji wa hela hiyo (1mil) then unataka kulima Mahindi, Mpunga n.k (kwa kuwa unaonekana una interest na vitu hivyo) then upate sasa mawazo ya GREAT THINKERS. Asikwambie mtu, KILIMO ni moja ya UZALISHAJI na si UCHUUZI, wewe lima tu kitaalamu, vuna mazao yako, utaona WACHUUZI wanakuja wenyewe kutaka kuuza bidhaa zako, we unapiga hela tu unakuna kitambi (unajua tena wabongo kwa vitambi) na nikupe siri, Tsh. 1,000,000/= kuwekeza kwenye kilimo ni mtaji mkubwa mno (kama upo tayari kuondokana na mawazo ya kukaa mjini).
Huku kwetu kukodi heka moja ni Tsh. 30,000 hadi 45,000 kwa mwaka na huku kwetu kwa mwaka tunalima mara mbili (mvua za vuli na masika), kwa hela ulonayo utakuwa na heka za kutosha, sema anza na heka 5 ambayo itakugharimu Tsh. 225,000/= kukodi tu mashamba. kulima kwa tractor kila heka moja ni tsh. 40,000 x 5= 200,000/= zinazobaki fanya matumizi mengine kama palizi, mbolea na matumizi mengine kama hayo, hapa bro unazungumzia miezi mitatu tu kama ume time mvua za vuli tayari utakuwa na magunia yako 5x15= 75 ya mahindi, huku kwetu wakati wa msimu wa mavuno gunia la mahindi linauzwa Tsh. 45,000/= x 75= 3,375,000/=, kumbuka hapa umelima mvua za vuli tu, utaingia tena shambani mwezi Feb ili u-tme mvua za masika, na hakuna tena gharama ya kukodi maana ni ileile ulolipa awali, mwezi wa sita tena unavuna mazao yako unasubiria WACHUUZI tu, unapiga hela. Mkuu ukikomaa ki-jasiriamali baada ya miaka michache nina uhakika mashamba hutakodi tena, utakuwa na ya kwako, utaanza ufugaji, maana kuna uzi wa MALAFYALE Jukwaa la Ujasiriamali unasema 'Kilimo na Ufugaji kwa pamoja vinalipa' nenda kasome pale uone GREAT THINKER wanavyokuwa na mawazo ya ki-GT.
Kwa leo mkuu.

Hii ipo poa sana.

Na ulilosema brother ni kwel lazma msomi ujasilimali wako uwe wa kisomi na sio bora tu kisa ujasilia mali basi uufanye hata hovyo hovyo.
 
coomon man anaweza kuwa na bei nzuri,mfano kuna kampuni moja pale kenya wanakufanyia market research kwahizi biashara ndogondogo kwa gharama haifiki hata elfukumi ya kibongo.wanakupa full infor kuhusu biashara husika,mfano capital ya kuanza nayo,process ya kuanzisha,location inayofaa,rent ya flame,maunjanja katika biashara husika etc.
Hii ni kweli, hembu nipe jina au contact yahiyo Kampuni ya kenya,maana lazima tugawane majukumu.
 
Hongera sana Mkuu karibu ktk ulimwengu wa fikira tofauti kwa wajasiriamali! vizuri ukifanya mwenyewe research kwa wafanya biashara na wenye maduka mbali mbali! ama kama upo tait nipe tenda hiyo Kampuni yangu inadeal na masoko inaweza kukufanyia kwa bei nafuu kabisa! my kampani ni Tangaza Marketing Solutions(TMs)

Karibu sana.
Weka website yenu tuone utendaji wenu,ulaya kampuni kama hizi zinalipa sana,ila hapa Bongo usanii mtupu
 
Mkuu Ibravo,
Kwanza kabisa nikukaribishe humu maana unaonekana umejiunga humu this month hivyo you are still junior member, kwa kifupi humu kuna changamoto nyingi na shauri nyingi ambazo hata nyingine zinaweza kukukatisha tamaa kabisa au hata kujuta kuwa hivi nani alikushauri kuingia humu na ku-post threads za hovyo hovyo (wachangiaji wengine wanaweza kuziona hivyo), leo nikupe changamoto moja juu ya hii thread uloleta hapa:

Ibravo, sina nia ya kukukatisha tamaa juu ya mpango wako wa kuanzisha biashara ya duka hilo kwa capital hiyo ambayo umebahatika kuipata, ila to be honest nimeshangazwa na kusikitishwa na wazo hili kutoka kwako (msomi/graduate mtarajiwa). Naomba niseme wazi kuwa elimu unayosoma haijakusaidia chochote na nadhani ulikuwa unapoteza muda huko au labda ulikosea fani ulokuwa unasomea, wapo vijana wengi wanaenda vyuoni kusoma kwa mkumbo tu bila kujua anakwenda kusomea nini hasa. Lakini nadhani hapa ni uelewa wako tu ndo maana una wazo la kujiajiri, vinginevyo ningekulaumu kwa namna tofauti.

Nina imani watajitokeza wana JF wengi ambao wakisoma mchango wangu huu hawatanielewa, ila acha tu niseme ulonilazimisha kusema hasa baada ya kusoma uzi wako Ibravo.
Hata kama tunasema UJASIRIAMALI, inawezekanaje MSOMI/GRADUATE mtarajiwa unatoka chuoni unapewa mtaji wa mil 1, then unakurupuka na wazo la kufungua duka la kuuza UNGA, MCHELE n.k (UCHUUZI)? hivi hapa tutasema shule/elimu imekusaidia??? Na hapa niseme kuwa kama vijana wengi mnaenda vyuoni mnalipa fees huko miaka 2,3-4 nakuendelea, mnamaliza mnakuja na mawazo ya namna hii huku mitaji ya kiasi hiki mnabahatika kupata then niseme wazi kuwa elimu itakuwa haijawasaidia. Haya ni mawazo MGANDO, mtu unataka kufanya kitu kwa mazoea tu kwa kuwa watu wanafanya, huu si UJASIRIAMALI, ujasiriamali ni uwezo wa kubaini fursa kulingana na mtaji ulionao.

Nafurahia sana na watu wanaokuja humu kuuliza ili wapate mawazo kutoka kwa wachangiaji wanaJF great thinkers, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kutamka kiasi (initial capital) alichonacho na anaomba ashauriwe afanye shughuli gani, watu wanatoa ushauri ktk shauri hizo wanasema AKILI YA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO, then unapata shughuli ya kufanya. Ibravo nimesema sina lengo la kukukatisha tamaa ila nakueleza tu ya moyoni, wewe umeleta hapa wazo ambalo tayari unalo kichwani ndo maana watu wameshindwa kukushauri ila nina imani wengi wamekushangaa GRADUATE mtarajiwa unaleta wazo la namna hii hapa. Shughuli unayotaka kufanya hata ambaye hajasoma anafanya tu, ni UCHUUZI huo. Nilitegemea msomo uje na wazo tofauti kabisa kwa mtaji huohuo kwa kuwa kwa mjasiriamali wa kweli mil. 1 ni mtaji tosha tu.

Baada ya kukueleza haya sasa nakupa wazo, unaweza kulichukua au ukaliacha integemea kama umenielewa au utaniona nimeku-dis sana; Kwanza kabisa kwa kuwa umesoma inabidi uwe na mawazo mchemko si mgando, inabidi uwe tayari kutoka mjini kwa kuwa kwa wazo lako ulilo nalo unaonekana unaishi ama unataka kuishi mjini tu, kwa mjasiriamali hili halimfungi kwa namna yoyote.

Pili inabidi uondokane na mawazo ya biashara hizi za UCHUUZI, jaribu kufikiria mawazo ya ki-uzalishaji zaidi, (kilimo, ufugaji, viwanda n.k) na siyo duka, kwa mtazamo wangu miye kuwa na duka la kununua na kuuza (UCHUUZI) ni uvivu wa kufikiri tu, hivi uliona wapi Mzungu anauza duka bwn? Hizi ni kazi za Wahindi, ni wavivu wa kufikiri tu. Sisemi Wazungu ndo bora sana ila walio wengi wana mawazo bora, yeye anafikiria akutengenezee SIMU, uwasiliane na jamaa zako, ukishaona umuhimu wake utamtafuta tu ununue kwake na hapo utaona WAVIVU WA KUFIKIRI aka WACHUUZI wanapanga foreni kiwandani kwa Mzalishaji kuweka order ya handsets za simu, JAMAA ANAPIGA HELA. MZALISHAJI anatengeneza kitu BORA kwa kuwa anajua WAVIVU WA KUFIKIRI/WACHUUZI watamsaidia (bila wao kujua) kuuza bidhaa zake.

Ibravo nimesema sikukatishi tamaa ila ningekukubali kama ungekuja hapa na wazo kuwa kwa kuwa umeenda shule basi ungeuliza humu kuwa una mtaji wa hela hiyo (1mil) then unataka kulima Mahindi, Mpunga n.k (kwa kuwa unaonekana una interest na vitu hivyo) then upate sasa mawazo ya GREAT THINKERS. Asikwambie mtu, KILIMO ni moja ya UZALISHAJI na si UCHUUZI, wewe lima tu kitaalamu, vuna mazao yako, utaona WACHUUZI wanakuja wenyewe kutaka kuuza bidhaa zako, we unapiga hela tu unakuna kitambi (unajua tena wabongo kwa vitambi) na nikupe siri, Tsh. 1,000,000/= kuwekeza kwenye kilimo ni mtaji mkubwa mno (kama upo tayari kuondokana na mawazo ya kukaa mjini).
Huku kwetu kukodi heka moja ni Tsh. 30,000 hadi 45,000 kwa mwaka na huku kwetu kwa mwaka tunalima mara mbili (mvua za vuli na masika), kwa hela ulonayo utakuwa na heka za kutosha, sema anza na heka 5 ambayo itakugharimu Tsh. 225,000/= kukodi tu mashamba. kulima kwa tractor kila heka moja ni tsh. 40,000 x 5= 200,000/= zinazobaki fanya matumizi mengine kama palizi, mbolea na matumizi mengine kama hayo, hapa bro unazungumzia miezi mitatu tu kama ume time mvua za vuli tayari utakuwa na magunia yako 5x15= 75 ya mahindi, huku kwetu wakati wa msimu wa mavuno gunia la mahindi linauzwa Tsh. 45,000/= x 75= 3,375,000/=, kumbuka hapa umelima mvua za vuli tu, utaingia tena shambani mwezi Feb ili u-tme mvua za masika, na hakuna tena gharama ya kukodi maana ni ileile ulolipa awali, mwezi wa sita tena unavuna mazao yako unasubiria WACHUUZI tu, unapiga hela. Mkuu ukikomaa ki-jasiriamali baada ya miaka michache nina uhakika mashamba hutakodi tena, utakuwa na ya kwako, utaanza ufugaji, maana kuna uzi wa MALAFYALE Jukwaa la Ujasiriamali unasema 'Kilimo na Ufugaji kwa pamoja vinalipa' nenda kasome pale uone GREAT THINKER wanavyokuwa na mawazo ya ki-GT.
Kwa leo mkuu.
Ubarikiwe sana.
Ashindwe mwenyewe japo labda alikuwa anataka kufanya hiyo biashara kwa kukuzia mtaji lakini bado ingemchukua muda kiasi.
 
Naunga mkono hoja ya Clik hapa..vile vile milion moja ni pesa ndogo sana kwa biashara ya duka hapa mjin,ukinunua frij na kutengeneza shelf pesa ishaisha+kodi ya chumba cha biashara ambayo kiwango cha chin ni sh elfu 50 kwa mwez*miez sita, angalia fulsa nyingine mkuu au ongezea hyo pesa.
 
Naunga mkono hoja ya Clik hapa..vile vile milion moja ni pesa ndogo sana kwa biashara ya duka hapa mjin,ukinunua frij na kutengeneza shelf pesa ishaisha+kodi ya chumba cha biashara ambayo kiwango cha chin ni sh elfu 50 kwa mwez*miez sita...angalia fulsa nyingine mkuu au ongezea hyo pesa
nakuunga Mkono kaka shankal, ila ushauri wangu mie angaweza kufanya biashara mbadala ya uzalishaji kwa mtaji wake huo huo. kama ifuatavyo
1. biashara ya kuuza barafu
  • eneo/ Soko: wauza maji wote walipo kando kando ya barabara, mama lishe na majirani wengine ambao hawana mafrihi ya kupozea maji ya kunywa( haswa uswahiliniI) Unachotakiwa kufanya ni kila unapotoka/ kwenda chuoni jitahidi kufanya utafiti hata kuuliza size za barafu na kutangaza biashara yako japo kwa kdgo uone kwa kila kituo unapata order ngapi/ mda mwingine kuna jamaa wanakuja kununua( mia kwa barafu) kwa jumla hapo kwako wenyewe wanasambaza kwa wengine( 200 wakienda kuuza road).
  • Mtaji: upo wa aina mbili. Mtaji wa kutokuwa na aibu( kuondoa aibu kubeba barafu asubuhi wakati wenzako wamepiga kadeti na tai wewe beba barafu zako peleka kwa customer zako..
  • Mtaji wa Pesa/vitendea kazi( Friza nakushauri ununue mpya na ya kusimama( friza maalumu kwa barafu) kabisaa kama ukipata used uwe umefanya uchunguzi wa kutosha na usijilaumu baadaye. Ukinunua jipya wapata warranty ndefu na mtumba wapewa waranty muda mfupi.. kingine cha ziada bei za friza zinategemeana zinacheza kuanzia laki 7 mpaka 2 million kulingana na brand name na size ya friza. pesa inayobakia ni kuandika bango(kitambaa cha matangazo kuwa unauza barafu kwenye njia kuu ambapo unawalenga wale wateja wako uliowapitia na wengine ambao watasoma (wale wa Jumla jumla) Mtaji mwingine ni ndoo ya maji(20 lita) na kikombe na vikaratasi vya barafu ( nenda kariakoo kanunue kwa jumla then unaanza kazi)
  • Mapato: ukiwa unaanza itakupa shida ila jitahidi uwe mbunifu wa biashara yako na jiwekee malengo ya kuuuza angalau barafu 50 kwa siku ziwe kubwa na zigande ziwe chuma(jiwe) ukiuuza kwa reja reja (150*50= 7500) na ukiuza kwa jumla ni (100*50=5000) mahali pengine unaweza ukauza kwa reja reja hata 200 kulingana na bei ya soko/eneo. wingi wa barafu inategemeana na ukubwa wa friza yako
  • Gharama;Friza mpya inaweza ikala unit 4 za umeme kwa masaa 24( makisio tu), ukiweka nauli na gharama nyingine za ziada weka 15000 kwa mwezi.. bei ya unit moja ya umeme ni 400-420 ukizidisha kwa mwezi unapata( 4*30*420=50400)+ 15000= 65400 fanya na mawasiliano unajunga kwa mwezi iwe elfu 70000.
  • FAIDA: NI mapato toa gharama( kama ifuatavyo
  • kwa mauzo ya rejareja ya mia kwa mwanzoni (50 barafu)*150 ((150*50*30= 225000)-gharama(70000)=155000) mengine kwa bei ya 200 na bei ya jumla ya mia utapga mwenyewe.
naomba kuwakilisha... USAKAPESA OYEEEEEEEEEE :yield::yield::israel::israel::israel::israel:
 
Last edited by a moderator:
Ooh thanks Mkuu I was well taught then,

HABARI WAKUU,

Cash maney nakushukuru sana kwa mwongozo wako wa namna ya kutunza kumbukukumbu za Duka. hata hivyo mimi nina shida kidogo namna ya ku itemize bidhaa hizo katika vitabu husika.

Kwa mfano kitabu cha manunuzi, au kitabu cha mauzo, nita itemize vitu gani? Nikichora Table nitaiwekaje kuonesha bidhaa zilizonunuliwa?
Samahani ndugu kwa usumbufu. Ingawa posti ni ya siku nyingi lakini ni ya manufaa.

Tafadhali ndugu nisaidie.
by Cassava a.k.a (Mhogo)
 
HABARI WAKUU,

Cash maney NAkushukuru sana kwa mwongozo wako wa namna ya kutunza kumbukukumbu za Duka. hata hivyo mimi nina shida kidogo namna ya ku itemize bidhaa hizo katika vitabu husika.

kwa mfano kitabu cha manunuzi, au kitabu cha mauzo, nita itemize vitu gani? Nikichora Table nitaiwekaje kuonesha bidhaa zilizonunuliwa?

samahani ndugu kwa usumbufu. Ingawa posti ni ya siku nyingi lakini ni ya manufaa.

tafadhali ndugu nisaidie.
by Cassava a.k.a (Mhogo)

Mbona rahisi tu we fanya hivi

Tengeneza table itakayokuwa navichwa vya habari kama vile:- 1.item no (number). 2. Item description (mzigo uliochukua/jina) , 3. quantity (jumla ya mzigo iliochukua) , 4, rate (bei ya kila kimoja) ,5 Amount ( jumla ya hela uliyolipa)
ukitengezeka kama hapo juu na kila ukileta mzigo unaigiza kwenye sheet/ukurasa wake itakurahishia kujua unatia kiasi gani, kingine usisahau pia kuingiza garama ya kugikisha mzigo kwenye frame yako I.e garama ya usafiri.
 
Back
Top Bottom