Biashara ya day care, ajira mkononi

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
929
1,278
Habari, ndugu na jamaa wa jukwaa hili pendwa la biashara, leo nataka kuweka uzoefu wangu wa mwaka mmoja wa kuanzisha, kusimamia, kuendesha na kufundisha nussery and day care kwa hapa mjini , hii baada ya kuacha biashara ya kuuza viatu , sio kwamba ninauzoefu wa mda mrefu sana, hapana, ila lengo langu ni kuwapa watu mwanga wa namna ya kuona fursa zilizopo kwenye biashara hii, namna ya uendeshaji, usajili, changamoto, faida, soko lake, mtaji wa kuanzisha n.k. pia naomba mnisamehe pale nitakapokuwa na lugha isiyonyooka kwa maana najijua ninamatatizo ya kuchanganya kati ya r na l. twende pamoja
AINA ZA DAY CARE
kuna aina kuu tatu za day care kwa mujibu wa uzoefu wangu mimi, sio wizara. aina ya kwanza ni
day care za kitajiri mfano day care za feza
day care za watu wa kati.
day care za watu wa chini, hapa ndio soko lilipo......kunamsemo unasema ukitaka pesa, wanazo masikini, wakina MO wanajua ndio maana wanauza juice ya kopo 200, U-fresh anajua anauza juice 200, so mimi nitajikita hapa kwenye day care ya watu wa chini.

USAJILI
hizi day care zipo chini ya wizara ya maendeleo ya jamii, hivyo kwa maana nyingine zipo chini ya afisa maendeleo ya jamii wa kata,au wilaya. hivyo unapotaka kuanzisha ni jukumu lako kumfuata afisa maendeleo wa eneo husika, lakini pia kwa upande wa shule za nussery zipo chini ya wizara ya elimu. hapo nadhani tupo pamoja. usajili, unakwenda kwa awamu, afisa anakuja anakutembelea, atakueleza mapungufu yaliyopo kisha unaweka sawa kidogo kidogo mpaka unakaa sawa, msiwaogope maana ni watanzania wote maisha yanafanana tu, kwa upande wa nussery hivyo hivyo, japo kwenye makaratasi yao na sheria vimejaa vitu vingi lakini mnaenda taratibu mpaka mnafika lengo.

ENEO
kwa mujibu wa sheria zao shule au kituo kinaitajika kiwe na eneo kubwa la watoto kwa lengo la michezo, je mjini hapa hayo maeneo yanapatikana???? ukiingia kwenye game utaelewa mambo mengine kwa undani
zaidi., pia eneo liwe na michezo ya watoto, mazingira mazuri na ulinzi wa kutosha.

VIFAA NA MIUNDOMBINU
vifaa vinavyohitajika ni slide, bembea za watoto, bembea za mizani ya watoto, mpira, kamba, midoli, n.k pia madarasa angalau matatu na kuendelea.je unapate madarasa?? penye ugumu ndio penye pesa, tafuta nyumba ya mtu kisha kodisheni, madara tosha hayo, kuwepo na viti, vitabu chaki na ubao.

SOKO LA DAY CARE
soko la day care kwa sasa ni kubwa sana, kwa maana kuna uhaba mkubwa wa wafanyakazi wa ndani kwa jamii ya sasa, hasa maeneo ya mijini, kama vile dar, hivyo wazazi wanatafuta sehemu ya kuwapeleka watoto wao kwa lengo la kusoma na pia kulelewa ili wao waendelee na shughuri zao, wapo tayali kulipa gharama tena kwa kukubembeleza ili uweze kukaa na watoto wao. hivyo hiyo ndio fursa ya kupiga pesa mapemaaaa au baridiiiii JK VOICEEEEE,
wazazi wanataka ulinzi na amani kwa watoto wao. ndio maana unaona kila kona zimejaa day care na bado hazitoshi, je hawa watu wa chini wanaweza kulipa ada ya shule, mimi nitakupa mfano shule yangu inamwanafunzi ambaye mama yake anauza machungwa na miogo ya kutembeza kichwani, lakini huyu mama analipa ada kwa mwezi, tena bila ubishi,je analipaje??? umiza kichwaa, ningeweza kufafanulia tatizo vijana wa FEDHA HOUSE hawakawii kuja na maboresho ya muswada. pia njia za kujitangaza zinajulikana kwa kila mmoja, castumer care pia muhimu, pia kuwapa huduma nzuri na kuonesha upendo kwa watoto.
soko hasa la huduma hii ni maeneo yenye watu wengi, maeneo yenye foleni kubwa za magari, maeneo ya uswahilini,kama vile mbagara, gongo la mboto, tandika, buza, chanika n.k,

GHARAMA ZA KUANZISHA
kodi nyumba nzima...........
bembea za iana zote
mshahara wa mdada wa kazi au mpishi
mwalimu
kuchora eneo la shule
viti, kanunue kiwandani
ubao
chaki
n.k

MALIPO YA ADA NA CHAKULA
inategemea na wewe, kwa kuwa ni uswazi malipo yawe hivi kwa mwezi au kwa wiki au kwa siku.....hii ni kwa chakula tu, ila kwa ada malipo yafanyike kwa mwezi.

MUDA WA KUTOKA
hapa kwa kuwa lengo lao ni kuwatazamia watoto wao, wakati wao wanaenda kupiga kazi kwa wachina, wewe weka mpaka jioni, mzazi atakapoludi kumchukua mtoto wake,mara nyingi ni kuwa mwisho saa 12 jioni, muda kuingia weka kuanzia saa 12:30 asb.

SARE ZA SHULE
shule hizi mara nyingi wenye maamuzi ni wanawake, hivyo ili uweze kuteka soko ni bora ukatafuta sare za kuvutia, hapo utawapata wakinamama kibao, kwa maana anapoona mtoto amependeza, na yeye atataka amlete mwanae.

CHANGAMOTO
Changamoto kubwa kuwa wazazi wanasumbua kulipa ada, watoto mara kibao huwa wanaongezeka na kupungua, hii kutokana na kuhama hama kwa wazazi, kuachiwa mtoto mpaka mda unapitiliza, watoto kulia lia muda mwingine kwa kuwakosa wazazi wao, watoto kupotea usipokuwa mwangalifu, watoto kutoroka n.k

FAIDA YAKE
kupata pesa ya mapema tu, kujiali, kutoa ajira, kuwa boss, ndio mwanzo wa kufungua shule kubwa, kutatua matatizo ya jamii yako.

MAONI YANGU
vijana ambao wanaangaika kutafuta ajira na wamemaliza ualimu au hata kama ujamaliza ualimu, mkiwa wawili tu inatosha kuanzisha hii biashara, kinachofuata utaniuliza mtaji napata wapiii???subili nitakujibu

NB: UKITHUBUTU, UTAFANIKIWA
kama kuna ambayo sikuyasema hapa, basi nitayasema kwenye maswali na majibu, sioni maana ya mtu kuja PM, lakini piaa kuna ambayo sijayasema kwa maana yanakuwa ni siri za biashara hivyo huwezi kuweka wazii, pia siwezi kuwatumia picha ya shule yangu kwa maana maalumu, mtanisamehe kwa hilo pia.i....wape salaaam, morson amesign simba.
 
Umefafanua vizur sana mkuu.

Maana umechanganua faida na changamoto zake,kiufupi umeelezea ukweli kuwapata watoto wa kujiunga ni rahisi sana ugumu wake huwa ikifika mwisho wa mwezi kwenye malipo wazazi huwa wanatoa excuses sana utadai hadi kichwa kiume.

Uzur ni kwamba utawapata baadhi ya wazazi watakaokuwa wanakulipa bila usumbufu hiyo itakuwa inakusogeza kupata hela ndogondogo za kula.
 
Back
Top Bottom