🤣🤣 Dah! Biashara huwa changamoto kweli yani lazima ujitoe kaka, ku compete na watu wanaoleta mzigo mkubwa kwa pamoja sokoni sio rahisi, na kasumba mbaya ni ile ya wafanya biashara kutaka uwaachie mzigo alafu wakulipe baada ya kuanza kuuza, Nakushauri uende kijijini tafuta mzigo quality, njoo nao kidogo alafu uza bei nafuu hata kama hutapata faida, wakishakujua maramoja leta mzigo mkubwa zaidi. Kuhusu soko angalia mzunguko wa general tu usitafute wateja kama huna dagaa mkononi
Unaweza kunichek inbox au uweke namba yako hapa, Maana nimefanya hiyo biashara kidogo angalau