Nenda kwa tahadhali sana mkuu miongoni mwa miji iliyo jaa wafanya biashara matapeli na washamba wanao jiona wajanja ni pamoja na Katoro.
Ukanda ule elimu kwa sababu ilichelewa kufika sana watu wengi sana katika biashara yao wanaamini sana katika ushirikina na sio kuboresha biashara.
Ni kweli ni biashara utayo pata fedha ila nakushauli uanpo anzisha ile biashara kwa pale Katoro usimuamini mtu mapema hata unae fahamiana nae ukisikia anaishi katoro chukua tahadhali kubwa kwa maana mimi mwenyewe ni muhanga nimewahi kutapeliwa pale milioni nane na laki sita.
Nilikua nafanya biashara ya kufyatua tofali za udongo na kuzichoma na kuuza na pia nilikua naishi nje ya katoro pale kulikua na wasimamizi.
Siku nimeenda na mteja kuuza tofali zangu nikakuta jamaa alisha ziuza na fedha kaisha kula tukaanza kuhangaishana kesi polisi mara mahakamani ambayo kimusingi nilipoteza pesa nyingine na mda