Biashara ya bodaboda!

Claranito

Member
May 26, 2014
28
3
Habari zenu wadau!

Natamani kufanya biashara ya bodaboda kwa maana ya kununua bodaboda na kutafuta dereva wa kuendesha wateja lakini sina uzoefu nayo. Naomba kwa wenye uzoefu tushauriane hasa kwenye mambo yafuatayo; marejesho kwa siku, maeneo gani ni mazuri kibiashara hiyo, aina gani ya bodaboda ambayo ni nzuri kibiashara na mambo mengine yafaayo kuyajua juu ya biashara hiyo.

Naimani mtanisaidia.

Asanteni
 
PIKIPIKI nzuri: boxer ikifuatiwa na sunlg then fekon.
Hesabu : inategemea makubaliano na eneo, ila sio chini ya Elfu 7 kwa siku.
ENEO LA KAZI : Eneo lenye Barabara ya lami ni zuri zaidi ili pikipiki isichakae mapema ila changamoto ni ajali Kwani penye wengi pana mengi.
Ninao uzoefu kiasi hiyo shuhuli.
 
Ingia makubaliano ya kukulipa 10,000 baada ya miezi 10 inakuwa ya kwake.

Hata kusumbua na ataitunza sana
 
Chukua ushauri wa Peri,
Hiyo ndio hesabu ya siku kwa sasa,na kuhusu eneo hilo anajua Dereva utakaempa,maana huwezi kumpangia kituo.
Pia ujue kwamba anakuwa analala nayo yeye(Sio Kitandani).
Hesabu ni Tsh:7,000 kwa siku na analipa kwa wiki kama anaweza kutunza,ila wapo wengien wanalipa kwa siku ila sio wengi.
Pia wapoa mabao kwa wiki anakupa Tsh:50,000
Hesabu yote hapo Services ni kwa Dereva.
Halafu hakikisha unamuandikisha mkataba kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa akiwa na mdhamini.(usikurupuke kichwa kichwa utakuja kulia)

Hesabu ya Tsh:10,000 kwa siku ili baada ya miezi kumi au mwaka iwe yako ni mfumo umepitwa na wakati na mara nyingi ulikuwa ni kwa pikipiki hizo za Sunlg au tetemesha makalio amabpo bei ya ni kati ya 1,600,000 kama sikosei,maana hesabu ya kuipata hiyo 10,000 kwa siku ni ngum kwa biashara ilivyo kwa sasa na pia itakuwa sio biashara yenye malengo.
Maaana ingekuwa hivyo basi Wenye madaladala nao wangefanya hivyo ili baadae madereva na makondakta yawe yakwao.
Nunua Boxer ndio itakutoa na ndio madereva na abiria pia wanaipenda sana,hii itamsadia Dereva wepesi wa kazi yake na yeye aweze kupata pesa ya kula na kukurejeshea pia ni imara sana na zinadum miaka zaidi ya miwili,hizo nyingine hazipendwi sana,maana zinatetemeka,sasa hadi abiria afike anakoenda akishuka anaona kama ------ yanatetemeka lazima ageuke nyuma aulize je kulikoni au kunamtu anamkobea.Na hata Dereva nae akilala usiku anaona ---- linacheza,kazikweli

Chukua kitu Boxer:Muda wake wa kudum kwa ubora wake ni Miaka miwili.

Ni Bishara nzuri ukipata Dereva mzuri,hakkisha inakuwa na full Bima na dereva unamnunulia helmets na unamuwekea full tank wkas siku ya mwanzo kama mtaji kisha unamkadhi unasuburia hesabu yako.

Mie ninazo kama sita zipo njiani,na changamoto ndio kama hizo,Madereva wengine ndio wengine mpaka mpigiane sim arushe ziko moja au mbili,ilasiku zinaenda hakuna biashara amabayo haina changamoto.

Boxer mpya kwa sasa pamoja na Bima,Helmets,na kama ukimtilia Driver mafuta full tagi inakaribia 2,300,000

Mie Pikipiki zangu huwa nabadiisha kila baada ya miezi sita,nakuwa nauza,kama unapesa ninayo moja imenunuliwa mwaka jana mwezi wa kumi na mbili,nimeishanunua nyingine ku replace hiyo,sasa ile ninanuza ikiwa na full Bima mpaka mwezi wa kumi na mbili.
Hii Hapa lete pesa kisha anza kazi hapo hapo,maana inakila kitu na ilikuwa unapatiwa services kila muda wake muafaka.
Kama unafundi anaweza kujakukusaidi kuangalia.
1.8m tu unasepa nayo(Number C )
Hii Hapa

Photo0633.JPG Photo0633.JPG
 
Kiongozi Zanzibar spices hz pkpk za BOXER mpya dukani yauzwaje?
Na hapo nyuma hakuna sehemu ya kuwekea mzigo (carrier)?
 
daah hakuna biashara kichaa kama ya piki piki. kiufupi mtu mwenye akili timamu hawez kufanya biashara hii
 
Nomefanya biashara hii Kwa miaka almost miwili, kama biashara zingine ina changamoto zake Kwa eneo nilipo hesabu ni 50,000/ wk changamoto ni kwamba vijana ni waharibifu sana so ninachofanya ni kukaa na pikipiki Kwa mwaka mmoja ukiisha nauza makusanyo yoote nakuuza ninanunua pikipiki mpya na nabakia na faida ambayo si chini ya 1,300,000 Kwa mwaka.
 
Asante kwa kushare nasi. Umenifumbua macho.
 
daah hakuna biashara kichaa kama ya piki piki. kiufupi mtu mwenye akili timamu hawez kufanya biashara hii

Usikatishe wenzio tamaa.
Mana siku hizi kuna watu wanamilki pikipiki kisha wakiona wenzao wanatka kununua wanawakatisha wenzao tamaa kama huyu.
Kila mtu na riziki yake na akili yake.
Kwani wanaomiliki mbona wapo na wanaendelea.We unafikiria kuna biashara utafanya kimama bila changamto.EBBO
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom