Wadau,
Watu wengi sana kwasasa wanataka kuanzisha radio, mwamko huu ukiendelea hivihivi kwakweli frequency zitajaa sana katika miji mikubwa! Ninachotaka kuzungumzia leo ni hoja ndogo tu kwamba ni nini kinatakiwa kuanza unapokuwa unataka kufungua kituo cha radio:-
1. Kuandaa utaratibu wa kuomba leseni.
Hapa kuna mambo makubwa mawili, 1. Kufanya upembuzi yakinifu (Feasibility Study), na 2. Ni kuandika documents zote zinazotakiwa kwa ajili ya kuambatanisha kwenye maombi ya leseni.
Feasibility Study ni muhimu sana japo radio nyingi hazikufanya. Hii ndiyo itaelezea uhalisia wa mradi wako kwa 100%. Na hii ndiyo itatoa bajeti halisi itakayotakiwa, masuala ya vipindi na wasikilizaji na mambo mengine yote muhimu.
Ukishamaliza hatua hii sasa mengine ni hatua za baadaye zinazofuata. Mnaotaka kuomba leseni kwa ajili ya kuanzisha radio hii hatua ni muhimu sana wakati unaweka sawa mambo mengine. gharama za maombi ya leseni TCRA ni $1000. Na gharama za kuandikiwa maandiko haya na kufanyiwa feasibility study ni Tshs 2,000,000/=
Asanteni.