Wewe kwa lugha ya kifinance unaitwa "Loan Shark" .
Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, tumia mwanasheria katika hiyo biashara yako. Mfano unaweza ukawa na mwanasheria mmoja ambaye mnakubaliana kuwa utamlipa amount flan for initial draft ya mkataba halafu katika kila mkopo unamlipa mfano 5% kwa certification. Hiyo 5% utakuwa unamkata mteja husika. So mtu anayekopa 100,000 ajue atalipia pesa ya mwanasheria 5,000 au kwa maana nyingine atapokea 95,000.
Mwanasheria atakusaidia kudesign mkataba uwe within the limits of the law ili uweze kuwa enforciable kwenye mahakama in case of default. Hiyo biashara kuna mahali ikifika lazima utatakiwa kuiweka rasmi. Watu wengi tunaowaona wameendelea kibiashara walianzia biashara ambazo siyo rasmi.