Biashara bora ya kuanzisha.?

Biashara bora ya kuanzisha.?

Naamini hakuna kitu kigumu kama hiki cha kuamua ni biashara gani ufanye, na hapa ukijichanganya kuzika mtaji ni jambo la muda tu.

Kuna wataalam watakuja mkuu, naamini watatusaidia wengi.
 
Kama wewe ndio mtendaji mkuu basi biashara rahisi kuisimamia ni ile unayoipenda, ila kama utatumia pesa watu wafanikishe kuendesha na kutatua changamoto na wewe uwe muwezeshaji na mtu wa kuhoji na kusimamia watekelezaji, basi biashara yoyote ni rahisi.

Biashara zote zina changamoto zake, utatuzi wa changamoto unahitaji akili, ubunifu na uvumilivu, kuna muda utapata hasara, kama wewe ndio mtendaji mkuu unaetakiwa kufikiri kila kitu na kukiweka kwenye utekelezaji ili kutatua changamoto, kama unachokifanya hukipendi itafika hatua utaona unateseka bure tu. Ila kama utatumia pesa kuwafanya watu wafikiri kwa ajili ya biashara yako, wakuletee mawazo, uyachakate na uamrishe kipi kifanyike vipi, basi fanya yoyote tu.

Zingati sio kila biashara ni ya kila mtu. Biashara iliyomtoa flani sio kweli kwamba ukifanya vilevile bila kupindisha itakutoa na wewe
 
Kama una pesa ya kununua bajaj mpya usinunue anzisha biashara Uza spare parts za pikipiki , pikipiki ni nyingi sana kuliko kwenda na wewe kutega kusubiri abiria we nenda kawatege wamiliki wa pikipiki kwenye matengenezo.
 
Nadhani majibu mazuri umeshayapata hapo juu kwa wachangiaji wa juu wote wametoa majibu mazuri na yenye mantiki,hapa sina cha kuongeza zaidi ya kukazia tu.
Hakuna biashara itakulipa kama hujaipenda kutoka moyoni,biashara yoyote ukiipenda kutoka moyoni na ukashiriki kikamilifu kwa asilimia mia itakufanya uongeze ubunifu kila siku na kuwa mvumilivu kwa kipindi kirefu baadae itakulipa tu.
Ila ukisema uanzishe biashara halafu utegemee mtu mwingine ndio afanye kisha awe anakurushia pesa tu za mauzo lazima utafeli,ni biashara ya majengo tu yaani real estate ndio unaweza kukaa tu nyumbani kisha unarushiwa pesa yako kwa sababu mpangaji hana ujanja wa kukimbia na nyumba yako.
 
Kwa kweli niwashukuru wote mlioichukua changamoto yangu na kuamua kunisaidia mawazo yenu. Naahidi kurudi hapa na ushuhuda wa mafanikio baada ya miezi michache ya utendaji. Mungu awabariki sana.
 
Kama wewe ndio mtendaji mkuu basi biashara rahisi kuisimamia ni ile unayoipenda, ila kama utatumia pesa watu wafanikishe kuendesha na kutatua changamoto na wewe uwe muwezeshaji na mtu wa kuhoji na kusimamia watekelezaji, basi biashara yoyote ni rahisi.

Biashara zote zina changamoto zake, utatuzi wa changamoto unahitaji akili, ubunifu na uvumilivu, kuna muda utapata hasara, kama wewe ndio mtendaji mkuu unaetakiwa kufikiri kila kitu na kukiweka kwenye utekelezaji ili kutatua changamoto, kama unachokifanya hukipendi itafika hatua utaona unateseka bure tu. Ila kama utatumia pesa kuwafanya watu wafikiri kwa ajili ya biashara yako, wakuletee mawazo, uyachakate na uamrishe kipi kifanyike vipi, basi fanya yoyote tu.

Zingati sio kila biashara ni ya kila mtu. Biashara iliyomtoa flani sio kweli kwamba ukifanya vilevile bila kupindisha itakutoa na wewe
Nakazia hapa👿!!
 
Back
Top Bottom