Emmanuel josh
New Member
- May 13, 2019
- 0
- 11
Habari wana jukwaa wenzangu karibuni na msome makala yangu
Tuangalie biashara 5 za mtaji mdogo usiozidi Tshs. 100,000 unazoweza kufanya na zenye faida kubwa. Mtaji mkubwa unaohitajika unapoanzisha biashara ni muda na wala sio pesa kama utakavyojifunza hapa.
Mimi binafsi siamini kama kuna biashara ndogo, ila najua kuna biashara unaweza kuanza na mtaji mdogo na zikakuletea faida kubwa. Hiyo ambayo inaitwa “biashara ndogo” ukiifanya kwa ubora wa hali ya juu na bidii ipo siku itakutoa.
Nilipokuwa narudi mazoezini asubuhi ya leo, nilijiuliza je ni biashara gani unaweza kuanza na mtaji mdogo (isiyozidi laki moja)? Nilijua zipo ila sikufikiria kama zinaweza kuleta faida nzuri tu utakapo zifanya kwa ubora.
Hivyo, nikaanza kuziandika kwenye simu na baada ya dakika chache nikajikuta nina orodha ya bishara zaidi ya ishirini unazoweza kuanza na mtaji mdogo na zenye faida kubwa ambazo nitaziandika hapa chini.
Kabla hatujaenda kwenye hiyo orodha ya hizo bishara za mtaji mdogo, ningependa kuweka sawa maana yangu ninaposema “zenye faida kubwa”.
Faida kubwa haimaanishi mamilioni ya fedha, bali ni kwamba faida utakayoipata kulingana na mtaji wako ni nzuri na usipokata tamaa zitakufikisha mbali.
Zingatia: Unapotaka kuanzisha biashara yoyote ile, ni vyema kufuatilia utaratibu na sheria za mahali ulipo. Tafadhali ilinde biashara yako kwa kufuata kanuni zote zilizowekwa na Serikali. Baada ya kulisawazisha hilo, twende kwenye hiyo orodha ya biashara za mtaji mdogo kama zifuatazo;
Unachoweza kufanya ni kwenda maofisi ya karibu yako na kuwaambia kwamba wakutafute wanapohitaji hicho chakula wakati wa mchana na wewe utawaletea.nUsisahau kuacha mawasiliano yako ili waweze kukutafuta. Wengi wao watapenda hiyo huduma kwasababu hawatohitaji kutoka tena kufata chakula.
Kuna watu wengi tu wanaendesha maisha yao kupitia biashara hizo. Kwanini wewe ushindwe? Na kama sio mtaalamu, hakuna tatizo. Chukua muda wako na kujifunza, ndani ya muda utaweza.
Uzuri wa biashara hii ni kuwa mtaji wake ni mdogo sana. Elfu kumi tu inatosha kuanzia na wapo waliofanya hivyo na wamekuza biashara zao kama vile Mak Juice au Zanana Juice Box.
Licha ya hivyo, bado kuna fursa ya kutengeneza kipato kupitia kilimo cha mbogamboga hata kama una mtaji mdogo. Anza na sehemu ndogo tu unayoweza kupata hata kama ni nyumbani.
Usafi wa mara kwa mara hasa hasa kwenye malisho yao utahitajika. Kwa vile mtaji ni mdogo, unaweza kuanza na kuku wa kienyeji, bata au hata njiwa. Japo kuwa wanachukuwa muda ila kuwa mvumilivu, faida utaiona
Tuangalie biashara 5 za mtaji mdogo usiozidi Tshs. 100,000 unazoweza kufanya na zenye faida kubwa. Mtaji mkubwa unaohitajika unapoanzisha biashara ni muda na wala sio pesa kama utakavyojifunza hapa.
Mimi binafsi siamini kama kuna biashara ndogo, ila najua kuna biashara unaweza kuanza na mtaji mdogo na zikakuletea faida kubwa. Hiyo ambayo inaitwa “biashara ndogo” ukiifanya kwa ubora wa hali ya juu na bidii ipo siku itakutoa.
Nilipokuwa narudi mazoezini asubuhi ya leo, nilijiuliza je ni biashara gani unaweza kuanza na mtaji mdogo (isiyozidi laki moja)? Nilijua zipo ila sikufikiria kama zinaweza kuleta faida nzuri tu utakapo zifanya kwa ubora.
Hivyo, nikaanza kuziandika kwenye simu na baada ya dakika chache nikajikuta nina orodha ya bishara zaidi ya ishirini unazoweza kuanza na mtaji mdogo na zenye faida kubwa ambazo nitaziandika hapa chini.
Kabla hatujaenda kwenye hiyo orodha ya hizo bishara za mtaji mdogo, ningependa kuweka sawa maana yangu ninaposema “zenye faida kubwa”.
Faida kubwa haimaanishi mamilioni ya fedha, bali ni kwamba faida utakayoipata kulingana na mtaji wako ni nzuri na usipokata tamaa zitakufikisha mbali.
Zingatia: Unapotaka kuanzisha biashara yoyote ile, ni vyema kufuatilia utaratibu na sheria za mahali ulipo. Tafadhali ilinde biashara yako kwa kufuata kanuni zote zilizowekwa na Serikali. Baada ya kulisawazisha hilo, twende kwenye hiyo orodha ya biashara za mtaji mdogo kama zifuatazo;
1. KUPIKA KWA ODA
Kama wewe ni mpishi mzuri au una mtu anayejua kupika, basi jitangaze kama unapokea oda za mapishi fulani. Tuchukulie unaweza kupika makande au wali nyama vizuri.Unachoweza kufanya ni kwenda maofisi ya karibu yako na kuwaambia kwamba wakutafute wanapohitaji hicho chakula wakati wa mchana na wewe utawaletea.nUsisahau kuacha mawasiliano yako ili waweze kukutafuta. Wengi wao watapenda hiyo huduma kwasababu hawatohitaji kutoka tena kufata chakula.
2. UREMBO (MAKEUP, KUSUKA & KUCHA)
Urembo ni gharama. Wanadada wanataka kupendeza wanapokwenda safari zao kama ni kazini ama shughulini. Uzuri ni kwamba hii ni biashara ya kila siku unayoweza kufanya. Baada ya kufanya utafiti wangu, nimebaini kwamba kufanya makeup, kutengeneza kucha na ususi wa nywele zinalipa vizuri tu.Kuna watu wengi tu wanaendesha maisha yao kupitia biashara hizo. Kwanini wewe ushindwe? Na kama sio mtaalamu, hakuna tatizo. Chukua muda wako na kujifunza, ndani ya muda utaweza.
3. KUUZA JUISI NA ICECREAM
Kujifunza kutengeneza juisi au icecream haitakuchukuwa muda mrefu. Ili kufanikiwa katika biashara hii, cha muhimu ni kujitofautisha. Muhimu zaidi unapofanya biashara ya kutengeneza juisi au icecream, ni kuweka mazingira yako safi na salama kwa wateja wako.Uzuri wa biashara hii ni kuwa mtaji wake ni mdogo sana. Elfu kumi tu inatosha kuanzia na wapo waliofanya hivyo na wamekuza biashara zao kama vile Mak Juice au Zanana Juice Box.
4. KILIMO CHA MBOGAMBOGA
Kilimo ni sehemu kubwa ya maisha ya watanzania na wale wa nchi nyingi za Afrika. Kila siku zikienda, kilimo huzidi kuwa ni biashara ya matajiri kwasababu shamba lina gharama kubwa.Licha ya hivyo, bado kuna fursa ya kutengeneza kipato kupitia kilimo cha mbogamboga hata kama una mtaji mdogo. Anza na sehemu ndogo tu unayoweza kupata hata kama ni nyumbani.
5. UFUGAJI WA NDEGE (KUKU, BATA, N.K)
Hii ni biashara ambayo ina faida kubwa lakini pia ina changamoto zake kama vile kuku wako kufa. Vifo vya mifugo huwaumiza sana wafugaji na mara nyingi husababishwa na mifugo hiyo kula uchafu. Hivyo, unapoingia kwenye ufugaji jitahidi uwe na mazingira safi na salama kwa mifugo yako.Usafi wa mara kwa mara hasa hasa kwenye malisho yao utahitajika. Kwa vile mtaji ni mdogo, unaweza kuanza na kuku wa kienyeji, bata au hata njiwa. Japo kuwa wanachukuwa muda ila kuwa mvumilivu, faida utaiona