Bi Tekka amfungulia Kesi ya madai Dc wa Korogwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bi Tekka amfungulia Kesi ya madai Dc wa Korogwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Sep 10, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HATIMAYE Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, mkoani Tanga, Bi. Najum Tekka, juzi ametimiza dhamira yake ya kumfungulia kesi Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Mrisho Gambo, kwa madai ya kumdharirisha na kudai fidia ya sh. milioni 96.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Bi. Tekka alisema kesi hiyo namba saba ya mwaka 2012, ameifungua katika Mahakama ya Wilaya ya Korogwe ili kulinda heshima yake kama mwanamke, "Sijamshtaki Bw. Gambo, kama Mkuu wa Wilaya, nimefanya hivi bila kujali cheo changu wala chake, hata samansi ya kufika mahakamani Septemba 10 mwaka huu, nimeshampa ili kujibu madai yanayomkabili," alisema Bi. Tekka.

  Alisema ameamua kuongeza kiwango cha fidia kutoka milioni 90 hadi 96, kutokana na uzito wa jambo hilo juu ya udharirishaji aliofanyiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo.

  Hivi karibuni, baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Manundu Mjini Korogwe, walidai kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya watendaji wa Serikali kushirikiana na wanasiasa ili kukwamisha jitihada mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Bw. Gambo.

  Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara sokoni hapo, Bw. Mussa Hussein, alisema hawakubaliani na njama zinazolenga kumdhoofisha ili ashindwe kutimiza wajibu wake ipasavyo.

  Wafanyabiashara hao walisema madai aliyotoa Bi. Tekka dhidi ya udharirishaji aliofanyiwa na Bw. Gambo hayana ukweli kwani hivyo kama Mkuu wa Wilaya atashtakiwa mahakamani, wapo tayari kumpa ushirikiano wakiamini madai hayo yamelenga kumchafua pamoja na kufifisha juhudi zake kiutendaji.

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Huyo Mrisho Gambo amelewa madaraka. Anadhani yupo kwenye malumbano ya uvccm Arusha! Natamani na akina mama wamsapoti mwenzao maana amewadhalilisha wote!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Ma DC wa facebook hao!utamtukanaje mtendaji wako matusi ya udhalilishaji namna hiyo?au wanalewa madaraka na kujiona kama bila yeye mambo hataenda!!!
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Haya mama songa mbele kabisa maana hiv vyeo vya kupewa kishikaji vinafanya hawa viongozi wa kisiasa kuropoka tu. Mpe dawa yake!!! Je ulfanikiwa kurekodi kidogo mambo?
   
 5. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Vita vya panzi furaha kwa.......
   
 6. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huyu dogo atapata wapi hiyo 96mil?
   
 7. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  Bi Tekka, well done, this man is hopeless! Ni PM nikupe mawazo how to crucify this blood hopeless power monger so called DC!
   
 8. b

  braza makaptula Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KOMBAJR usinichekeshe! 96 mil zinapatikana kilaini sana kwa Gambo kwani ni mfuasi wa David cameroon huyo, tumpr pole tu jinsi atakavyolipa, Cameroon akiwa busy kuna waarabu anawafaham huyo
   
 9. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu unayoyasema unamahanisha?
   
 10. i

  iseesa JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanasheria tusaidieni hapa. Huyu Bibi Sheria anazijua sheria? Hii Kesi itakuwa ya Madai au "Defamation"?
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  kwa kuwa suala lipo mahakamani tayari basi tuipe nafasi mahakama ifane kazi yake pasi na kuingilia na kitu kingine chochote.
   
 12. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Udhalilishaji huu unatakiwa uchukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa hawa MaDC wasiokuwa na hekima,Busala na maadili ya uongozi, eti Degree ya CHUPI hivi hata hicho chuo alichosoma huyo binti wakiamua kumshitaki si watakuwa sahihi, kwamba na wenyewe wana award chupi kwa watahiniwa wao loo aibu.
   
 13. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,859
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kwa uelewa wa Haraka Huyo DC alikwenda Kuchukua Rushwa kwa Hao wafanyabiashara ambao kwa haraka naona walikuwa wanafanya Biashara sehemu Isiyoruhusiwa!! Sasa mwanasheria alishawafungulia kesi wahamishiwe sehemu stahiki!! Sasa DC analeta siasa kwenye Utendaji!! Kwani ni Lini Mwanasheria wa Wilaya aka-report kwa DC??
  Ila kwa udhalilishaji wa huyo DC Umenifanye Niwaone Wanawake wengi Mbele Yangu Kama wana degree aliyosema Gumbo!! Hivyo ni Bora akinamama wote mkajiunga na kuanzisha umoja wa kutafuta Haki katika huu udhalilishaji!!
   
 14. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Mkuu, are you serious ama nyie ni watani wa jadi?
   
 15. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Hii kesi itakuwa ni DEFAMATION CASE na kesi za aina hii zinatakiwa zifunguliwe MAHAKAMA KUU TU na si MAHAKAMA ZA CHINI YA HAPO.
   
 16. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,298
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Hii ni ishara tu kwamba mwisho wa CCM umefika, how come viongozi mtukanane hadharani, kwanini asingemwita ofisini na kumpa warning? Wamechanganyikiwa hawa. Wote ni hao hao
   
 17. j

  jingojames JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 882
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 80
  huyu gambo alishazoea kutukanana matusi ya nguoni na wakina millya,uvccm kule arusha ndiyo maana alimrushia matusi mwanasheria huyu kuwa anadegree ya CHUPI kwa wasomi unapomwambia mwanaMKE anadegreee ya CHUPI maana yake ni kilaza ambaye hakuwa na uwezo wowote wa kusoma na kuhitimu shahada isipokuwa alifanikiwa kuwaonga URODA(NGONO-ALIVULIWA CHUPI) na walimu wake na kisha kusaidiwa kuhitimu!

  ni TUSI BAYA na UDHALILISHAJI mkubwa sana KUMTUKANA MWANAMKE MSOMI kama mwanasheria na hT hasikuchukulie hatua!
   
 18. mka

  mka JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu 'Defamation' nazo ni kesi za madai.
   
 19. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Mh.. Cijaicikia hii Wakuu.. Kwa anaejua naomba anijuze kilitokea nini kati ya huyo dc na mwanasheria huyo mwanasheria wa Halmashauri..
   
 20. N

  NKANOELI JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  BASI NDO TUSEME NA YEYE VYETI VYAKE ALIVYONAVYO NI VYA ******.MAANAKE SIDHANI KAMA ANA DECREE/DIPLOMA HUYU,MSHENZI SANA.OLE WENU SHERIA ISIPOFUATA HAKI,SS NDO WAPIGA KURA.PUMBAFFFFFFFFFFF SANA GAMBO:sleepy:ZIRO MKUBWA WE.
   
Loading...