Napenda (sana, sana) nyimbo za Shakila:
- Macho yanacheka moyo unalia.
- Kifo cha mahaba
Macho yanacheka, Moyo unalia,
Nikimkumbuka wangu maridhia,
Chozi hunitoka, kwa zake tabia.
Nenda nateseka, nalia na njia,
Siku zitafika, kukugeukia,
Waja hangaika, ulie na njia.
Uache dhihaka, mpenzi sikia,
Moyo waniwaka, kweli nakwambia,
Wanipa mashaka, kwa zako tabia.