Bi kizee anaswa akiwanga kwenye wodi ya watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bi kizee anaswa akiwanga kwenye wodi ya watoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Dec 10, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280

  *Adai alimpelekea mjukuu dawa ya degedege
  *Aitaja kuwa ulikuwa ni mkojo wake
  KATIKA hali isiyo ya kawaida, bibi kizee mmoja mkazi wa Mtoni Mtongani, Temeke jijini Dar es salaam ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja amebambwa akiwanga katika Hospitali ya Manispaa ya Temeke.

  Bibi huyo alibambwa saa 7 usiku wa kuamkia jana akiwanga katika wodi namba mbili, wodi ambalo ni maalumu kwa ajili ya kulaza watoto akiwa amejifunga kipande cha khanga kufunika sehemu zake za siri.

  Ilidaiwa kikongwe huyo mwenye macho mekundu, alikwenda hospitalini hapo kumwangiai mjukuu wake, mtoto wa mwanawe wa kike aliyekuwa amelazwa katika wodi hiyo ambaye alifariki muda mfupi baada ya bibi huyo kumnywesha na kumpakaa dawa ambayo ilidaiwa kusababisha kifo cha mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minane.

  Wakizungumza na Dar Leo hospitalini hapo, mashuhuda wa tukio hilo ambao ni wazazi waliokuwa wamelazwa na watoto wao katika wodi hiyo walisema ghafla usiku huo, wakiwa wamelala walishtukia mlango wa wodi hiyo uliokuwa umefungwa umefunguliwa huku watu wane¬ówanaume watatu na mwanamke mmoja¬ówaliovalia mavazi yaliyoficha tu sehemu zao za siri, wakilandalanda ndani ya wodi hiyo wakiwanga.

  Walisema wanga hao walimchomoa mtoto huyo katika mashine ya kumsaidia kupumua aliyokuwa amewekewa na ghafla wanga watatu wa kiume walitoweka na kubakia bibi huyo ambaye alionekana akimnywesha na kumpakaa mtoto huyo vitu ambavyo vilidaiwa ilikuwa dawa ya ushirikina.

  Baada ya kumnywesha na kumpakaa dawa hiyo, walisema mtoto huyo alifariki na bibi huyo alishindwa kuondoka na kuanza kuzunguka ndani ya wodi hiyo huku akiwa ameinama mithili ya mtu anayeokota kitu.

  Walisema kwa kuona hivyo, wanawake wawili walishirikiana na nesi aliyekuwa zamu katika wodi hiyo, Rehema Mkula, kukemea hali na vitendo vya kishirikina alivyokuwa akiendelea kuvifanya bibi huyo katika wodi hiyo wakiamru ashindwe na alegee kwa jina la Yesu.

  Wakati hayo yakiendelea, mama wa mtoto aliyefariki alikuwa akilia kwa uchungu akimshutumu mama yake kumfanyia tendo hilo la kumuua mwanaye kishirikina tukio ambalo alisema ni la pili kwani, mwanawe wa kwanza naye alikufa katika mazingira ya utata kama huo na mama yake huyo kuhusishwa na kifo chake.

  Walisema mambo yalipozidi kuwa makubwa, bibi huyo akiwa katika hali ya kuduwaa hasa baada ya watumishi wa Mungu kumchoma kwa injili ya Yesu, waliitwa walinzi waliomchukua na kumhoji kwa saa kadhaa kabla ya mkwe wa bibi huyo pamoja na kukiri kutendewa na bibi huyo tukio la namna hiyo mara mbili kuwasihi walinzi hao wamuache aende zake.

  Akizungumza hospitalini hapo, mmoja wa walinzi wa kampuni ya ulinzi ya SSG aliyejitambulisha kwa jina moja la Ismail ambaye alimkamata na kumhoji bibi huyo alisema bibi huyo alidai alikuja kumpa mjukuu wake dawa ya degedege baada ya kupigiwa simu na mwanawe kuwa mtoto amezidiwa, na kwamba dawa aliyomnywesha ulikuwa mkojo wake ambao aliamini utasaidia kumtibu mjukuu wake ugonjwa wa degedege.

  Hata hivyo, gazeti hili limefanya jitihada za kuwasiliana na uongozi wa Hospitali ya Temeke jitihada zimekwama.

  Gazeti hili lilipata fursa ya kuongea na daktari mmoja ambaye hata hivyo alikana kuwa si msemaji wa hospitalia hiyo na kusema Serikali haina ushirikiano na mambo ya kishirikina hivyo hawezi kulizungumzia suala hilo.
   
 2. E

  Edo JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mkuu ipo gazeti gani hili?
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,486
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  itakuwa gazeti la hospital ya temeke
   
 4. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hawa wazee ni hazina ya taifa letu, ila wakati mwingine ni noma ile mbaya
   
 5. ghumpi

  ghumpi Senior Member

  #5
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mbaya sana. Mungu apishe mbali haya mambo.
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  wananichosha sana watu wa aina hii.......
   
Loading...