Bi. Annar Cassam: Moja kati ya personal assistant (PA) wa the late Nyerere

Bi. Annar Cassam alikua mwanafunzi wa London School of Economics (LSE) miaka ya 60 ndipo alimsikia na kumuona Mwl. Nyerere kwa mara ya kwanza, kipindi ambacho Nyerere alipenda kutembelea wanafunzi alipokua anakwenda London kwenye misafara yake.

Akiwa Geneva - Switzerland miaka ya 70 Bi. Annar aliombwa kurudi nyumbani na kufanya kazi mambo ya nje wakati ambao Dar es salaam ilikua makao makuu ya African Liberation Comitee (ALC), chombo cha kupigania uhuru Kusini mwa Africa kwa wakati huo ilikua ni kipaumbele kwa Mwl. Nyerere na sera ya mambo ya nje.

Kutokana na uwezo wake akaanza kufanya kazi Ikulu na Mwl. Nyerere kama msaidizi wake binafsi. Alikua akitumika sana kama mtafsiri wa Kifaransa wa Mwalimu na alikua karibu sana na Mwalimu alipokua akikutana na viongozi wanaozungumza kifaransa kama mtafsiri wake.

Baada ya kustaafu kwa Mwalimu mwaka 1985 Bi. Annal Cassam alihamia Geneva ambapo alifanya kazi umoja wa mataifa. Akiwa uko alichapisha makala na vitabu mbalimbali juu ya maisha ya Mwalimu ikiwemo President Nyerere on Liberation, Nyerere on Nyerere, Africa's liberation: The legacy of Nyerere kitabu alicho andika na Chambi Chachange.

Bi. Annar Cassam alifariki mwaka 2020 uko Geneva Switzerland anakumbukwa kama kati ya waTanzania wenye asili ya Asia (India) wenye machango katika harakati za kujenga taifa baada uhuru, pia kwa mchango wake katika utumishi wa umma, harakati za kutafuta uhuru Africa kusini na mchango wake katika kueleza historia ya Mwalimu, Tanzania na Africa kwa ujumla.

Link za makala zake:

President Nyerere on liberation:


Nyerere on Nyerere


View attachment 1793939View attachment 1793940View attachment 1793941View attachment 1793944View attachment 1793942View attachment 1793943

View attachment 1793923

View attachment 1793924

View attachment 1793926

View attachment 1793927

View attachment 1793928

View attachment 1793934

View attachment 1793935

View attachment 1793936
Wa kwanza alikuwa mama Joan Wickens ambaye alimsaidia kutengeneza katiba ya Tanganyika, huyu alikuwa mwingereza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom