Betting sio biashara halali

Nenda thailand uone watu wakibet kwa mchezo wa kuku kupigana na vibosile wako wanabet tembea ujionee.
 
Mtoa mada leo kazi unayo, sijui kama utapata mtu wa kukusapoti, watu wameshakua addicted na huo uchafu

Sitafuti kusapotiwa, ila naeleza ukweli kama ulivyo.
Siku wakiamka usingizini, watayaelewa haya.
 
Katika huyo mmoja aliyepata kiasi hicho, ni wangapi ambao wameliwa?
Maana huwa mnachukua hadithi ya mtu mmoja na kuacha wengi ambao wanaliwa.
 
Majibu yako ni tofauti na maswali niliyouliza, na hata maelezo niliyotoa.
Sikuomba nifafanuliwe kuhusu betting,
Bali jibu swali la msingi; NI THAMANI IPI INATENGENEZWA KWENYE BETTING?
 
Unaingilia faragha za watu hizi ni starehe zetu jamani. Mimi si mpenzi wa beer wala wanawake lakini ni mpenzi wa gambling. Matajiri wote unaowajua wamewekeza kwenye bet na wana bet.
Katika orodha ya matajiri wakubwa duniani, africa na hata tanzania, hebu nitajie waliofika pale kwa kutumia betting, ili tuwatumie kama mfano kuwashawishi watoto wetu wakazane na kubet zaidi.
 
Katika orodha ya matajiri wakubwa duniani, africa na hata tanzania, hebu nitajie waliofika pale kwa kutumia betting, ili tuwatumie kama mfano kuwashawishi watoto wetu wakazane na kubet zaidi.
Sijasema walipata utajiri kwa kubet bali huo ni mchezo wao pendwa na wao ndyo walioanzisha na wanahisa na kuidhamini hyo michezo nenda las vegas marekani ujionee lile ni jiji la michezo ya kubashiri. Maana ya mchezo ni ule ama uliwe au ushinde au ushindwe.
 
Utakuwa umeliwa sana kwenye kubet,acha kudanganya uma kijana
 
Kuna mateja ya unga na mateja ya betting, kwa bahati mbaya wanatetea addiction, ila ipo siku mtajua mnachokifanya ni upuuzi tu.
 
Juzi UEFA barca vs juve jamaa odds ya droo ilikuwa na point 20 jamaa kajitoa fahamu kaweka 50000,sisi wajanja oohh barca anashinda hii mechi tena handicap!!!maanina zake jamaa kalamba 1mill ,,,high risk high return and vice versa is true!!!
 
Kubet ni jambo la hatari sana. Kwanza ni 'habit forming' yaani ukishazoea kubet huwezi kuacha. Utaiba pesa au uuze vitu vya nyumbani kwako ili mradi upate pesa za kubet. Unazoea kama vile mtu anavyokuwa mtumwa wa kuangalia picha chafu (pornography). Pili kama Makirita alivyoandika, kwenye nchi za wenzetu betting inafanyika kwenye maeneo maalum tu (yaani kwenye casino tu). Huko hakuna mtoto anayeruhusiwa. Hapa kwetu hata watoto wa shule wanabet. Wanajengewa mazoea mabaya sana. Tatu wanaobet wanadhani wanaweza kupata pesa kirahisi. Jiulize: Kama kila mtu anayebet anapata pesa kama alivyobet je, huyo mwenye kampuni inapolipa watu inapata wapi pesa za kulipa watu waliobet wakapata? Lazima ninyi mnaobet mjue kwamba wenye hayo makampuni wanapata mabilioni wakati wewe ukibet elfu 20 labda unapata laki tano ukibahatisha. Kama wewe unabet hebu andika mzigo unaoweka kwa miezi mitatu ulinganishe na kiasi unachoshinda kwa wakati huo. Utaona wazi kwamba utakuwa umeshakula hasara kubwa. Nne na mbaya zaidi ni kwamba unajijengea mazingira ya kuzoea kubahatisha mambo yako badala ya kuyapangilia kiakili
 
Katika huyo mmoja aliyepata kiasi hicho, ni wangapi ambao wameliwa?
Maana huwa mnachukua hadithi ya mtu mmoja na kuacha wengi ambao wanaliwa.
Sasa mkuu kama 50cent anayeingiza dola laki 2 kwa kila SAA kutokana na Muziki pamoja na Investments zake anabet sembuse sisi ambao hatuna uwezo wa kuingiza hata Milioni 2 kwa siku...???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…