So far away
Member
- Jan 7, 2017
- 58
- 121
Watu wengi wakisikia neno bet, moja kwa moja wanahuisha na mpira wa miguu, ni kweli wapo sawa ila betting siyo kwenye mpira wa miguu tu hata kwenye michezo kama cricket, basketball, ngumi na michezo mingine. Embu tungalie kwa upande wa mpira wa miguu ambo unaongoza kwakua na mashibiki wengi duniani. Kwa hapa Tanzania kuna makampuni mengi yanayo jihusisha na mechezo ya kubahatisha/bahati nasibuu mfano wa makampuni hayo ni m-bet a meridian ambayo yanaongoza kuwa na wateja wengi.Tuangangalie kwa uande wa m-bet. Ukifuata hatua hizi utaweza kuwa unashinda katika ubashiri utakaofanya
1. usiweke mechi nyingi kwa mkeka mmoja/ticket. Hii ni kwasababu unapoweka mechi nyingi katika mkeka mmoja unapunguza uwezekano wa wewe kushinda. Japo kuwa wengi wanawaza kupata hela nyingi lakini wanasahau kuangalia uwezekano wa kushinda. Ni kweli kwamba ukiweka mechi nyingi ndio hela inaongezeka ila uwezekano wakushinda unapungua, ndiyo maana wenye makampuni hawaruhusu kubeti/kutandika mkeka wa mechi moja .angallia mfano hapo chini
2. Zijue timu unazozibetia/ ambazo unazitabiria : kujua timu kabla ya kubeti ni jambo muhimu sana kwa sababu kunatimu ni mahasimu sana katika ligi fulani. Kwa mfano ligi kuu vodacom wakicheza simba na yanga, hata kama simba akiwa anashika nafasi za mwishoni katika ligi hatakubali kufungwa kirahisi na yanga kwa hiyo mechi itakua naupinzani mkali. Mara nyingi zikikutana timu kama hizi matokeo huishia kuwa droo/draw au utofauti mdogo wa magoli kwa mfano mechi inaweza kuisha 0-0, 1-1, 2-2, na sare nyinine au 1-0, 0-1, 2-1, 3-2. kwahiyo kwa timu kama hizi usibeti kwamba timu fulani itashinda kwa tofauti ya magoli mawili au zaidi. Pia kingine atika kuzijua timu jaribu kuangalia kama kuna timu ni kibonde wa mwingine. Kwa mfano asernal ni mteja wa man united mara kwa mara, kwahiyo jaribu kuangalia nani anamfunga mwenzake mara kwa mara kisha mpe.
3.usibetie timu kwa sababu ya ushabiki: hiki ni kitu cha kuzingatia kwani wengi wwamekua wakibet kwa sababu tu ya mapenzi ya katika timu fulani. Ushauri ni bora usibetie timu unayoipenda kama uwezi kazuia hisia zako, kwani hisia zinamzuia mtu kuichambua timu anoyo ishabikia
4.Angalia goal differences/ tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa: ni vizuri kuangalia tofauti ya magoli kwa zile timu ambazo unataka kuzibetia na hii ni nzuri hususani kwa wale ambao watakua wanabeti kama timu zote zitafunga. Kwa mfano kama timu inamagoli mengi ya kufunga kuliko ya kufungwa ni wazi kwamba timu hii haifungwi mara kwa mara kwa hiyo ikikikutana/kucheza na timu ambayo ina magoli mengi sana ya kufugwa kuliko ya kufunga, hii inaonyesha kuwa hii timu itafungwa bila yenyewe kufunga kwahiyo kama uliweka both team will score “yes” huo mkeka utakua umechanika.
NB: hii haimanishi kwamba itakua hivyo kwa mechi zote ila ni kwamba uwezekano mkubwa/ possibility ipo hivyo
5. Usibet mechi zaidi ya tatu: Na maanisha kuwa the more teams the greatest possibility to lose but the less teams the greatest possibility to win. Watu wengi wanakosea. Huandaa mkeka wenye idadi kubwa ya mechi matharani mechi 8; 10; 12; 15 wengine hadi 20 na huweka sh. 500 au sh.100 na wakitegemea kula mamilioni ya pesa. Ndugu zangu hizo ni ndoto za mchana. Bora hiyo sh.500 au hiyo buku ungenunua vocha. Haiwezekani na mara nyingi watu huliwa kila siku. Wengine huchagua list kubwa ya big team kama barca; real madrid; bayern; psg; juventus ambazo zinapewa possibility kubwa ya kushinda. Lakini team hizi hupewa odds (point) ndogo sana kama 1.11; 1.03; 1.20. Cha ajabu sasa ni kwamba kila week end au week lazima big team ifungwe. Utashangaa barca vs betis. Barca kapigwa au katoa droo. Au psg vs lorient matokeo bi sale au kapigwa psg. Mala nyingi timu kubwa huangusha na kujikuta mkeka umechanika!
A good betters mara zote huwa abeti timu yenye uhakika wa kushinda. Pia huangalia timu tatu au mbili zenye odds 2 na kadhalika halafu anatupia mzigo mkubwa. Kwa mfano: 1. Bolton 2.14 vs luton 4.21 matokeo Bolton win. 2, Southend 2.33 vs Morecambe 2.76 matokeo Southend win na tatu Genk 3.22 vs Wz 3.88 matokeo Genk win. Kwa hiyo hapa utakuwa na odds hizi: 2.14×2.33×2.22= 11.069364 sasa weka dau la elfu kumi. Utavuna pesa hizi. 11.069364 × 10000= 110693.64 toa kodi asilimia 18 utabaki na 90,768.7848. Kanuni nzuri hapa ni chagua timu zisizo zidi 3 na zenye odds zaid ya 8 na weka mzigo wa maana. Nakuhakikishia namna hii hurokuwa mtu wa kulia lia.
6. Beti over under:
Over maana yake jumla ya magoli yalofungwa katika mechi hiyo yawe 3 au zaidi. Kwa mfano: 1-2 ; 0-3; 2-1 ; 3-0 ; 2-2; 4-1 nk. Lakini Under maana yake jumla ya magoli iwe na isizidi 2. Yaani 0-0; 1-0 ; 1-0; 1-1; 2-0; 0-2; 0-1. Kanuni hii ya over under hutokea sana pale timu zenye upinzani mkubwa zinapokutana magoli huwa either kidogo au mengi. Kwa mfano. Real madrid vs Bayern: mechi hii kwa vyovyote magili huwa under yaani 0-2. Hali kadhalika mechi kama juventus vs Lazio; Celtic vs Rangers; Simba vs Yanga ;Liverpool vs Tottenham; hali kadhalika Liver plate vs Corinthians yaani strong team vs strong team magoli huwa machache either Droo ya 0-0 au 1-0; 1-1 saana ni 2-0. Lakini mechi kama Barcelona vs Malaga; Simba vs Panone fc; Atletico de Madrid vs Osassuna yaani big team vs weak team matokeo huwa na magoli mengi.
7. Bet GG. ( both teams to score)
Kanuni hii ni nzuri na ni maarufu sana kwa mabetters. Kwani mara nyingi ndo huleta matokeo mwisho wa mechi. Mara nyingi kama timu zina kiwango sawiya cha uchezaji matokeo haya hutokea. Kwa mfano: Swansea vs Crystal Palace; Olimpio vs union ; Torino vs Roma; Celtic vs Ranger; Varcelona vs Real Madrid; Arsenal vs Chelsea; Simba vs Yanga; Bandari vs Gor Mahia; Boca junior vs Liver plate; Bayern vs Brussia Dortumond n.k. kwa maana nyingine Strong team vs Strong team na Weak team vs weak team.
8. Bet win from the first half. (Yaani ongoza mwanzo mwisho)
Hii inamanisha kuwa timu huyo unayo taka ishinde mwanzo mwisho maana yake ianze kuongoa toka kipindi cha kwanza hadi dk 90. Yaani 1-1 au 2-2.
1-1 maana take home team (teamu ya nyumbani) iongoze toka kipindi cha kwanza. Kama hivi. Besiktas vs Adanaspor matokeo awe ivi: " First half : Besiktas 2 Adanaspor 1. Second half matokeo yoyote yale ila tu Adanaspor asiongoze kipindi cha pili na mechi iishe Besiktas akiwa mshini. Kanuni hii hutokea mara nyingi pale Strong/big team inapocheza na small/weak team.
2-2 hii inamaanisha kuwa away team iongoze mwanzo mwisho kama ilivo kuwa kwa home team yaani 1-1. Kwa mfano inverness vs Celtic.kwa hiyo celtic aongoze toka kipindi cha kwanza. Kanuni hii 2-2 hutokea endapo weak/ small team inapocheza na strong/ big team.
9. BET DOUBLE WIN ( WIN ALL HALVES)
Hapa tuna kanuni mbili HW2 au AW2. HW2 maana yake ni kwamba home team ( timu ya nyumbani iongoze /ishinde vipindi vyote viwili.) Kwa mfano Real Madrid vs Leganes na matokeo awe hivi: First half result: Real Madrid 1 Leganes 0 na second half result iwe Real Madrid 2 Leganes 1. Na mwisho wa siku matokeo yawe Real madrid 3 Leganes 1. Hii kanuni ni maarufu kama timu kubwa iko nyumbani na inacheza na kibonde!
Aw2. Maana yake ni kwamba timu ya ugenini ishinde/iongoze vipindi vyote viwili. Kwa mfano Crotone fc vs Juventus. Na matokeo first half yawe: Crotone 1 na Juventus 2. Na second half result Crotone 0 na Juventus 3. Na mwisho wa siku mechi iishe kwa matokeo : Crotone 1 na Juventus 5. Kanuni hii hutokea sana kama timu Kibonde iko nyumbani na ina cheza na timu kubwa . Nb. Mfumo huu una odds nyingi sana.
Note:
.Cheza kwa kiasi mchezo huu. Usiwe na tamaa kwamba unaweza pata pesa nyingi kwa mara moja kwahiyo ukacheza hovyo bila mpangilio, hutaumia. Jaribu kuweka mikakati na mipangilio juu ya uchezaji wako, hakika hutajuta. Cheza mechi chache kwa siku unazoamini zinaweza kukupatia ushindi sio lazima ubashiri mechi nyingi kwa mkupuo. Hii itakusaidia wewe kukupa ushindi mara nyingi
.Usibashiri kwa mapenzi ama ushabiki, eti kwa kuwa mimi ni mshabiki wa liverpool Fc ama chelsea basi ndo nakuwa naitabiria ushindi kila mara, angalia uwezo wa timu yako dhidi ya timu pinzani kama inaweza shinda na hii itakuwa rahisi endapo utakuwa mfuatiliaji mzuri pia wa ligi ama mchezo unaobashiri.
.Epuka kubet ligi moja tu.
Kuna watu hawajui ligi nyingune mbali na ligi ya uingereza. Jitahidi ujue ligi nyingine kama Laliga; Bundasliga; france ligue 1; Italy serie 1; england championship; england ligue 1; england ligue 2; Argentina ligue; Mexico ligue, brszilian ligue; Chile ligue; scotland league; belgium ligue; Usa league.nk
UBARIKIWE.