Betri Inayojaa ndani ya Sekunde 60!

Betri Inayojaa ndani ya Sekunde 60!

no nm

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
212
Reaction score
32
Watafiti kutoka Chuo cha Stanford nchini Marekani wamefanikiwa kutengeneza betri linaloweza kuchajiwa na kujaa ndani ya dakika moja. Pia teknolojia ya betri hilo ni salama zaidi kuzidi teknolojia ya betri zilizopo sokoni kwa sasa. Mfano hata kama betri hiyo ikitobolewa bado inaweza fanya kazi kwa muda mrefu tuu bila madhara wakati betri zilizopo kwa sasa kama zikiharibiwa wakati zinafanya kazi zinaweza ata kulipuka na kuleta madhara kwa mtumiaji au kifaa husika. Pia betri hilo litadumu muda mrefu zaidi wakati
linatumika zaidi ya teknolojia ya mabetri ya
sasa ambayo baada ya kuchaji mara kwa
mara yanawahi kuishiwa nguvu ya kuhifadhi
chaji muda mrefu zaidi. na habari njema ni kuwa betri hili litaweza kukunjwa bila kuathiri utendaji wake. Hakuna Kuvunjika..!
 
Nimeisoma thread yako mpaka mwisho ili nijue ni betri ya kitu gani lakini hola, waweza nijulisha ni betri kwa ajili ya kifaa gani ??????????????
 
Nimeisoma thread yako mpaka mwisho ili nijue ni betri ya kitu gani lakini hola, waweza nijulisha ni betri kwa ajili ya kifaa gani ??????????????

Simu, tablet, & device nyingine yoyote,
 
ndo kwaanza technology imegundulika. so be patient nimeziona saa hizi bbc.
 
Akizingua tuh simu haina chaja, unasema poa basi nitakupigia baada ya dakika mbili.....no kisingizio
 
Na m nimeiona bbc ikopoa sana hyo,ila walete mapema kabla ile sheria haijaanza kufanyA kazi,
 
Hii itakua poa sana kwa sisi tunaopenda kushinda online cku nzima..
 
Naomba msaada wa link ya kudownload driver za printer >> photosmart All-in-one B010b>>
 
Tatizo hua ni kuoptimize ili product iwe fit for normal consumers, kuna products nyingi zinaishia behind doors hazifikii watu sababu ya vitu kama cost of manufacturing... Hii ni ya sekunde 60, mwaka juzi mdada wa high school alitengeneza inayochaji kwa 30seconds, Israel napo CES mwaka huu walionyesha ya kwao nayo inajaa kwa 30s, They take years to get to consumers, watu tunachoka kusubiri...
 
Back
Top Bottom