• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Beter late than never!!

K

Kamuli

New Member
Joined
Sep 2, 2011
Messages
2
Points
20
K

Kamuli

New Member
Joined Sep 2, 2011
2 20
Nguzo kuu ya taifa lolote duniani ni watu, na wao ndio wanaopaswa kutoa maamuzi ya mwisho kuhusiana na maswala yanayohusu taifa lao. ni taratibu nzuri kwa watu kuchagua wawakilishi wanaoamini watapaza sauti kwa niaba yao na kutoa maamuzi yatakayonufaisha taifa kiujumla.
Bunge ndio muhimili wa serikali unaocheza nafasi hii. Na inafaa waheshimiwa wa mjengoni wasisahau kuwa kilichowapeleka pale bungeni si ushabiki wa vyama, umaarufu au maslahi binafsi bali kutumikia wananchi waliowatuma. Kwa sababu za kiubinadamu ni muhimu kwa wananchi kufuatilia mara kwa mara maamuzi wabunge wanayoyachukua bungeni kwa niaba yao. Itakua vizuri zaidi kama wabunge nao watatambua kua kuna macho na masikio ya wapiga kura wao yanayofuatilia kila nyendo zao hasa katika maslahi ya taifa.
Utaratibu wa bungeni wa kupitisha au kutengua miswaada kwa spika kuhoji na wabunge wote kujibu kwa pamoja haunisaidii mimi kama mwananchi mpiga kura kujua kama mbunge niliyemchagua katoa maamuzi gani na hivyo kuona kama kweli maamuzi anayoyachukua bungeni ni kwa manufaa yangu au la! Mfano: ingekua rahisi kumhoji mbunge wangu juu ya sheria mpya ya mafao ya uzeeni kua ililenga kumnufaisha nani kama ningejua mbunge anaeniwakilisha aliiunga mkono kwa kusema ndio.
Ili kuwapo demokrasia ya kweli kwa mtazamo wa kitaifa inafaa utaratibu huu wa kupiga kura bungeni ubadilike. Nimeshuhudia mambo mengi yenye mtazamo wa kumsaidia mwananchi wa kawaida yakiishia kapuni kwa utaratibu huu. utaratibu huu unaendekeza uchama na unanufaisha maslahi ya waheshimiwa zaidi. uwekwe basi utaratibu ambao mwananchi wa kawaida atajua maamuzi ya mwakilishi wake bungeni na hivyo kuweza kupima kama kweli anastahili kuvikwa kofia ya "Mtetezi wa wanyonge" au la na hivyo kuwa na maamuzi sahihi atakavyokuja kuomba kura kwa mara nyingine. Just a simple parliamentary voting software inaweza kusaidia na ninauhakika wapo wasomi hata Tanzania hii wenye uwezo wa kudesign. Its about time serikali ikaonesha transparency basi angalau Bungeni. WATU WANAPASWA KUFAHAMU!!!
 

Forum statistics

Threads 1,402,831
Members 530,989
Posts 34,406,358
Top