Best man na Matron wanakuwa vilevile mashahidi katika hiyo ndoa na wanatakiwa kuweka sahihi zao katika vyeti vya maharusi kama mashahidi. Best man, anatakiwa awe mtu wa karibu sana wa bwana harusi na Matron anatakiwa awe mtu wa kariu sana na bibi harusi.
Hawa wanakuwa washauri wa maharusi hawa wapya katika maisha yao ya ndoa, na kama kukitokea shida yoyote kuhusu ndoa, hawa ndio wa kwanza ambao maharusi wanatakiwa kuwaona.
Kutokana na ukaribu wao kwa maharusi, matron na bestman wtakuwa wamekuwa wamejuana kwani ni watu ambao kwa muda mrefu wamekuwa katika maisha ya maharusi, au hata kushuhudia mwanzo wa uchumba.
kwani ni nini maana halisi ya neno matron?
hao ni watu tu wa kupendezesha harusiHivi kazi ya "Best Man" na "Matron" katika harusi ni nini hasa?.
Katika miaka ya hivi karibuni kameibuka ka mtindo kwa wasimamizi wa harusi ("Best Man" na "Matron") kutumika tu siku ya shughuli kama mapambo na pengine huwa ni seti mbili tofauti, kama kandambili za mguu moja. Utakuta Bwana kivyake na bibi kinyake (bestman hamfahamu bibi harusi wala matron hajui chochote kuhusu Bwana harusi).
Katika harusi nyingine utakuta maharusi wanahangaika kutafuta watu wa "kumechi" nao kwa maumbo, mwonekano na vipimo na pengine hata kwenda kumkodisha "matron au bestman" wasiemfahamu ilimradi tu wapate kupendeza siku ya harusi....na siku ikiwadia unakuta Bestman au Matron kazi yake ni kufuta jasho tu la bwana au bibi harusi.
Hivi hakuna Hadidu za Rejea (Terms of Reference) za "Best Man" na "Matron"???
bestman na matron wamepoteza maana kwenye ndoa za kisasa.... hawana ile hadhi kama inavyoelekezwa kwenye vitabu vya dini...
tume-commercialize ndoa sasa imekua tabu tupu