Bernard Membe hahusiki na MODSPAN

Bernard Membe hahusiki na MODSPAN

Kwani Membe ni nani?
Anatokea chama gani?
Yuko tayari kusema ukweli kuusu maoni ya tume ya warioba?
Kama anasimama na msimamo wa Chama chake basi wote ni walewale ukoo wa panya. Hakuna asiyetoboa gunia la mahindi anapoingia kwenye stoo.
 
Ha ha hili suala lipo wazi sana. Memorundum ama articles za kampuni toka lini zikaandika ushemeji?? Ukweli ni kwamba jamaa amempigia pande shemeji kupata tenda.

Weka ushahidi wa kuhalalisha uongo wako
 
Duh, mbona nguvu ya kujibu ni kubwa sana kuliko habari yenyewe?
 
Membe haitaji Kuwa ktk tenda board, inajulikana nchi yetu ki-memo kinamaliza yote. Membe ni moja ya jamii ya panya. Hatuitaji ushahidi kwani ndivyo wanavyofanya wakijua hakuna material evidence ya kuwatia hatiani, but just common sense he did I it.
 
Jana katika mitandao kuna habari za uongo ambazo hazivumiliki zilienea kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ndugu Bernard Kamillius Membe anahusika na suala la ujenzi wa gati la Mbamba Bay kujengwa chini ya kiwango kulikofanywa na kampuni ya kandarasi iitwayo MODSPAN ambayo inahusishwa na shemeji yake.

Ukweli juu ya suala hili ni kwamba hakuna kitu kama hicho kinachomtia hatiani ndugu Bernard Kamillius Membe kwasababu ya mambo yafuatayo;

Moja,yeye sio mjumbe wa bodi ya tenda ambayo iliipa kampuni hiyo ya kandarasi kujenga gati husika.

Pili,walioeneza habari hii wameshindwa kutoa ushahidi usio na mashaka kwamba kweli mmiliki wa kampuni hii ya MODSPAN ni shemeji yake na ndugu Bernard Kamillius Membe iwe kwa kutumia hati ya kiapo au la!

Tatu,waliozusha jambo hili wameshindwa kuainisha kwa ushahidi wa kutosha ni wapi kuna dalili za rushwa ambazo ndugu Bernard Kamillius Membe anaweza akahusishwa nazo moja kwa moja zilizotumika yeye kumsaidia mmiliki wa kampuni ya MODSPAN kupata tenda ya ujenzi wa gati hii!?

Lakini kubwa zaidi ni kufeli kwa watoa habari ya suala hili kuweka hadharani Memarts za kampuni hii ya MODSPAN ili watu wajue kama ndugu Bernard Kamillius Membe anamiliki hisa kiasi fulani za kampuni hii.Mwisho tuhitimishe kwamba hizi sio habari za ukweli.

Zimelenga kumchafulia taswira hii ndugu Bernard Kamillius Membe ambaye anaonekana kuwa mwiba mkali kwa wanasiasa uchwara na mafisadi wanaosaka urais na vyeo ndani ya chama CCM.

Ndugu Bernard Kamillius Membe ni msafi pasipo na shaka linapokuja suala la maadili ya uongozi,diplomasia na ukada ndani ya CCM.

Imetolewa na Friends Of Hon. Membe!

Jana niliongea na mtu wa karibu na Mhe Membe,ameshangaa mno namna ambavyo watu hao wanavyojaribu kumhusisha Mh Membe na jambo hilo,ila yote ni Hofu ya wataka madaraka kumuogopa Membe na kujaribu kutengeneza tuhuma Bandia juu yake.Nimefurahi kuona friends of Membe Wameweka sawa jambo hili.Ni ukweli pasi na Shaka rekodi ya membe ndani ya ccm ni safi!
 
Ukweli hutolewa sio kwa mazuri Tu, hata kwa mabaya yake, Hilo lipo wazi kwa Bw. Membe, SI msafi hata kidogo!

lazima ulete data za kuprove,sio unaleta umbeya na uongo,Mtake msitake Membe ni mtu safi ndani ya ccm,mandingo wacha kuharisha,leta data kuprove!
 
Ha ha hili suala lipo wazi sana. Memorundum ama articles za kampuni toka lini zikaandika ushemeji?? Ukweli ni kwamba jamaa amempigia pande shemeji kupata tenda.

weka ushahidi
 
Ni kweli kampuni ya shem!!! Fisadi tu huyu.
 
Jana niliongea na mtu wa karibu na Mhe Membe,ameshangaa mno namna ambavyo watu hao wanavyojaribu kumhusisha Mh Membe na jambo hilo,ila yote ni Hofu ya wataka madaraka kumuogopa Membe na kujaribu kutengeneza tuhuma Bandia juu yake.Nimefurahi kuona friends of Membe Wameweka sawa jambo hili.Ni ukweli pasi na Shaka rekodi ya membe ndani ya ccm ni safi!

Wamuogope kwa kipi? Kafanya nini kwa nchi hii??? Utamlinganisha na Lowasa Sitta, au Slaa??? Uwaziri kapata kwa mgingo wa dada!
 
Hivi be. Membe Ni na nani katika siasa za nchi hii?.. Tatizo alilonalo Ni uwaziri alioupata kupitia mama salma kikwete unaomfanya ajilinganishe na wanasiasa nguli kama Lowassa e.t.c.

CCM kinatoa usawa katika uteuzi wake. Haiwezekani Mhe. Mkapa rais mstaafu atoke kusini na Bw. Membe anaetokea kusini apewe kuwania urais.

This is automatic disqualification.

Bw. Membe hauna chako tena, chukua jembe ukalime na mbwembwe zake zote zinaishia 2015 pale Mhe Lowassa atakapowa rungu kupeperusha bendera ya CCM kwenye urais.

A FRIEND OF LOWASSA.
 
Bado sijashawishika pamoja na kumchafua mzee membe kwa kiasi hiki.tuhuma feki,za kitoto,hazina ukweli.kwangu Mimi bado yeye(membe)namkubali 100000%
 
Back
Top Bottom