Bernard Membe had a Chance but waiting for night dreams to happen made him loose it.

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Mwaka 1963 Dr. Martin Luther King Jr, alisimama mbele ya watu 250,000 kati yao elfu 60 wakiwa wazungu (karibia robo ya waliohudhuria) na kutoa hotuba…I have a dream…

I have a dream that my four little children will one day live in a nation where they will not be judged by the color of their skin but by the content of their character… akaendelea …We have also come to this hallowed spot to remind America of the fierce urgency of now.”, for that “Now is time to make justice a reality for all of God’s children”

Kwa kifupi sana, ndoto ya Dr. Martin Luther King Jr, ilikuwa very very clear. Ikumbukwe, siku moja kabla hajatoa hotuba yake, vyombo vya usalama vilihujumu sound system siku moja kabla. Robert Kennedy mwanasheria mkuu wa Marekani wakati huo, kwa kujua mfumo wa sauti umehujumiwa, aliamuru ifungwe sound system nyingine na “alisimamia show” kuhakikisha hotuba ile inafanikiwa kutolewa. Actually, hotubali ile ilifuatiliwa na watu wengi akiwemo Rais JFK ambae alimsikiza Dr. King Jr kwa mara ya kwanza.

Ndugu yetu Bernard Membe ambae umwekuwa Waziri wa mambo ya nje kwa takribani miaka zaidi ya 7 na katika tenure yako alikuja Rais George W. Bush then akaja Xi Jing Ping wa China, akaja Barack Obama. Yote hii ilikuwa chini ya ushawishi wako kimataifa kama waziri. Tunakumbuka mwenzetu ulikuwa afisa mwandamizi wa ubalozi nchini Canada kabla ya kuja kugombe ubunge.



Wakati mmoja ukihojiwa kupitia kipindi cha dakika 45 ITV kama una mpango wa kuwa mkuu wa “kaya yetu” , ukaepa kwamba kubainisha kuwa nafasi ya Urais huna mpango nayo, unless umeoteshwa. Na kila mmoja aliekuwa akikufuatilia akitaka kusikia lini umeota na umeota nini hakuwahi kusikia licha ya kukuona umechukua fomu 2015. Na basi ndiyo hivyo, mchakato wa kura ndani ya NEC ulikutema. Na hatimae imebaki historia.

Labda ungeweza wazi ndoto yako wazi ili wale wote ambao 2020 wameanza kukupigia chepuo, bila shaka nasi akina Thomaso huenda tukasadiki kuwa you’re serious na you’re in business. Japo nakushauri ndoto yako iwe wazi kwa 2025, maana 2020 sijui utakuwa na nini kipya ambacho atatuambia una nia ya kweli ya kutufanyia ili uwe a real substitute ya Ngosha ambae bila shaka atarejea Chato, japo naendelea kuona 2020, viatu hutaviweza.

Kwa upande mwingine, ifahamike kuwa sisi Watanzania Mwl. Nyerere alitufundisha undugu, basi kuna nyakati pia tunapena ushauri kama ndugu. Huu ni ushauri wa wazi kwako na kwa mwingine ambae anapiga jalamba la 2025. Pengine tukiamua kundoa ukomo kwa mgombea Urais, ili JPM apige kadri awezavyo, basi msijisikie vibaya jamaa akaendelea kupeta. Kwani akina Angela Markel wa Ujerumani, mbona wamekaa vipindi vine na hakuna alielalamika. Tony Blair wa Uingereza, alikaa vipindi viatu, Margareth Thertcher nae hali kadhalika. So, kama sisi Watanzania tutamtaka Ngosha alisongeshe kama anaona kuna mambo anatakiwa kuyafanya, bila shaka kum-beat kwa kura haitawezekana hata kidogo. Ila kwa 2025 kama hatutamua kufuta ukomo wa Uraus, basi chance unayo kwa kuwa u Mtanzania na sasa labda ndoto yako itakuwa ishafahamika waziwazi.

"I Have a Dream" speech, haikubagua dini, rangi na jinsi na iliwaunganisha watu wote waliokusanyika kama kaka na dada wakiunganishwa na imani na values. Walijiona wanaungana kama Taifa kwa kuwa ilikuwa inatoka moyoni (they could feel it in their gut.) What do you have so touching which should make us to beging to think of you as a potential successor?. Na matokeo yake bill of civil right ilipitishwa Marekani.

Sasa basi, ushauri wangu unaanzia hapa… Rejea Marshall Plan kwa ajili ya Ulaya ya Magharibi iliyogusa mataifa 17 na kabla ya Marshall Plan, Ugiriki na Uturuki walikuwa washafaidika na fedha za kufufua uchumi wao pia.

Lengo la Marekani kuwapa fedha Ulaya Magharibi ilikuwa kudhibiti ushawishi wa USSR kwenye ardhi ya Ulaya ambayo ilikuwa na matatizo yafuatayo.
  • Survivors wa vita hawakuwa na makazi, kulikuwa na njaa na hapakuwa na ajira.
  • Mfumko wa bei ulikuwa juu sana na waliokuwa na kazi hawakuweza kumudu gharama za bidhaa na huduma.
  • Viwanda, reli, barabara, madaraja na mifumo ya maji na umeme ikiwa imeharibiwa kabisa.
  • Wakulima walikumbana na ukame na mazao machache waliyofanikiwa kuyafikisha sokoni, wakazi wa mji hawakumudu, maana “wallet” zilikuwa hazisomi.
  • Biashara na mtiriri wa mitaji iliyokuwa inahitajika ili kuimarisha biashara ilikuwa interrupted.
Lengo mahsusi la Marshall Plan, lilitaka kurejesha a “sound economic conditions.” Kati ya 1948 na 1951, major reforms zilifanyika na Uchumi wa Ulaya ikakua kwa 30-40%: na viashiria vya matokeo yalikuwa yanapimika vilikuwa kama ifuatavyo:

Kwa haraka sana chakula kilipatikana cha kutosha, madawa hosptalini na uhakika wa makazi bora.

Kulikuwa na ongezeko la viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo yaliyozalishwa kwa wingi na mipaka ya Ulaya kufunguliwa kukuza biashara kwa kuwa ujenzi wa viwanda, barabara, reli na madaraja vili-facilitate haya kufanyika.

Mwenzetu una advantage moja kubwa. Umekuwa afisa wa ubalozi Mwandamizi na Waziri wa mambo ya Nje kama Rais Mkapa na Rais Kikwete. Ukitumia vyema influence yako kwa kuja na clear Membe Plan unaweza kuvutia mikopo mikubwa ya uwekezaji ambao tutarejesha baada ya kujenga uchumi wetu. Rais Obama akiwa IKULU ya magogoni 2013, alihimiza kufanya biashara kati yetu sisi na Marekani. Kuna vitu vingini kupitia AGOA tunaweza ku-trade na Marekani, mbona South Africa wanapiga hela kwa biashara, mbona Kenya wanapiga hela kwa mauzo ya nje ya bidhaa. They are human beings like us they are only incorporating technology and know-how in their course of doing business to export quality products in the foreign markets. Technology inanunuliwa na know-how kuna potential consultants kwa kutujengea uwezo ili kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa soko la nje ambalo raw materials zipo kwa wingi sana Tanzania.

Bila shaka Watanzania tukakuamini 2025. Vinginevyo, kama Dr. Mahiga bado ana mpango wa kuingia Magogoni kama ulio nao, kwa nafasi yake kama aliyokuwa nayo Waziri Marshall, basi yeye atateleza kiulaini sana wakati wa mchakato 2025.

Seriously, Tanzania inaweza kukopesheka kwa kutumia rasilimali zetu za ndani na Waanzania kuwekeza kwenye major economic projects watu wawe sehemu ya kufurahia neema ya nchi.

Reserves za ndani zikitumika vyema tunaweza kuwekeza katika miradi yenye quick multiplier effect na tukapaa kiuchumi. Ila kama siasa tu za kukomaa bila sisi wapiga kura kujua what are the specific problems you’re aiming to solve, dhu, chances za kuaminiwa zinakuwa very narrow. Na ukizingatia Ngosha yeye ni mtu wa tangible deliverables, una kazi kubwa ya kupandia hapo ili upige kazi. Kimsingi kama una nia njema kuwa Prezdaa, inawezekana kabisa tu, kama utajipanga na kuwa team nzuri, pasipo kumharibia/kumkwamisha Farao wa sasa. Maana kukwishana sio uzalendo; mbegu ya kukwamishana/kuharibiana ikimea ina potential kubwa yak u- reciprocate kitu ambacho sio afya ya udugu tulio nao Watanzania.

Mwisho naomba ku-declaire interest, mimi ni timu Tanzania na kwa sasa namuunga mkono Farao aliepo kwa mujibu wa katiba yetu, taratibu na tamaduni zetu. Ila kwa kuwa suala la kupanga ni kuchagua, kama kweli ndugu yetu Bernard Membe umepanga na kuchagua kuendeleo kuota, njozi yako ikiwa wazi, bila shaka utapata watu wa kukuunga mkono kwa wakati ukifika.

Shalom!
 
Kilichomkosesha Membe ni majungu na kufitiniana baina ya wanamtandao. Hilo ndo limewafanya wote kutupwa nje ya duara
 
Sauti ziliazo nyikani ni nyingi mno na kubwa kiasi kwamba pepo hizi za bahari zinaleta vilio huku nchi kavu. Basi tayarisheni mapito.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom