Samatime Magari
Senior Member
- Feb 10, 2017
- 128
- 474
Juzi Kati camera zime-mumulika Daudi akiwa kwenye Bentley Flying Spur, Moja ya expensive na full sized luxury sedan kutoka kwa Mkoloni huko Uingereza kwa Malikia..
.
Kama wapiga kura tukaitolea macho kumchuzi huku tunawaza ukosefu wa madawati Shule Msingi Nyambitilwa kibondo, Tukapata tags za hapa na pale raia wakiomba kujua undani wa machine ya mtumishi wao..
.
Maana Malawi unaambiwa nchi ni ya wananchi ila wananchi wenyewe hawaelewi kama wao ndo wenye nchi Au nchi ni ya kijani na wao ni wapangaji tu maana mambo upande wao moja wala mbili haiikai.
.
Na sisi tukaona hii chuma isipite hivi hivi bila kukata kiu ya wadau wetu acha tuimulikie kurunzi then tuwajuze Habari zake. Machine inayohusika hapa ni Bentley Flying Spur machine moja makini sana kutoka Bentley Motors Limited...
.
2005 ndo Hii gari uzalishaji ulianza na as of now iko na generation 3. 2005-2013 ndo G1. 2013-2019 2nd generation na 2019-Mpaka LEO hii inakua 3rd generation na hii ndiyo iliyoonekana Juzi na mpigania haki za wanyonge..
.
.
Hii machine ni full sized luxury car na nikisema full sized namaanisha kwanza ina maximum interior spaces with high end comfort, Pili Iko na advanced technology na imetengenezwa kwa premium materials, hapa kwenye material tuna refer leathers, wood, na chuma..
.
Hii gari kwa sedan inachokupa hakuna gari nyingine inaweza kupa Labda the likes kama S Class Benz., Audi A8, Lexus LS, BMW 7 Series and the likes, Ukianzia ndani tu seating the space mbele to nyuma ni ya kutosha. Ndo Maana Daudi na unene wake bado anafit vizuri, Hapa Bongo wakina Gisiemuu ndo wanapush chuma kama hizi.
.
.
Diamond nae kipindi flani alivuta la 2020 lilikua linaitwa Bentley Continental GT W12 ilikua 1.4B Kama sikosea Bei za Ki-Kaole. Ukiangalia interior ukianza dashboard infotainment system steering na button zake kwa kweli ni design za juu sana na hapa sitii neno, Wewe angalia picha tu then utaelewa nachomaanisha ni nini, ubunifu wake ni wa kifahari sana..
.
Siti vina setting option Zaidi ya 15 + vinatunza kumbukumbu. Kuna mtu anajiuliza vinatunza kumbukumbu gani tena hapa, hio nakuachia homework ukishindwa njoo WhatsApp. Hizi siti unaweza adjust siti mbele nyuma juu chini, sukuma mgongo, pandisha headrest, shusha etc na Vinaweza kuku massage, kukupasha joto, kukutia ubaridi
.
.
Hizi siti ndugu yangu zina adjustment mpaka za kiuno [Lumbar support], Sasa kiuno kinakuaje adjusted hilo Daudi anaweza elezea vizuri. Hapo ndani kuna mood lighting yani ukiwa na hasira machine inakuwashia taa za kuku calm, au ukiwa na mbebezi kuna taa zake pia..
.
Na hata taa za Ibada zipo, Inshort NI taa flani za ku control hisia kizungu wanaita mood lighting na haya mambo ni ya ki-masaki masaki sana kama umezoea balbu na gropu unaweza usielewe hapa, achana napo tu...
.
Music bana upo wa kutosha kwanza kuna speaker 10-20 kutokana na toleo husika zikiwa na watts 1500 to 2200 Yale mambo ya underseat sabufa humu hayafai. Music uko na mfumo wa Beosonic unaoatoa music ulio sawa [Clear and balanced sound] usioumiza masikio unaoleta utulivu wa moyo na ukipiga singeli humu mfumo unakataa..
.
Infotainment yake ukiweka vents za AC steering dashboard ni za kipekee sana so far zina muonekanano wa kisasa Zaida katika uzao huu.
.
.
Nyuma katikati ya siti pale iko na refrigerated bottler cooler kwa ajili ya chupa mbili tatu, massage heating na ventilation unapata pia. Control za ubaridi pia unapata bila kusahau kuna screen za inch 10-12 pale nyuma na vitu kama wireless charging na etc.
.
Kwa hii chuma huwezi sikia mtumiaji anauliza kama unacharge type C na kina USB iko na wireless charging system. inshort mambo ni mengi siwezi yamaliza ila nimekugusia muhimu upate ka kitu uendelee kupambania katiba mpya..
.
Ina long wheel base kwa ajili ya kuwa na smooth riding lakini pia ina suspension za upepo [air suspension system]...Hizi za upepo kuna raia wa Discovery huwa wanazitoa wanaweka za Tunguu pale Unguja mambo yasiwe mengi..
.
.
Muonekano wa njee wa kibabe sana kuanzia grilles na taa zake za mbele badge ya gari, exhaust system etc hapa mtu wa Mungu endelea kuangalia picha. Kuna gari uspeciall wake kuzielezea unaishiwa maneno inabidi uwe mtazamaji tu then ujifunze kwa picha...
.
Ndio maana hii machine inaitwa the ultimate driver’s limousine hapa kaiulize AI ina maana gani itakupa majibu. Ukienda kwenye engine huko ndio kuna balaa sio la nchi hii kuna engine option mbili 6.0 L W12 twin-turbo hii na 4.0 L V8 twin-turbo..
.
Hizi mbili ni Petrol engine, Yani cc 5998 na CC 3998 Jichanganye sasa Maana hapo machine ni cylinder 8 nyingine cylinder 12 bila kupepesa jicho. Ziko na hp 680-880 zikiwa linked na gearbox ya 8 Speed AT kutoka Porsche, Hizi ndo GB zenye dual clutch alafu Tiptronic...
.
Yani gear zina shifts extremely fast na unaweza hata usijue kama imebadilika, Imagine Gearbox kubwa kama engine ya Crown wewe ulishaona wapi ?.Hapa gear inadakwa kabla haijatoka nyingine ishaingia na inakupa feeling kama ya gari za mashindano na ukilikanyaga linaamka..
.
.
Koo lake ni kubwa sana so kuhusu mafuta hii halitumii ila linabugia, imagine within 4 second 0-100km hii hapa na gear number 4 unaitafuta, hii acceleration rate sio ya nchi hii. Full tank linakula 90 Litres na mafuta ni 4-5Km/L na sometime inaweza kuwa chini ya hapo au juu kidogo kutegemeana a uendeshaji wako..
.
So dude linakimbia [twin turbo] na top speed ni 320Km/hr na inafikika kipengele ni huku Tunguu uje na barabara yako tu ili uwezi kufika 320. Na usalama wake ni wa hali ya juu imagine gari ina airbag 10 mpaka airbag za goti eti, lakini pia ikisense Ajali inaku alert+braking..
.
Inaitwa Forward Collision Warning (FCW) ikiwa na Emergency brake asssit bila kusahau Electronic Stability Control (ESC) na Traction Control (TCS). Hili kwenye Kona alibinuki labda ubinuke wewe imagine chuma ina ton 2.4, longer wheelbase halafu ina mifumo ya umeme ya stability..
.
Spare part hazipo huwezi enda ilala ukakutana nazo hapo ni mpaka Kuagiza Dubai au UK wanakoyatengeneza huko. Mafundi wapo kwa hapa DSM wako hapo CMC Automobile, huyu ni official dealer wa gari baadhi za UK. Hizi ndo garage unakuta fundi mkuu ni kama branch manager wa NMB kule Masasi so ujipange..
.
.
Hii Machine bana bei yake ni $220K-300K Kama 550M++ kwa Pesa ya Tunguu, Ushuru ni 200-300M so inaweza cheza 800M++...
.
Sasa turudi kwa default mode Kama una mpango wa kuagiza gari zetu Pendwa Subaru Spacio Premio Rav 4 and the likes kutoka Japan, Uk, Singapore T njoo. Tuko na network ya trusted dealers. Dealers wanaotupa gari zenye ubora wa juu kwa discount nzuri so upande wa bei nao uko safi ..
.
Pia tuna uzoefu wa kuspot gari nzuri kwenye sites za Japan gari zenye viwango na grades nzuri maana tunashinda mtumbani kila siku. Tutafanya mchakato wako wa kupata gari kuwa rahisi na salama kwa pesa yako na unaojali muda wako..
.
Simply njoo WhatsApp 0714547598 au ofisini Posta Mpya MUA House 4th Floor mkabala na Mkapa tower tutaku assist + kukushauri..
.
.
Kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari karibu, utatupa hitaji lako tutakupa Ushauri pia then tutakutumia options za gari ukishachagua utapewa invoice...Utafanya malipo at cost [no extra cost] huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo..
.
.
Natumaini umejifunza kitu kama jibu ni ndio basi kwa madini zaidi follow kurasa za jamii instagram X @samatimemagari sasa ili next time usipitwe na haya madini. Pia kuwa karibu na famili hii ya magari save this number [0714547598 Samatime Magari] then share jina lako..
.
Tutasave number yako na utapata ushauri Bure na pia utaona OFA na huduma tinazotoa bure kwa wanafamilia wa Samatime Magari. tunakutakia siku njema ya uzalishaji
.
Samatime Magari
0714547598