Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Bara, Benson Kigaila, ametoa wito kwa watanzania, hususan vijana, kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa kupiga kura ili kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
Akizungumza Agosti 10, 2025 katika kongamano la kuelekea siku ya vijana Duniani, Kigaila amesema ni wakati sasa kwa vijana kutumia kura zao kufanya maamuzi ya msingi kwa hatma ya taifa, badala ya kuwa wasindikizaji wa mchakato wa kisiasa.
“Ni muda wa kufanya mabadiliko, vijana tukitumia nguvu yetu ya kura tunaweza kukipeleka Chama Cha Mapinduzi likizo isiyo na malipo,” Kigaila.
Aidha, amesema kuwa endapo CHAUMMA itapata ridhaa ya kuunda Serikali, italeta mageuzi makubwa kwenye sekta ya elimu kwa kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya msingi hadi chuo kikuu ili kumpunguzia mzigo kijana wa kitanzania na kumwezesha kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
Kwa upande wake, mratibu wa kongamano hilo la vijana, Mkola Masoud, amesema lengo kuu la kongamano hilo ni kuhamasisha vijana kuwa sehemu ya maamuzi ya kisiasa kwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi, badala ya kusubiri kushangilia maamuzi ya wengine.
“Tunataka vijana wasiwe watazamaji wala wasindikizaji wa siasa,Tunataka wawe sehemu ya mabadiliko ya kweli kupitia sanduku la kura,” Masoud.