Elections 2015 Benson Kigaila apinga uteuzi wa Anthony Mavunde Jimbo la Dodoma

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
kihga-620x308.jpg

Mgombea Ubunge jimbo la Dodoma Mjini kwa tiketi ya Chadema, Benson Kigaila

MGOMBEA Ubunge katika jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila amekata rufaa ya kupinga uteuzi wa mgombea ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Anthon Mavunde. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akuzungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Kigaila amesema awali aliweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea huyo kutokana na kutokuwa na sifa za kugombea nafasi hiyo.

"Mgombea huyo hana sifa za kumfanya ateuliwe kugombea nafasi hiyo kwa sababu amekiuka taratibu na kanuni za utumishi wa Umma akiwa yeye mtumishi wa Umma.


"Kwenye fomu yake ya uteuzi kifungu (5) amekiri kuwa yeye bado ni mtumishi wa Umma kwa ngazi ya Mkuu wa Wilaya hivyo Mavuinde hadi anarudisha fomu za Tume 21 Agosti mwaka huu bado alikuwa mkuu wa wilaya jambo ambalo ni kinyume na waraka wa maadili ya utumishi wa Umma.


"Mbali na hilo inaonesha wazi kwamba Mavunde ambaye ni mkuu wa wilaya bado analipwa mshahara na kodi za watanzania wenye vyama na wasiokuwa na vyama," amesema Kigaila.


Alisema kwa mujibu wa Mavunde jinsi alivyojaza fomu ya tume yeye bado ni mkuu wa wilaya na hivyo amekiuka sheria na kuudanganya umma na kukiuka kiapo hivyo hastahili kuwa mgombea.


Hata hivyo Kigaila amesema kutokana na pingamizi hilo alipokea majibu kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma akidai kuwa pingamizi hilo amelitupilia mbali kwa sababu maelezo yake yanahusu watumishi wa umma.


"Nilijibiwa kuwa, kwa mujibu wa waraka wa Rais Na.1 wa Mwaka 2015, 7 Julai, mwaka huu alitoa utaratibu utakaotumika kwa Mawaziri, Naibu waziri, Wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya watakaoamuya kugombea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, kwa mgombea ataketeuliwa na tume ya Taifa ya uchaguzi likizo yake itaendelea hadi Tume itakapotangaza matokeo," amesema Kigaila.


Alisema aliambatanishiwa na barua ya ruhusa ya Mavunde ya kuanzia 11 hadi 22 Agosti, mwaka huu na hiyo siyo fomu ya likizo kwa kuwa mgombea huyo ana muda wa miezi miwili tangu ateuliwe kushika wadhifa wa ukuu wa wilaya na taratibu za utumishi wa umma hapaswi kwenda likizo bali anapaswa kupewa ruhusa hivyo mgombea Mavunde anaruhusiwa kuendelea na mchakato wa ubunge wa jimbo hilo.


Alisema alifika hatua hiyo ya kukata rufaa kutokana na mgombea huyo kwenda kinyume na sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 pamoja na marekebisho yake, waraka wa utumishi wa umma na waraka wa Rais.


"Ndugu Mavunde hajaacha kazi wala kuchukua likizo hadi 21 Agosti mwaka huu siku ambayo Tume ilitakiwa kumteua, na hadi sasa ndugu Mavunde anaomba kugombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini akiwa mtumishi wa Umma (Mkuu wa Wilaya) kinyume na sheria ya uchaguzi, waraka wa utumishi wa Umma na kinyume na waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2015.
 
Safi sana huyo imekula kwake na arudi kwenye ukuu wa wilaya na mwisho wake ni siku ya kuapishwa Rais wa tz EL
 
Kwahiyo hata mawaziri hawatakiwi kugombea?

Sio mawaziri tu,kwa mujibu wa Kigaia ata Rais anapogombea muhura wa pili inabidi aache urais kwanza.

Yaan kwenye kampeni za 2010 kwa mfano,Kikwete angejiuzulu kwanza urais ndio aingie kwenye kampeni na Dr Slaa.Mpumbavu huyu!
 
Sio mawaziri tu,kwa mujibu wa Kigaia ata Rais anapogombea muhura wa pili inabidi aache urais kwanza.

Yaan kwenye kampeni za 2010 kwa mfano,Kikwete angejiuzulu kwanza urais ndio aingie kwenye kampeni na Dr Slaa.Mpumbavu huyu!
Watafute wenzio wakusaidie kufikir maana naona unapata shida sana kwa uvivu wa kufikiri
 
Mavunde amelivundisha, waraka wa utumishi wa umma wa 2015 unaeleza wazi ukichaguliwa na chama cha siasa kugombea nafasi ya ubunge au udiwani basi inabidi uandike barua ya kuacha kazi ya utumishi wa umma.

Ndio maana watu wanaichukia CCM kwasababu wao ndio wanatunga hizo sheria lakini hawazifuati

Yaani sheria ni kwa wapinzani tu, kwa mtindo huu Kenya wataendelea kuwa mbele na Tanzania tutaendelea kusoma nyayo za Kenya
 
Ingwa Kigaila anaweza kuwa na point hawezi kushinda hiyo rufaa. Kwa sababu akishinda itakuwa na madhara karibu nusu ya wahombea. Hata hivyo itasaidia kuwafungua mavjo na kurekebisaha kanunu na taratibu.
 
Watafute wenzio wakusaidie kufikir maana naona unapata shida sana kwa uvivu wa kufikiri

Fikra zangu na zako yawezekana ni kama mlima na kichuguu, kwa akili za Wapumbavu wanafikiri kila cheo ukitaka ugombee lazima uache kazi,sivyo hivyo.

Kwa vyeo vya kisiasa,Rais,Waziri,Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya haviendeshwi kwa masharti ya utumishi ya umma yanayowahusika watumishi wa umma wasio wa vyeo vya kisiasa.Kulinganisha hayo makundi mawili ni tatizo la upumbavu tu.

Kwa mawazo hayo ya kipumbavu wangefikiri ata Obama kuwa alipaswa ajiuzulu kwanza urais kabla hajaingia kwenye kampeni za urais kwa mara ya pili mwaka 2012 kushindana na Romney, ni upumbavu tu.
 
Kumbe kigaila hana akili madevu mengi akili hana mbona hajawapinga na mawaziri sasa jamaa ziro kama sumaye.
 
Kumbe kigaila hana akili madevu mengi akili hana mbona hajawapinga na mawaziri sasa jamaa ziro kama sumaye.

Wapumbavu wenzake wanamshangilia hapa kwa jinsi nao walivyo watupu kama alivyo Kigaila.

Eti analipwa mshahara?nadhan hajui kuwa Mawaziri wote akiwemo majirani zake akina Simbachawene, Nyalandu na wengineo nao pia bado ni mawaziri na wanapokea mshahara mpaka Baraza jipya litakapotangazwa mwezi wa 11.Upumbavu tu.
 
Fikra zangu na zako yawezekana ni kama mlima na kichuguu, kwa akili za Wapumbavu wanafikiri kila cheo ukitaka ugombee lazima uache kazi,sivyo hivyo.

Kwa vyeo vya kisiasa,Rais,Waziri,Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya haviendeshwi kwa masharti ya utumishi ya umma yanayowahusika watumishi wa umma wasio wa vyeo vya kisiasa.Kulinganisha hayo makundi mawili ni tatizo la upumbavu tu.

Kwa mawazo hayo ya kipumbavu wangefikiri ata Obama kuwa alipaswa ajiuzulu kwanza urais kabla hajaingia kwenye kampeni za urais kwa mara ya pili mwaka 2012 kushindana na Romney, ni upumbavu tu.
Mkuu nimekuja kujua kumbe kule chadema kunamapumbavu mengi sana kama wako sahihi kwa mawazo yao mbona mawaziri nao hawajawakatia rufaa hayawezi hata kutofautisha kati ya utumishi wa umma na ule wa kisiasa.
 
Mkuu nimekuja kuju kumbe kule chadema kunamapumbavu mengi sana kama wako sahibi kwa mawazo yao mbona mawaziri nao hawajawakatia rufaa hayawezi hata kutofautisha kati ya utumishi wa umma na ule wa kisiasa.

Kweli Mkapa hakukosea, tuna tatizo kubwa la hiki kitu upumbavu,na bahatu mbaya hawajui na hawajui kuwa hawajui.

Ndio maana Kigaila bila aibu mbele ya kamera eti analalamika Mkuu wa Wilaya na utumishi wa umma unaosimamiwa na tamisemi.
 
Uzima wa mtu aujuaye ni Mungu tu.Sasahv wewe uko mzima umejaa kiburi cha uzima lakini kesho si yako.Ushindi wa

UKAWA ni asubuhi tu kwa nafsi ya Urais

Mtaishia nale nale tu, Ikulu sio hospitali ya rufaa, aende Muhimbili
 
Back
Top Bottom