Benki ya Posta na Ajira za Upendeleo

Benki ya Posta na Ajira za Upendeleo

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,435
Dodoma. Wakati Watanzania waliohitimu vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi wakihaha kutafuta kazi, Benki ya Posta Tanzania (TPB) imeajiri wafanyakazi 40 katika nafasi mbalimbali, huku matangazo ya nafasi hizo za kazi yakitolewa kupitia barua pepe na anuani za ndani za benki hiyo.

TPB iliajiri wafanyakazi hao kuanzia Julai 2012 hadi Aprili 2013 na waliokuwa na uwezo wa kuona tangazo hilo ni wale tu waliokuwa na neno la siri (password) ya barua pepe na anuani za ndani za benki hiyo. Jambo hilo lilitoa mwanya kwa wafanyakazi kuwapeleka marafiki, jamaa au ndugu ili kupata fursa hiyo.

Pia, benki hiyo iliajiri wafanyakazi watatu katika nafasi za juu na kuwalipa viwango vya mishahara tofauti na vilivyoainishwa katika muongozo wa utumishi wa benki hiyo. Ufisadi wote huo umesababisha Sh185milioni kutowekea kusikojulikana.

Hayo yamebainishwa katika ripoti ya ukaguzi wa mashirika ya umma ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka 2012/13, ambapo pia imefafanua jinsi benki hiyo ilivyotumia mamilioni ya fedha kukarabati jengo la benki hiyo na nyumba ya mkurugenzi wake mkuu.

"Ajira hizo zilikuwa zikitangazwa kwa njia ya matangazo ya ndani kupitia barua pepe ambazo zinaonekana kwa wafanyakazi wa ndani tu au mtu husika aliyetumiwa barua pepe ya tangazo," inaeleza ripoti hiyo.

"Mtu yeyote asiye na ‘password' hawezi kuona tangazo hilo. Jambo hilo lilitoa mwanya kwa wafanyakazi kuwaleta marafiki, jamaa au ndugu ili kupata fursa hiyo."

Kuhusu ajira za watumishi watatu ripoti hiyo inaeleza kuwa "mmoja alipewa mshahara wa Sh3.6 milioni kwa mwezi badala ya kulipwa Sh2.4milioni. Mwingine analipwa Sh5 milioni badala ya Sh2.4 milioni na mwingine analipwa Sh5,5 milioni badala ya Sh3.3milioni."

Kuhusu ukarabati wa jengo la benki hiyo tawi la Mkwepu, ripoti hiyo inaeleza kuwa kampuni ya Kiaren Investment ndiyo ilipewa kazi hiyo na kutakiwa kulipwa Sh86 milioni lakini ikalipswa Sh144milioni.

Baadhi ya wananchi wameitaka Serikali kuifanyia kazi ripoti hiyo ya CAG na kuwachukulia hatua wote waliofanya ufisadi huo.

Mytake: Serikali inapaswa kuwa makini na namna taasisi mbalimbali zinavyoajiri watu wake. Binafsi nilipata fursa chache kuomba nafasi zinazotangazwa na benki ya posta. Kwenye matangazo yao wanasisitiza lazima maombi yatumwe kwa mtandao kwenda kwenye email yao! lakini kwa mshangao kila nikituma maombi, system inaniambia hiyo email haipo na kwamba maombi hayajaenda nikapiga simu ikapokelewa na receptionist ambae licha ya kumtaka anielekeze niongee na HR au IT manager yeye alikomaa nimweleze tatizo langu. Nikaona isiwe tabu, baada ya kumweleza tatizo yeye akanijibu eti huwa wanapata hayo maombi yanayotumwa na waombaji mbalimbali (licha ya mimi kupata return email kuwa application haijaenda!). So kuna tatizo kubwa kwenye ajira za hawa jamaa. Nawapongeza ofisi ya CAG kwa kuwabaini.

Source:Mwananchi
 
hii benk ifungwe tu kwani ni moja ya mashirika yanayoiingizia serekali hasara kila mwaka
 
haaaa dawa yao n kukopa nqkusepa bank wakisema watoke mbele nao watatoka kwan! duhhhh
 
Inakuwaje bado kuna ubabaishaji huu wakati tuliaminishwa benk imepata menejiment mpya
 
Sasa hata kama ni matatizo,hayo ni vitatizo vidogo na ungeleta mezani kwetu tungeshughulikia.Kwa kuwa umeleta kwenye mtandao wa kijamii (tena tishio) Hivyo basi kwa niaba ya menejimenti ya TPB hatutatoa nafasi ya kazi kwa wote wenye majina yanayo anza na "M" na tunaanza na wewe masulupwete.


Popote toa kitu,upate kitu!

Msemaji.
 
ha ha ha ha ha ha du tanzania bana ni zaidi ya ujijuavyo aisee
 
hawa posta bank si juzi tu wametangaza nafasi za kazi lakini ukituma maombi kwenye email yao inakataa. Kweli mafisadi
 
Sasa hata kama ni matatizo,hayo ni vitatizo vidogo na ungeleta mezani kwetu tungeshughulikia.Kwa kuwa umeleta kwenye mtandao wa kijamii (tena tishio) Hivyo basi kwa niaba ya menejimenti ya TPB hatutatoa nafasi ya kazi kwa wote wenye majina yanayo anza na "M" na tunaanza na wewe masulupwete.


Popote toa kitu,upate kitu!

Msemaji.


Haa haa haa huwez kuwa siriaz!
 
Hata mimi ni mhanga niliyejeruhiwa na masuala ya ajira kwa benki hii ya posta
 
Back
Top Bottom