Benki ya Dunia yaipongeza Tanzania kwa ukuaji wa uchumi

Ngasere45

Senior Member
Dec 31, 2022
149
565
WAZIRI NCHEMBA AZINDUA CHAPISHO LA 19 LA RIPOTI YA BENKI YA DUNIA

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amezindua chapisho la 19 la Ripoti ya Benki ya Dunia ya Hali ya Uchumi (Tanzania Economic Update-The Efficiency and Effectiveness of Fiscal Policy in Tanzania), katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Rotana, Jijini Dar Es Salaam.

Ambapo Ripoti hiyo, pamoja na mambo mengine, inaonesha Tanzania kufanya vizuri katika maeneo mengi yaliyofanyiwa utafiti ikiwemo kuimarika kwa hali ya uchumi, wenendo mzuri wa utoaji wa fedha kwenda kwenye miradi ya maendeleo, nchi kuwa na hifadhi ya fedha za kigeni za kutosha, kuimarika kwa ukusanyaji wa kodi za ndani, mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara pamoja na usimamizi mzuri wa deni la Serikali na kushauri mambo kadhaa ikiwemo uimarishaji zaidi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kupitia kodi za ndani, usimamizi bora zaidi wa Bajeti Kuu ya Serikali na huduma nyingine za jamii.

Mwigulu.jpg
 
Na hii inflation iliyopo ndo upandaji gan wa uchumi..! Au ndo ile ukiona wb na imf wanakusifia jiulize mara mbili mbili
 
Back
Top Bottom