Benki ya Dunia yaipatia Tanzania dola mil 65

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
BENKI ya Dunia imepanga kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kuboresha utendaji wa Idara ya Mahakama kwa lengo la kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kusogeza haki jirani zaidi na wananchi.

Hatua hiyo ilifikiwa jijini Washington, Marekani jana baada ya Bodi ya Juu ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia kupitia taasisi yake inayoshughulikia utoaji wa misaada na mikopo nafuu kwa mataifa masikini duniani (IDA) kuidhinisha mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 65 kwa Tanzania ili kuweza kusaidia Mpango wa Maboresho ya Mhimili wa Mahakama ili kuongeza ufanisi, uwazi na urahisi wa kupata huduma za Mahakama.

Mradi huo mpya umeainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa na pia katika Mpango Mkakati wa Maboresho ya Idara ya Mahakama wa mwaka 2015-2025.

Kupitia mipango hiyo, Serikali imelenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, kuongeza uwazi, uwajibikaji na kupunguza umasikini.

Mpango wa Maboresho katika Mhimili wa Mahakama utaongeza ufanisi katika utekelezaji wa vipaumbele vya taifa kwa kusaidia kuboresha utoaji wa huduma na pia kuongeza wigo wa upatikanaji wa haki.

“Kuna idadi kubwa sana ya Watanzania ambao kwao upatikanaji wa huduma za kimahakama ni mgumu kutokana na ugumu wa gharama, lakini haipaswi kuwa hivyo kwa vile ni suala muhimu kwa ustawi wa maisha ya jamii na maendeleo ya watu wake,” alisema Bella Bird ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia katika mataifa ya Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi


Chonzo: Habari Leo
 
Sio vibaya kukopa lakini mbona ufanisi au tija ya mikopo mikopo haionekani? Au kuna sehemu mikopo hii inaendekeza?
Deni la Taifa linongezeka na kukopa tunaongeza wakati huo huo hatulipi, kuna jambo hapa.
 
Hatutaki mkopo tena, tunataka kujitegemea huku kichinichini mnaomba mikopo, sasa kaeni kimya maana hatuwaelewi
 
Sio vibaya kukopa lakini mbona ufanisi au tija ya mikopo mikopo haionekani? Au kuna sehemu mikopo hii inaendekeza?
Deni la Taifa linongezeka na kukopa tunaongeza wakati huo huo hatulipi, kuna jambo hapa.

Tija haiwezi kuonekana so long anaekopesha ndie anapanga matumizi. Kulipa tunalipa, japo kidogo kidogo sana.
 
Bila mikopo nchi itayumba kwa sasa! Tupende tusipende! Mkakati uwe kuja kujiteemea miaka michache ijayo! Ila kwa sasa hatuna ujanja!
 
90% ya nchi duniani hukopa so sio ajabu Nasi tukakopa hasa kwenye miradi ya kimaendeleo chukulia wewe mwenyewe bila kipato cha ziada itakuchukua miaka mingapi kujenga nyumba au chumba
 
Alafu kuna mijinga humj ndani ilikua inasema tujitegemee...mara hatutaki misaada ya wazungu...yani ujinga tuu!!! Sasa sijui yakiona huu uzi yatasemaje!!!
 
Mbona kichwa cha habari na content ni tofauti?Umesema WB waipa 65 TZ.Wakati content inasema wamepanga...je marekani wakisema wasipewe?Unajua WB inaongozwa kwa sera za nani duniani?
 
Jana niliangalia kipindi cha mlumbano ya hoja na kuna mchangiaji mmoja kanichekesha sana.
Ametoa mfano eti kuna jamaa alikuwa anaishi kwa mjomba wake anayefanya kazi TAZARA huku akiwa anahangaikia naye kutafuta kazi, baadae akaja akapata kazi kwenye kiwanda cha nondo na akawa analipwa mshahara huku bila kumfahamisha mjomba hivyo mjomba akaendelea kutoa msaada.
Akafananisha hali hiyo na Tanzania kwamba kuna wakati tulikuwa na huitaji wa misaada lakini sasa hivi tunaweza kujisimamia ila tunajifanya tuna shida. Baada ya kupewa misaada tunaitumia kumhudumia V8!

Hii pesa ina masharti yake lakini tunasahau kuwa pesa za escrow tu ambazo imezitoa serikali hiyo hiyo ni karibia mara mbili ya hizi!
 
Hapa mnashangilia, wakisitisha mtasema hatuzitaki, haya ni mambo ya kutiana anibu tu, chagudoa kanyimwa pesa na mtu fulani kaahidi kujitegemea kaja mwingine kumshika mkono, kachekelea mpaka jino la mwisho eti mie wananihitaji sana bwana, hovyo.
 
Alafu kuna mijinga humj ndani ilikua inasema tujitegemee...mara hatutaki misaada ya wazungu...yani ujinga tuu!!! Sasa sijui yakiona huu uzi yatasemaje!!!
Kweli mkuu mijitu pengine ikisha kunywa viroba haijuwi hata inasema mini tz bado sana huwezi kujitegemea ikiwa Watoto ashuleni wanakaa chini huwezi kujitegemea wagonjwa wanalala watu watatu kitanda kimoja huwezi kujitegemea kama maji ya kunywa mnashea na ngombe nchi bado sana hata tz ikiwa miongoni mwa nchi Dona yaani kusaidia itachukuwa miaka 3000 huko ndio ukweli usipo penda saga nyembe ule
 
Back
Top Bottom