Benki ya Dunia yaionya Tanzania kuhusu kuitegemea China

BUSAMUDA

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
612
358
Taarifa za hivi karibuni kutoka katika serikali ya China kuwa Tanzania itapewa kiasi kikubwa cha fedha cha dola bilioni 20 ambazo China imezitenga kwa ajili ya kuzisaidia nchi za Afrika kufanya mapinduzi ya kiuchumi, inaonyesha ushirikiano mkubwa uliopo kati ya nchi hizi mbili.

Benki ya Dunia imeonya kuwa, kuongezeka kwa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na China kunaweza kuathiriwa na kushindwa kukua kwa Beijing.

China ni moja kati ya wabia wakubwa wa biashara na Tanzania na hutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na pia imewekeza nchini. Mwaka 2014 inakaririwa kuwa thamani biashara ya Sino-Tanzania iliongezeka thamani hadi kufikia dola bilioni 2.6 kutoka kiwango kidogo kilichokuwepo mwaka 2000.

Katibu Mkuu katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Adelhelm Meru, alisema Tanzania inatumia nafasi ya mapinduzi ya viwanda China kwa kuhakikisha uwekezaji unafanyika kwenye vitu vitakavyoisaidia nchi.

Aidha aliendelea kueleza kuwa ifikapo mwaka 2020 sekta ya viwanda itakuwa inachangia asilimia 15 ya pato la taifa.



Katika ripoti ya uchumi nchini Tanzania yenye jina, The Road Less Travelled: Unleashing Public-Private Partnerships in Tanzania, Benki ya Dunia ilibaini kuwa kwa miaka ya hivi karibuni uchumi wa China umekuwa ukikua kwa kasi ndogo. Hili ni onyo kwa Tanzania ambayo ushirika wake na Beijing umekuwa ukizidi kila iitwapo leo.

Fedha za China katika miradi ya maendeleo ya Tanzania zimezidi kuongozeka kila baada ya mwaka ikiwa ni pamoja na dola bilioni 1.2, 2013/14-2014/15 kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam. Ripoti ya iwekezaji wa China nchini Tanzania imeongezeka maradufu, unakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 60 kwa mwaka 2013

Kuyumba kwa uchumi wa China kuna weka katika mashaka uchumi wa Tanzania ambapo unategemea sana uwekezaji toka China. Benki ya Dunia ilieleza kuwa kuyumba kidogo kwa uchumi wa China kunaweza kutaiathiri tanzania moja kwa moja au vingine kupitia uwekezaji.

China imechaangia asilimia 10 ya bidhaa zote zinazotolewa nje ya nchi na ni nchi ya tatu kwa kuchukua bidhaa baada ya India na Afrika Kusini.

Chabzo: Swahili times
 
Hao Bank ya Dunia hawana nia nzuri na sisi. Huo uchumi wa China wanaosema unakua kwa kasi ndogo ni kwamba unakuwa kwa kati ya 6%-7%. Kama hiyo ni kasi ndogo na hizo chumi za ulaya zinazokuwa kwa < 2% tusemeje? Au wanataka tushirikiane na Ivory Coast tu labda maana ndio wenye uchumi unaokua kwa kasi
 
Nyie wajinga na malofa tutamtegemea mchina mpaka uchumi wetu ukae sawa na baada ya hapo tutaendeleanaye kama kawa, huo ni wivu kwa mchaina sababu economy yake inaongoza hadi sasa ulimwenguni, maana hata msaada marekani mwenyewe anategemea pale, so na sisi tusemeje?
 
Wanabodi ! Naomba tu kuelimishwa kidogo ! Nadhani kuna ccertain kind of explanation that i am missing !

Hivi ni kwa nini gesi ya Mtwara ilibidi ijengewe bomba kwa gharama kubwa kuletwa Dar es Salam ,ilhali hizi project za Kinyerezi zingeweza fanyikia kule ?

Honestly ningependa kujuzwa ni kwa nini haswa ilibidi ifanyike hivyo ! Nina amini kuna sababu za kiuchumi ila tu mimi sijazijua
 
Hili kwa watz wakawaida hawawezi kuliona labda impaka itokee ndiyo tutaju athari ya kutegemea inchi moja, Nyerere aliposema inchi ya tz haifungamani na upande wowote aliona mbali

mmmmhhhhhhhhhh.....tayari liberalism loaders wameshaanza....
 
Hili kwa watz wakawaida hawawezi kuliona labda impaka itokee ndiyo tutaju athari ya kutegemea inchi moja, Nyerere aliposema inchi ya tz haifungamani na upande wowote aliona mbali
Ndugu Mr Majanga hapo hakuna cha kuhofu, hiyo report imetolewa na watu ambao wapo pro western, Tanzania haiitegemei China ili ikue kiuchumi, ila China ni kati ya nchi ambazo au ambayo imejitokeza kuisaidia sana Tanzania katika miradi ya maendeleo. Sasa hofu kubwa ya watu wa huku western ni influence ambayo China inaweza kuwa nayo katika nchi ya Tanzania, sababu wao wanakata misaada kutokana na hali ngumu za uchumi katika nchi zao, lakini China anaongeza hiyo hawa furahii. Lakini point muhimu ni ya pale chini kuwa nchi zinazo ongoza kuchukua bidhaa Tz ni India na South Afrika, China ni ya tatu, kwa hiyo hizo nchi mbili za mwanzo ndio muhimu kwa uchumi wetu, sababu ndio wanao weza hata kuongeza thamani ya fedha yetu, lakini pia bila kuisahau China sababu ni ya tatu. Hakuna nchi ya western imetajwa hapo. Kwa hiyo bora wakae kimya sababu wanaboa.
 
Back
Top Bottom