Benki ya dunia kuikopesha Tanzania dola milioni 350

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,886
Waziri-wa-Fedha-na-Mipango-Dkt.-Philip-Mpango.jpg


Benki ya Dunia imekubali kuikopesha Tanzania fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mkopo wa Dola Milioni 350 kwa ajili ya Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa Mazungumzo kati yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaye shughulikia Kanda ya Afrika, Makhtar Diop.

Amesema kuwa kukamilika kwa upanuzi wa Bandari hiyo kutasaidia kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa na Bandari hiyo hatua itakayo chochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Makhtar Diop, amesema kuwa Benki yake imefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kukuza uchumi na kwamba Benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa yana fikiwa kwa haraka

Aidha, Makhtar ameishauri Serikali kuongeza ushirikiano kati yake na Sekta Binafsi katika kuchochea biashara na uwekezaji pamoja na kutupia jicho sekta ya kilimo kwa kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo pamoja na kuongeza thamani ya mazao hayo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuondokana na umasikini na kuchochea uwekezaji katika sekta hiyo.


Chanzo: Dar24
 
Na bado ni wakati wa kuwa wazi kama sio tra kukaa kimya na kujisifu wamekusanya pesa za kutosha..
 
Wanakopa mamilioni ya dola huku tuna-rush kuhamia Dodoma,tunajenga airport Chato,n.k

Madeni mengine yangeweza kuepukika au kupunguzwa kabisa.
 
Trump lazima atekeleze ahadi yake ya kutudondoshea mabom ya nyuklia kama alivyoahid wakati wa kampen
 
Kukopa kwa ajili ya kufanikisha miradi ya maendeleo sio kitu kibaya kiuchumi.

Kibaya ni kukopa ili kula, au kukopa ili kulipa mishahara.
 
Kaz kweli halafu wajinga utasikia kila mtanzania anadaiwa
Nidaiwe kwa sbb ya ujinga wa watu wengine. Kuna mambo yalikuwa yanapaswa yafanye taratibu.
VIONGOZI WA AFRIKA NI MIZIGO
 
Kwenye kampeni alisema ''uchumi utaimarika hadi tuwe tunakopesha nchi nyingine''

...........Kwa hiyo sasa hivi kila mtanzania atakuwa akidaiwa Tsh. ngapi? maana mwaka jana kila MTZ alikuwa na deni la laki nane.
 
Wanakopa mamilioni ya dola huku tuna-rush kuhamia Dodoma,tunajenga airport Chato,n.k

Madeni mengine yangeweza kuepukika au kupunguzwa kabisa.
Dar Port: USD 359 million
Bagamoyo: USD 10 billion?
Tanga??
Mtwara??

Then Kama kuna Bagamoyo then why Dar??
Confusing; pesa nyingi mno!!
 
Kumbe kweli hali ni tete kwani ajira 71,496 zilizositishwa tika May mwaka jana ni miezi tisa sasa! Kwa wastani wa kulipwa 600,000/= @ mtu.
600,000 X 71496 X 9 = 386,078,400,000/= hiyo pesa yote imetolewa kwenye mzunguko na kubakia hazina lakini bado hali si hali!! Kweli Hapa kazi tu!
 
Kwanini tujenge au kupanua bandari kwa pesa yote hiyo tsh 0.8 trillion hivi tumeshindwa kuipanua kwa kutumia makusanyo ya hiyo bandari halafu tunasikia mizigo inapungua sasa kwanini tunasolve kizembe yaani biashara wateja wanapungua due other factor wewe unaongeza mtaji pumbavu
 
Kama tunaweza kukopa tirioni 20 + kwa mwaka.......

Maana Yake tutakopa 20 tr×5 = 100 trioni by 2020..............

Deni la taifa litakuwa kwenye 150 trioni........

Wakati wanaokuja kulilipa wanakaa chini halafu unakuja kusema walipe kodi wakati uliwatesa hata wakati Wa kusoma maajabu Africa hayatakaa yaishe..............

85225a14a26a37ba388f4809aef082b2.jpg
6ab0a0d15712ee967cbd18a545d2dceb.jpg
 
Tulipokosa fedha za umeme wa REA walisema to hell na fedha zao..kumbe tunahitaji misaada? Nazishauri nchi za magharibi na mashirika ya fedha wakaze zaidi masharti ya misaada. Tunaweza kujitegemea, why do we still need aid after more than 50 years of independence???
 
Back
Top Bottom